econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Tangu kifo chake mwaka 2004, kuna sintofahamu ni kipi hasa kilimuua Kiongozi wa zamani wa Palestina Yasser Arafat. Kuna nadharia nyingi juu ya kifo chake, wengine wanadai aliuaawa na wengine wanadai alikufa kifo Cha kawaida.
1. Nadharia ya kwanza: Aliuawa.
Wengi kwenye nadharia ya kwanza wanadai ya kwamba Yasser Arafat Aliuawa na maadui zake wa kisiasa. Kwamba baada ya kukataa offer ya Waziri Mkuu wa Israel wa Ehud Barak mwaka 2000 ya uwanzishaji wa mataifa mawili ya Israel na Palestina, shida ilianzia hapo.
Inadaiwa ya kwamba Yasser Arafat alidhamiria ya kwamba ili Taifa la Palestina lianzishwe basi inabidi wakimbizi wote wa kpalestina waliofurumushwa kutoka Israel warudi kwenye maeneo yao kwanza ndani ya Israel ndipo Sasa wakubaliane kuanzisha nchi mbili za Israel na Palestina. Msimamo huu ndio chanzo Cha uadui na hata kuuawa.
Kwenye nadharia hii inadaiwa na wapelelezi wa kifaransa ya kwamba Yasser Arafat Aliuawa kwa sumu aina ya Polonium 210. Wapelelezi Hawa wanadai ya kwamba, sample ya mkono iliyopatikana kwenye chupi ya Arafat ilionesha ya kwamba ilikuwa na kiwango kikubwa Cha Polonium 210. Ingawa ni nani hasa alimwekea sumu hiyo hakuna ajuaye. Wengine wanadai ni mke wake wa ndoa, wengine wanadai ni Israel na wengine wanadai ni mahasimu wake kutoka Palestina.
2. Nadharia ya Pili: kifo Cha kawaida.
Kwenye nadharia ya Pili ya kifo Cha Arafat, inasemekana Alikufa kwa maradhi ya kawaida ingawa inashtusha kidogo. Mwaka 2007, Daktari binafsi wa Yasser Arafat, ajulikanaye Kama Dr Ashraf Al Kurdi, alidai ya kwamba walipopima damu ya Arafat waligundua Ina virusi vya HIV. Ingawa Daktari huyo anadai pamoja na damu ya Arafat kuwa na HIV ila hakufa kwa maradhi ya UKIMWI Bali maradhi mengine kabisa. Majibu ya Dr Al Kurdi yameleta mabishano mengi Sana, ni Kwa vipi afe kwa ugonjwa mwingine kabisa usiohusiana na HIV? Na je ni kweli sample ya damu yake haikuchezewa kuleta majibu yanayoonesha alikuwa ameambukizwa HIV.
Mpaka Leo kifo Cha Yasser Arafat kimekuwa kigumu kujua kilisababishwa na Nini.