Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kijana mhadhiri wa historia katika moja ya vyuo vikuu kanifahamisha upinzani dhidi yake jinsi anavyosomesha historia.
Nimemwandikia hayo hapo chini:
WAASISI WA AFRICAN ASSOCIATION 1929 NA AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA 1933
African Association imeanzishwa na Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Rawson Watts na Raikes Kusi mwaka wa 1929.
Viongozi hawa waasisi wa African Association watoe hao Wakristo watatu: Cecil Matola, Rawson Watts na Raikes Kusi wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.
Ikawa sasa Waingereza wanapambana na vyama viwili yaani African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hii ndiyo sababu unaona historia ya TANU ikawa hivi ninavyoihadithia pale ilipokuja kuundwa mwaka wa 1954.
HOFU YA KUANDIKA NA KUHIFADHI HISTORIA YA AFRICAN ASSOCIATION NA TANU
Historia hii baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 ikawa mfano wa jinamizi inawatisha baadhi ya watu.
Wakawa kwanza wanaogopa kutaja majina ya waasisi wa African Association hao ambao majina yao yapo hapo juu na pili wakawa na hofu pia hata ya kuhadithia historia yenyewe ilivyokuwa.
TANU ILIUNDWA VIPI?
Historia ya kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954 imetanguliwa na simulizi nyingi za kusisimua hasa kuanzia mwaka wa 1950 baada ya kuundwa kwa TAA Political Subcommittee ambayo wajumbe wake walikuwa Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdulwahid Sykes (Secretary), Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Hamza Mwapachu, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Kamati hii ina historia kubwa sana.
UPI UKWELI WA HISTORIA YA KUASISIWA KWA TANU?
Sababu kubwa inayonifanya mimi kuwa mbele kupita wenzangu katika kuijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni kuwa kwanza ni uhusiano wangu na wazalendo walioshiriki katika vuguvugu hili la siasa.
Wenzangu wao waliamini kuwa kabla ya Nyerere hapakuwa na harakati zozote dhidi ya ukoloni.
Wenzangu hawa waliamini siasa zilianza na Julius Nyerere mwaka wa 1953 alipochaguliwa kuwa President wa TAA.
Bahati mbaya sana Nyerere mwenyewe katika hotuba yake ya kuaga Diamond Jubilee Hall mwaka wa 1985 hakueleza vipi alichaguliwa na baya zaidi aliwaaminisha wasikilizaji wake kuwa yeye aliikuta TAA katika usingizi na yeye ndiye aliyeiamsha kutoka usingizini.
Hii si kweli.
MAPINDUZI NA UONGOZI WA VIJANA TAA 1950
Ukiisikia historia ya Schneider Abdillah Plantan nini alifanya kuwaingiza vijana katika uongozi wa TAA 1950 na kuutoa madarakani uongozi wa wazee utashangaa.
Vijana walioingizwa katika uongozi ni Dr. Vedasto Kyaruzi (President) na Abdulwahid Sykes (Secretary).
Wazee waliotolewa madarakani ni Thomas Saudtz Plantan (President) na Clement Mohamed Mtamila (Secretary).
Moto huu wa 1950 haukuzimika na ndiyo uliomtia Nyerere katika uongozi wa TAA katika uchaguzi wa mwaka 1953 alipogombea nafasi ya urais na Abdul Sykes.
Schneider Plantan ni mtoto wa Affande Plantan Mzulu kutoka Imhambane, Mozambique aliyekuja Deutsch Ostafrika na Hermann von Wissmann akiwa kiongozi wa jeshi la askari mamluki 400 wa Kizulu kutoka kijiji cha Kwa Likunyi walioletwa kuja kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith wa Pangani.
Watoto watatu wa Affande Plantan ambae kwao alijulikana kama Chief Mohosh Shangaan wana historia yao katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Watoto hawa ni Thomas Plantan, Schneider Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.
Mimi nikiijua historia hii na kumsikia Nyerere anasema TAA iliamshwa na yeye...
Kuna mtu muhimu sana katika historia hii ya Nyerere kùwa kiongozi wa TAA na kisha TANU.
Mtu huyu ni Hamza Mwapachu Mdigo kutoka Tanga na muhitimu wa Makerere College na University of Wales.
Mwapachu ndiye aliyeweka shinikizo kuwa Nyerere ndiye anaefaa kuwa kiongozi wa TAA 1953 na 1954 TANU iundwe aongoze harakati za kudai uhuru.
Hizi si dalili kuwa TAA ilikuwa usingizini.
Yote haya yamo katika kitabu cha Abdul Sykes.
HITIMISHO
Nilibahatika kuzungumza, kusoma nyaraka na vitabu vinavyoeleza maisha ya siasa za waasisi hawa wa TANU waliokuwa New Street Dar-es-Salaam na wengine majimboni: Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Saadan Abdu Kandoro, Germano Pacha, Joseph Kimalando, Julius Nyerere na Japhet Kirilo.
Majina haya yote na yale waliyofanya kama mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika yamo katika Nyaraka za Sykes.
Hawa wanachama 9 ni katika waasisi 17 waliounda chama cha TANU tarehe 7 Julai 1954.