Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 14,762
- 32,386
Wanaendelea Kubweka. ISRAEL HACHEKI NA WOWOTE. ANAKUPIGIA POPOTE ANAPOTAKA. WAULIZENI IRAN WANAELEWA HILI JAMBO.
Wizara ya mambo ya nje ya Yemen imesema kuwa shambulio la Israel “linadhoofisha juhudi za kikanda na kimataifa zinazolenga kumaliza vita dhidi ya wananchi wa Palestina” na “linakwamisha juhudi za amani” zinazokusudia kutatua suala la Palestina.
Wizara ya mambo ya nje ya Algeria imesema kitendo cha Israel cha uchokozi ni “cha kikatili” na kimeonesha dunia kwamba “mnyakuzi hana mwelekeo wa amani, haoni kikomo cha ujeuri na kiburi chake, na hapuuzi thamani, kanuni na masharti ya msingi yanayoshikiliwa na mataifa ya dunia.”
Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, amesema matukio ya leo yako “ndani ya mfululizo wa mashambulizi yanayofanywa na Israel” na yanaonesha dhamira yake ya kuvuruga juhudi zote zinazofanywa kuleta utulivu na usalama katika eneo hilo.
Soma Pia: Israel yashambulia makao makuu ya viongozi wa Hamas nchi Qatar
Oman imeonya kuhusu hatari ya “ongezeko hatari la mivutano linalotishia usalama na uthabiti wa eneo na kuliondoa katika njia ya amani.” Pia imeitaka jumuiya ya kimataifa “kubeba wajibu wake wa kimaadili na kisiasa” na kuzuia ukiukaji zaidi unaofanywa na Israel.