Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
Tumeshindwa kabisa kukaa vikao vya kichama na kuyamaliza?, tuliolelewa ndani ya chama tunarekodi nzuri juu chama chetu na mifano lukuki juu ya ccm yetu,ambayo inapotokea misuguano basi sisi wana ccm wote kwa pamoja huchutama chini na kukaa pamoja na kuondosha zimwi linalotaka kujitokeza na hatimaye ndani ya vikao vyetu hutoka humo tukiwa wamoja zaidi ya Awali.
Kwa hali iliyopo mkutano wa dharura haukwepeki yaani mkutano wa kikao cha ndani cha kichama,usio na waandishi wa habari,ndivyo tulivyowahi kufanya huko kitambo, Haipendezi sisi wacheza kwata tuliokosa nafasi za kichama tukafahamu kanuni zaidi ya nyie ambao mpo katika mamlaka halali zakiuongozi,
Bungeni pawe mahala pa kuiambia serekali juu ya kero za watanzania hawa,na pasiwe pahala pa kunyoosheana vidole baina ya wana CCM kwa mwana CCM,hii ni fedhea kubwa na si ukomavu katika falisafa za kiitikadi za chama chetu cha mapinduzi.