Yatokanayo na usafiri wa bodaboda

Yatokanayo na usafiri wa bodaboda

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Yatokanayo na bodaboda;
  1. Ukipanda boda boda unakuwa sehemu ya pikipiki kama mzigo
  2. Ukibebwa na mwendesha pikipiki mwenye mawenge nawewe unasomeka waruwaru mkipita wote mnaonekana pipa na mfuniko.
  3. Ukibebwa na mwendesha pikipiki mfupi kwenye utelezi au mchanga jiandae kuagushwa
  4. Endapo mtakutana na mgambo awapige rungu, basi mgongo wako ndiyo utakaopigwa rungu
  5. Dereva wa bodaboda akitukanwa mkiwa pamoja kakubeba, tambua tusi hilo linawahusu wote!
Hivyo shiriki kuilinda heshima yako kwa kupanda bodaboda iliyokamilika kwa kuzingatia usafi wa dereva, umahiri, Uvaaji Helemet pia ukifika kijiweni chagua pikipiki yenye (Side mirrors) inayo mrahisishia dereva kuona ya nyuma msije gongwa kwa nyuma au kusukumiwa mtaroni!

Ni hayo tu!!
 
Madereva wa bodaboda wakiona mwanamke mwenye makalio makubwa wanageuka na kuwasikia umeona mzigo ule[emoji15].



Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Hata mseme vipi kazi ya bodaboda siiachi leo nilikumbatiwa na mshangazi mmoja huyo hatari alikua anaogopa kuanguka barabara nzima ni miluzi tu
Mume wake angeona angenishikia bastola
 
Hata mseme vipi kazi ya bodaboda siiachi leo nilikumbatiwa na mshangazi mmoja huyo hatari alikua anaogopa kuanguka barabara nzima ni miluzi tu
Mume wake angeona angenishikia bastola
Na ukimshusha kijiwe kingine wahuni lazima tukwbia asanteeee baba kwa kutuletea zigooo
 
Joto la tank linaleta uhanithi baadae,harufu ya petrol inaleta uchizi
Ndio maana wanaanza kula mafao kabla ya kustaafu. Wanazichakata kweli kweli na hawachagui yeyote wanabeba tu kama abiria maana wanajua mwisho wao uko karibu..
 
Ndio maana wanaanza kula mafao kabla ya kustaafu. Wanazichakata kweli kweli na hawachagui yeyote wanabeba tu kama abiria maana wanajua mwisho wao uko karibu..
Ooohhhh
 
Hakuna kosa kama piki piki iyumbe then abiria uweke mguu chini yani lazima mle mzinga, au piki piki iyumbe then dereva ushike brake yaani mzimga ni huu hapa.

Piki piki chombo cha ajabu sana, [emoji23]
 
Back
Top Bottom