Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema Marekani na Israel zimechanganyikiwa baada ya kuona nchi za kiarabu zikiungana dhidi yao,
Tamko hilo amelitoa baada ya wanajeshi wa Houth kuzishambulia meli za kivita zinazoongozwa na meli ya USS Harry Truman ikiwa ni siku moja tu tangu Donalda Trump atoe amri ya kushambuliwa kwa Yemen kwa kile alichokiita kutaka kuishambulia tena Israel kuhusiana na Gaza.
Katika maelezo yake kwenye mtandao wa kijamii waziri huyo amesema njia inayotumiwa na Yemen ndio njia pekee ya kuondosha dhulma ni hiyo ya mapambano.
Mapema hapo juzi baada ya kutoa amri ya kushambuliwa kwa mamlaka ya Yemen chini ya Houth,raisi Trump alikiri kuwa huko nyuma jeshi lake lilipata hasara kadhaa kutokana na mashambulizi yaliyofanya na Houth ijapokuwa muda uliopita wote nchi yake ilikuwa ikikanusha mashambulizi hayo kuleta athari yoyote kwa meli zao za kivita.