Yeke Yeke!!...

Yeke Yeke!!...

Washaanza kupika nyama kwa ajili ya Magumalu sasa sijui kama atarudi huku maana mapishi yakiwa bomba unajua tena watalala huko huko
Nitamsubiri as long as i takes!Leo mpaka kieleweke!
 
Hachomi mahindi mtu hapa!Kitaeleweka tu!
 
Yaani baada ya kusoma nimemwomba dj anipigie hapa bar. Amenipigia nikakumbuka zamani.
 
Hongera kwa kusikiliza Congo,mwenzio nimekumbuka mbali sana leo!
 
Dogo huo wimbo wa alfa blond hauitwi Jamaica,unaitwa Afriki!
sermon!bakenjula ayayayayaya.......jamaica eyaaaa afriki yeyeye yeyea jamaika eyaaaakibwagizoning'amalayani ning'amalayani
 
mnakumbuka wimbo ule wa shabba ranks km analia nimeusahau jina lake! kuna binamu yangu yupo anaishi mitaa ya magomeni kagera alikuwa mpenzi sana wa Shabba alinunua hiyo tape hiyo akaiweka kwa sauti kubwa shabba analia, majirani wasije nini eti wanakuja kutoa pole wanadhani kuna msibaa hahahaaaa shangazi yangu akapandwa na hasira akaitupa huko hah ting a ring a ling shabbaaaaaaaaaaaaaa!
 
kabla ya yekeyeke kulikuwa na kitu kinaitwa WAGADUDU!(ougadougou) kikikuwa ni ala tupu haimbi mtu humo.
 
dah mmenipandisha mzuks mnakumbuka enzi za nyimbo za ki south? akina tchiko sello twala, chakachaka! na wengineo! hiyo ilikuwa 84-88. 1984 niko songea mkomboti ya chakachaka ipo juu balaa wakati ule ikifika miezi hii kunakuwa na sherehe za komunio ya kwanza na vipaimara! kwa wakatoliki basi kila house karibu utakuta kuna sherehe. ile mnaenda church pale kwa father Hunja miaka ile kanisani MATOGORO akina mama njiani wanahanikiza kwa nyimbo tamu tamu utasikia LELU KUONJA, LELU KUONJA KUONJA KUONJA yaani leo kuonja kwa mara ya kwanza ekaristi takatifu! mkitoka kwenye misa nje mnakuta ngoma za kumwaga sijui beta, ligwamba, ligihu lizombe haya mkitoka hapo mnarudi home, wakati ule hakuna family wanamiliki gari ni GAMA tu mkuu wa mkoa ndo ana range na mandolini, na magari ya serikali, mwendo wa maandamano tu na udongo mwekundu wa songea mnafika wekundu. jioni sasa kila house wanaweka disco hapo basi nyimbo zilizokuwa zinatamba ni za chakachaka na hao wengine. ikipigwa mkomboti kila mtu na kisonjo cha ugimbi anasimama kwa style yake anayarudi. dah ilikuwa raha mnooooo
 
weeh eiyer umeanza zamani eeh,teh teh! naupenda sana huu wimbo,tatizo maneno yake siyajui so inabidi nisiuimbe hadharani manake!sijui hata niliupata wapi!

Wimbo wa yekeyeke uliwahi kuwa maarufu sana mwishoni mwa miaka ya 80, kipindi hicho mie bado kijana mdogo. Kwa wanaoukumbuka wimbo huu, napenda ku-share taarifa zifauatazo:

Mwimbaji:
Jina la mwimbaji wa wimbo huo ni Mory Kante, mzaliwa wa Guinea. Alizaliwa(29 Machi 1950) ktk familia ya wanamziki na elimu ya awali ya mziki aliipata Bamako Mali(Kwa shangazi yake).Akiwa Bamako, alijifunza kutumia Kora, hiki ni kifaa cha mziki (a large harp-lute) Mwaka 1971 alijiunga na Railband, ambako aliimba na Salif Keita. Mwaka 1978-1983 alikuwa Abidjan baada ya kuachana na Railband. Akiwa huko alijifunza ala nyingi za asili, wakati ambao wanamziki wengi wa afrika wakikimbilia zana za kisasa kama gitaa na keyboard. Baada ya hapo akawa anaishi Paris, ambako ndiko yekeyeke alikopikwa.

Mafanikio ya Wimbo wa YekeYeke:
Yekeyeke iliweka historia ya kuwa moja ya nyimbo za kiafrika kuwahi kuuzwa kwa wingi zaidi (takribani nakala 1.5m). Pia wimbo ulishika nafasi za juu ktk chati mbalimbali duniani, ikiwemo chati ya Billboard kwa nyimbo za kiafrika. Unaweza kuusikiliza wimbo wenyewe kupitia youtube-tafuta mory kante yekeyeke.

Mashairi ya wimbo:
Bi sounkouroun lou la donkégna, aha
Bi sounkouroun lou la donkégna, aha
I madji I ma yélé
I kanan n'bila nara ro
N'bo n'**** bila
Kanfalani yana sara le ila

Yékéké nimo yé ké yé ké
Yékéké nimo yé ké yé ké

Bi kamberen lou la donkégna, aha
Bi kamberen lou la donkégna, aha
I madji I ma yélo
I kanan n'bila nara ro
N'bo n'**** bila
Gnin kisse gbela serra le ils

Yékéké nimo yé ké yé ké

Ké woyé boli lalé n'na doni kassi kan
Woyé boli lalé (Hey, hey! )

Ké woyé boli lalé n'na doni kassi kan
Woyé boli lalé (Hey, hey! )

I kanan n'bila doni kassi kan
Woyé boli lalé (Wo dén té soron)
Nyé n'ta sorona kono mi ma ta I yonfé (Wo dén té soron lonkéléna)
Sini Mory la diyandé
Timba bara wouloukounta
Souba ma kata I yala
Ah sara lila

Yékéké nimo yé ké yé ké
Yékéké nimo yé ké yé ké (Djely mousso ni kédjou to wara bo)
Yékéké nimo yé ké yé ké (M'ba mofila téma yan féou)
Yékéké nimo yé ké yé ké
[ Lyrics from: Mory Kante - Yeke Yeke Lyrics ], info source:
 
Tafsiri ya Yekeyeke kwa kiingereza ...
You're my own little movie star
I've found you
you are my superstar
the number 1 in my heart

If you do not kiss me now give
that's a sin
This is a solid happy ending
and our new start

hey you
I'm crazy for you
hey you
you're such a nice pretty face
your little summer trials

yeye ye Yeke
Yeke Yeke yeye
Yeke yeye
Yeke Yeke yeye

you play the leading role
n a fairytale
I have invented
you are my prince super
I'm your princess

you are the first of my
love wins
You're just what I wanted
I love you

hey you
I'm crazy for you
hey you
you have such a nice pretty face
your little summer trials

yeye ye Yeke
Yeke Yeke yeye
Yeke yeye
Yeke Yeke yeye

The first sweet nothings

My little brother
 
Back
Top Bottom