Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Mambo ya kufanya wakati Mnajadili kuhusu Mshahara na Mwajiri wako
Mosi, fanya utafiti kujua je Kwa nafasi uliyoomba wanalipa level ya Mshahara kiasi gani? Hii itakuwezesha kushawishi ulipwe shilingi ngapi kutokana na taarifa ambayo unayo tayar.
Pili, Ni Jambo jema kushukuru ofa ya Mshahara ambayo Mwajiri wako mpya ameitaja,lakini je angalia inakuwezesha kuendesha Maisha yako? Uwe na limit na Mshahara ambao unajua kabisa unaweza kuishi.
Tatu, Kujiamini ndio kila kitu katika majadiliano ya Mshahara, onyesha kutokana na taaluma yako,elimu yako na uzoefu ni Kwa kiasi gani utaweza kuongeza uzalishaji/ ufanisi katika kampuni hiyo na hivyo unastahili kulipwa Mshahara husika unao uhitaji.
Nne, Kampuni nyingi au waajiri wengi huwa na kawaida ya kutaja ofa ndogo ya Mshahara wakitegemea mjadiliane kuhusu malipo,kwahiyo usikubali Tu ofa ya Kwanza Bali nawe shawishi mshahara ambao unakuwezesha kuishi mjini.
Tuje Jambo gani usifanye wakati unajadili jambo la Mshahar na Mwajiri wako
Mosi, Usianze wewe kuleta jambo la Mshahara mezani, Yani swala la mshahara achana nalo kabisa mpaka Mwajiri wao alianze yeye.
Pili, Ukiulizwa je kazi yako ya awali au kazi ya sasa hivi unalipwa shilingi ngapi. Kamwe usidanganye kwasababu wanaweza fanya utafiti na kuijua Hilo hivyo utakuwa umeshajivunjia heshima tayar.
Kutoka kwangu ETUGRUL BEY
Ni hayo Tu!