Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23]Kwa hapa nchini unajitafutia matatizo nenda Kongo ila angalia usije ukapigwa
NimekuelewaSheria
Ni sawa, ila yeye anaonge kama nani? ni mtaalamu wa soka?Kwenye hili niko na makonda hatuwezi kuanza kuwabeza wachezaji kila mtu kujifanya mchambuzi
Nimeukumbuka ule uzi wako wa tafsiri zitokanazo ktk picha.Hahahaaa macho huongea
Kuna mbulu mmoja hivi anaitwa Paul mwaka wa sita sasa sijamuona akiniletea tena sijui alikamatwa akafungwa ?Hata mimi nayahitaji ndugu yangu hasa mwakani
kujipaka nyara ya taifaZimepita dakika nne tangu siku mpya ianze... Ni saa sita na dakika nne... Usiku tulivu kabisa... Kwangu mimi ndio kumekucha lakini kwa wengine wengi ndio muda wao wa kupumzika, kupumzisha mwili na akili...
Taifa stars... Yaani timu yetu ya mpira wa miguu ya Taifa la Tanzania ndio gumzo kwasasa kutokana na hatua iliyofikia kwenye mashindano ya mpira Afrika.. Ni hatua ambayo timu yetu haijawahi kuifikia kwa miaka 40 hivi... Kwa hiyo ni sawa na kipofu aliyeona kwa mara ya kwanza....
Ukame unapotamalaki kwa muda mrefu sana kisha ghafla mvua ikanyesha kuna mengi ya kusimuliwa yatatokea...
Timu yetu imefika hatua ya kucheza katika mashindano makubwa ya Afrika kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka arobaini.. Miaka mingine yote tuliangukia pua pamoja na maandalizi mbalumbali... Kipofu hatimaye kaona.... Ukame wa muda mrefu hatimaye mvua imenyesha.... Jambo hili kubwa limenivutia nami nisiyejua lolote kwenye kabumbu kusema lolote... Ni haki yangu jamani
Natambua una hamu ya kufahamu kuhusu mafuta ya mnyama Simba na jinsi yalivyohusishwa na timu yetu ya Taifa... Taifa stars... Kuwa mpole.... Jambo hili kubwa limekuja na mengi... Yameshasemwa mengi na bado mengi yatasemwa.... Mazuri na mabaya.... Bahati mbaya sana yanayosikika sana ni mabaya... Hii ndio asili ya kiumbe mwanadamu.... Hebu twende kwa uchache wa mengi yaliyosemwa na makundi ya wawakilishi wa jamii
1. Wanasiasa ; kwa bahati mbaya sana uono hafifu wa kimtazamo, itikadi na uhalisia na kuifanya siasa ndio kila kitu kwenye maisha ya mtanzania... Timu yetu ya taifa ikatekwa mazima na wanasiasa... Na kama kawaida yetu kwenye kila kitu, wajuzi, wataalam, mafundi na walimu wa soka wakawekwa kando... Siasa ikashika hatamu hasa baada ya kuona timu ilipofikia...
Wabunge 30 taslimu.. Asilimia 90 wakiwa hawajui ABC za soka wakaenda na timu Misri yanakofanyika mashindano... Yani ghafla hawa wakawa muhimu kuliko mashabiki na wataalam wa soka.... Kilichotokea ninini? Wakapigana ugenini hata kabla ya mechi ya kwanza..... Nuksi no moja hii...!
2. Wachambuzi uchwara; kama nilivyotangulia kusema... Siasa imepora fikra zetu, mitazamo yetu, maono yetu, utashi, uelewa na utambuzi wa mambo muhimu
Ghafla baada ya kichapo cha kwanza toka kwa wasenegali lawama za kwanza zikaelekezwa kwa kocha
. ghafla akabatizwa jina la kocha mbovu kuwahi kutokea Tanzania [emoji1241]
Mambo muhimu kama
Ushiriki wa mara ya kwanza (ugeni)
Umahiri wa timu pinzani
Maandalizi hafifu
Bajeti
Ushirikishwaji wa wataalam wa soka nknk havikuzingatiwa kabisa.... Tulicheza na timu ambayo kwenye viwango vya soka imetuacha mbali kiubora kwa mbali mno karibia nafasi mia moja.... Kuishinda timu kama hii kulihitaji muujiza mkuu....
3. Watabiri bandia : jambo kubwa huwa na makubwa pia... Wameibuka viongozi wa kidini maarufu kama manabii na nitume... Nao hawajaachwa nyuma kwenye hili... Yule mchungaji wa Amber Rutty kaibuka na maono makubwa juu ya ushindi wa taifa stars... Lakini hataki kuyatoa hapa... Anaitaka serikali imgharamie kila kitu kuanzia viza, usafiri, malazi, chakula na posho aende Misri iliko timu akatoe maono yake
4: Wataalam wetu wa soka... Hili kundi limekaa kimya ama sauti zao zimemezwa na wanasiasa au wamewasusia.. Lakini pia pengine wanasubiri wa kubwabwaja wamalize ili sasa wataalam waongee kitaalam na kwa vigezo....
Muda unanitupa MKONO, hebu tuachane na hayo makundi kwasasa tuongee kuhusu mafuta ya mnyama Simba
Kama ilivyo nguvu na umahiri wa Simba mbugani na nyikani akijulikana kama mfalme asiye na mpinzani, basi hata kiroho ana nguvu ileile... Kumbuka maisha ya nuruni ni replica ya maisha ya rohoni... Yaani haya ni matokeo tu lakini asili ya yote ni ulimwengu wa roho
Kwa kulitambua hilo binadamu kajiongeza na kumtumia Simba na mazao yake kimwili na kiroho pia
Kinyesi cha Simba ni kinga ya mambo mabaya
Ngozi yake ni kiwakilishi cha ukuu, mamlaka nguvu na utawala... Wafalme wengi walipendelea kuvaa ngozi ya Simba kama kiwakilishi cha ukuu na nguvu.......
Kucha zake pia huvaliwa kama silaha ya kiroho... Hii huwa na tafsiri ya kujenga kinga na uhodari wa kupambana....
Ukiachana na vingine vyote.... Mafuta yake ndio kiboko... Ukitaka uwe
Jasiri
Mahiri
Kuogopeka
Katili
Roho ngumu/mbaya
Mwenye kiburi
Mwenye majivuno nknk basi jipake mafuta ya Simba.. Hakikisha ni mafuta ya Simba jike na dume ili kumiliki nguvu zote mbili...
Inapofikia mtawala haoni kuwa jambo fulani haliwezi kwenda bila fulani.... Inapofikia hata wakuu wa mihimili mingine kumgwaya mtu mmoja... Basi tambua nguvu ya mafuta ya Simba kwenye muktadha huo.... Sijazungumzia nguvu na ubabe wa Simba mbele ya yanga....
Alamsikini... Nimeandika mada hii kwa muda wa lisaa na dakika nane kamili....
Aliwahi kukuletea? [emoji44][emoji44][emoji44]
Hapana hayakuwa halisi.... Hayapatikani kirahisi hivyo... Na asingeweza kamwe kukamatwa