Sawa tukubaliane na ushuhuda wa majirani kuhusu kijana Hamza aliyeuawa na polisi baada ya yeye kuwaua polisi wawili na mlinzi moja, ukitazama tukio lilivyokuwa kupitia video zilizorekodiwa, utaona kuwa huyu bwana alikuwa na uwezo wa kutumia mashine gun au silaha nzito ya kivita, haya mafunzo aliyapata wapi?
- Alipita JKT?
- Alifunzwa Mgambo?
- Wakati anafungwa kutumia pistol alifundishwa kutumia na silaha ziingine?
- Kupitia picha mbali mbali zinazotumwa kupitia mitandao ya kijamii, inaonekana Hamza alikua kijana wa UVCCM, alikuwa kwenye kambi za ukakamavu za vijana akafunzwa huko?
Haiwezekani mtu hajawahi kushiriki vita yeyote from now where tu atumie silaha za kivita. Mbaya zaidi alionekana kushambulia na kukwepa mashambulizi ya askari halafu alikua shabaha.
Hamza alifunzwa na nani kutumia AK47?
Hili swali mpaka sasa halijapata jibu.