Tetesi: Yawezekana hiki ndio kilichopelekea Kinana alalamikie Traffic

frankkilulya

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2022
Posts
590
Reaction score
1,494
Mh Kinana kakerwa na Trafiki huenda alipita hii njia kutokea Njiapanda hadi Arusha wanajipanga hivi.

Njiapanda - 4
Uchira - 4
Kawawa - 8
Mjohoroni - 2
Kiboriloni - 6
Changbay - 5
Kibosho - 4 na mmoja wakike mkalii
Mali Sita - 8
Machame - 4
Kwasadala - 11
Boma - 16
Kwa wasomali - 4
KIA - 4
King'ori - 2
Kikatiti - 6
Maji ya Chai - 12
USA - 16
Leganga - 4
Makumira - 4
Tengeru - 8
Kwa Mrefu - 8
Ngulelo - 4
Kimandolu - 4
Kwa Shabani - 6
Philips - 8
MountMeru - 2
Sanawari - 2
Mianzin - 6
Stand Kuu - 12

Ukichomoka wote hawa katambike.

😁😁😁😁😁😁
 
Very risk Road ndio maana ina huu wingi wa Askari
 
Pana haja ya kufanya sensa ya polisi kujua wapo wangapi traffic, FFU, upelelezi nk. Kwa mtaji huu, yawezekana traffic ni unnecessarily wengi!
 
Cc: RPC Kilimanjaro
: RPC Arusha
 
Kinana anacheza na akili za wananchi na wabongo walivyo wavivu kutafakari wanapatikana kweli kweli. Alichofanya Kinana ni kutafuta umaarufu kwa kukemea kitu ambacho anajua ni kero inayosumbua watu wengi. Watanzania tulivyo bongolala tutaanza kuimba sifa na mapambio ila ukweli tatizo halijaondoka ila limetulizwa kwa muda tu na baada ya siku hadhaa hali itarudi kuwa mbaya zaidi. Katu mtu kama Kinana hatagusa yale mambo muhimu yenye kuleta mabadiliko ya kweli na ya moja kwa moja bali atagusa hapa na pale ili kutafuta umaarufu.
 
uwekezaji kwenye teknolijia ungesaidia kuondoa huu uwingi wa traffic polisi na wengi wangeenda kwenye majukumu mengine.

Njia panda pale HIMO to ARUSHA to NAMANGA to BABATI kuna ugumu gani wakufunga road camera's kuangalia muenendo wa barabara na speed camera ambazo by automatic zinaregister faini kwenye system.

Ukifunga hizo cameras unaweka road patrol with 2 police kila 300km's, road patrol wanakuwa controlled na control room.

Hizi issue za speed na ujinga ujinga barabarani watu wanakutana na mafaini ya mamilioni ya hela, na mtu akiwa ticketed mara tatu per month tuna burn driving licence for 5yrs..
 
Hawa wapo kukusanya pesa tu ingekuwa wana lengo la kuzuia ajali wangetumia scientific approach za kitehama
 
Agenda yao ni kukusanya 2000, huo usalama kwao siyo agenda
 
Ila hawa jamaa wanapenda rushwa aisee. Sijui kama watakuja kuacha. Ukiwakuta na zile mashine zao, yaani ni full mikwara!

Ukigoma kutoa elfu 10, unaandikiwa faini ya elfu 30!
 

Jambo la maana kwa waungwana haijalishi nani kawa na ujasiri wa kulisemea.

Alichokisema Kinana ni dhahiri ni moja ya kero zilizo kuu nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…