Kikosi cha Yanga kimeondoka leo Jumanne Desemba 3, 2024 kuelekea Algeria kwa ajili ya kuivaa MC Alger katika mchezo wa kundi A michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inaenda kwenye mchezo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal nyumbani lakini wakijivunia mastaa wao watano waliokuwa majeruhiwa kurejea.
Your browser is not able to display this video.
Mastaa hao ni Dickson Job, Khalid Aucho, Chadrack Boka, Clement Mzize na Aziz Andambwile.
Taarifa za ndani zinasema tayari Hafidhi Saleh ambaye ni mratibu wa timu amewasili Algeria akiwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa klabu hiyo, Ibrahim Mohamed kuweka mambo sawa.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 7, mwaka huu katika Uwanja wa Ali La Pointe saa 4:00 za usiku.
Yanga na full mkoko havitakiwi kutajwa katika sentensi moja.
Kuweni wazalendo msimwage yale mambo yenu airport ya Dar au ya Algeria ili kuwadhuru wachezaji wa Simba. Ninachojua ni timu moja tu ya TZ itashinda huko Algeria weekend hii na timu hiyo haivai rangi ya majani kibichi.