Yasmine na Fari Ipupa

Yasmine na Fari Ipupa

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,904
Reaction score
8,371
Kwa wale waliohudhuria tamasha alilotumbuiza mwanamziki Fari Ipupa kutoka DRC nadhani watakumbuka akitaja jina na kumwita mwanadada Yasmine ambaye kwenye hilo tamasha alikuwa amekaa kwenye jukwaa la wanamziki ,ni dada ambaye kwa hakika ni kipisi cha mdada mungu kamjalia alivaa gauni jekundu nashinda nikijiuliza je anauhusiano gani na Fari Ipupa hata Fari alipomaliza aliongozana naye na pia sijui huyo mwanadada Yasmine ndiye huyo alipokuja mwanamziki D'banj kutoka Nigeria ndiye anatajwa kuwa huyo kijana wa Kinigeria amewehuka kiasi cha kumchukua mwanadada huyo mpaka Nairobi kutumbua maraha na alienda huko na wapambe wake,kama ni yeye sijui anawadaka vipi hao maselebu wa muziki.Tafadhali mwenye CV ya huyu dada atudokolee kidogo nataka nami nkauze shamba langu Visiga ili nimtafute Yasmine teh teh
 
hahaha na wewe kisa tu unataka kuponda starehe Vip na Mwanadada Olivia mwimbaji wa Marekani ambaye Fally Ipupa kajiopolea ?
 
Jamani itabidi niwe mwanamziki sasa,Fally chiboko siku akina dada walivyokuwa wanajipeleka ni kama mbwa kwa chatu lakini match winner akawa Yasimine,ah nilitaka kusahau nao mapedeshee wa town walivyojifanya wanavijisenti huko kutunza ili mradi wapaishwe ilionyesha watu walivyo malimbukeni na hivyo vijisenti hao akina Ndama mtoto wa ng'ombe sijui kama huko kwao wanatoa hivyo vijisenti kusaidia jamaa zao,mi naona ni ulimbukeni tu unawasumbua watu waliopata vijisenti kwa njia za kitapeli na ambao hata abc ya shule hawana
 
Back
Top Bottom