Yanga yavunja ukimya kuhusu kuondoka kwa Fiston Mayele

Yanga yavunja ukimya kuhusu kuondoka kwa Fiston Mayele

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema kuondoka kwa Fiston Mayele ni hatua ya kukua kwa soka ndani ya timu yao na watampata mbadala wake kwa kuwa maisha ni lazima yaendelee.

Mayele mchezaji na mfungaji bora msimu uliopita 2022/23 ametambulishwa rasmi juzi na klabu ya Pyramids ya nchini Misri na kufunga mjadala wa tetesi za kuondoka kwake Jangwani.

Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Saad Kawemba, alisema jana kuwa, klabu ya mpira mambo ya kuuza wachezaji ni kawaida pale ikitokea ofa yenye manufaa zaidi kwa mchezaji hawawezi kumkatalia kuondoka.

“Maisha ndivyo yalivyo leo hapa kesho pale, wanayanga walimpenda na alitufanyia makubwa kwa kushirikiana na we wenzake lakini kujaribu maisha kwingine sio shida,”

“Mayele ataendelea kuwa Mayele tutampata mwingine mzuri ambaye hata kama hatofanana na Mayele lakini atakuwa bora,”alisema Kawemba.

Alisema Yanga imesajili na ina wachezaji wote bora ambao watawavusha katika malengo yao ambayo wamejiwekea.

Katika hatua nyingine Kawemba alisema, msimu ujao wanajua ushindani utakuwa mkubwa ila wanajipanga kuhakikisha wanayatetea kwa mara nyingine makombe yote waliyoyatwa msimu uliopita.

Yanga ilifanya vizuri msimu huo kwa kutwaa taji la mchezo wa hisani, Ligi Kuu, Shirikisho la Azam huku ikifika fainali Kombe la Shirikisho.

MWANANCHI
 
Nadhani klabu yake mama maniena ndo walipaswa kusema kitu,cos alikuwa kwa mkopo tu hapo
 
Back
Top Bottom