Kumbuka maneno yako, be careful with your words. Natambua wewe ni mtoto wa miaka ya hivi karibuni maana hakuna taifa lililowahi kusifiwa kama ni kiboko wa USA kama Iraq.
Middle East Taifa lenye nguvu za kijeshi na ambalo linaogopewa ni Iran pekee! Kwa kutambua nguvu zao ndio maana tangu late 70 walipigwa vikwazo baada ya Ayatollah kumpindua kibaraka Mfalme Shaha,bahati mbaya sana pamoja na vikwazo,Irani chini ya utawala wa Ayatollah imezidi kua na nguvu zake binafsi kwa kuzalisha kila kitu ndani yenyewe,hata silaha hatari inazomiliki ni matunda ya Teknolojia yake..
Hakuna USA wala Israel wanaoweza kuanzisha vita rasmi dhidi ya Iran kwa sasa,sana sana kuvizia kufanya mapinduzi ya kiutawala (wameshajaribu mara kadhaa kupitia maandamano na kulaani mfumo wa utawala kwa kutumia vibaraka wa ndani na wakashindwa)
Iraq unayoisema isema ilipigwa na Marekani chini ya utawala wa George Bush Jr, pengine haujui kua Iraq ilishapigana na USA na NATO na wakashindwa kumtoa Sadam,late 90s raisi akiwa Bush Sr,Iraq ikawekewa vikwazo lukuki jeshi lake likawa dhaifu kwani tofauti na Iran, Iraq ilikua inategemea silaha kununua kutoka Ulaya na USA- baada ya jeshi kudumaa,miaka 20 mbeleni USA akaja na NATO wakamuua Sadam na kuweka kibaraka wao mpya!!
Yote kwa yote,wazungu wapo middle East kwa ajili ya mafuta na gesi maana ndio uhai wa uchumi wa nchi zao na dunia nzima na OPEC 70% ya mafuta ni kutoka middle east.
Irani ni kinyume chake,kila kitu anatengeneza mwenyewe,vikwazo vimewakomaza na kuwakuza!