Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Huku viongozi wa Marekani wakitoa matamko ya wazi ya utayari wao kuisaidia silaha zaidi Israel na kivitendo imeshasogeza meli za kivita kwenye bahari ya mediteranean karibu na Israel..
Viongozi wakubwa wa mataifa ya Yemen na Iraq wameionya Marekani dhidi ya uingiliaji kati wake huo.
Huko Iraq Hadi al-Amiri ambaye ni kiongozi wa kundi kubwa la Badri lenye mafungamano na Iran,amesema watu wake wanafuatilia kwa karibu kauli na uungaji mkono wa taifa hilo kwa Israel.
Na huko Yemen kiongozi wa kikundi cha Houth kilichoilazimisha Saudi Arabia kuingia nayo mkataba wa kusitisha vita baada ya kuishambulia nchi hiyo mfululizo naye amesema wataanza tena kutumia droni zao kushambulia popote penye maslahi ya Marekani.
Kule Iraq mwaka juzi na mwaka jana wanamgambo waliweza kuvurumisha makombora kwenye kambi za kijeshi za Marekani yaliyoleta madhara makubwa kwa kambi hizo.