Saudi Arabia imeacha kushambulia Houthi majuzi 2022 ndio unataka kusema Saudi yenye majority Sunni tiyari iko pamoja na Houthi Washia wanaopewa silaha kwa Iran?
Kinachowaunganisha Waarabu kwa sasa ni Israel kuishambulia Gaza. Wengine wanajiona aibu, wanahisi watatengwa inabidi waishi kinafiki waikatae Israel. Ila Israel ikiacha mashambulizi Gaza, hao Waarabu wana ugomvi wa ghafla ghafla.
Qatar wanakuwa neutral kidogo ila wanatajwa kuhusika kidogo na Al Shabaab wa Somalia, na ndio walikuwa wadhamini wa Muslim Brotherhood hadi Saudi Arabia na Egypt zikawatenga.
UAE hiyo hapo ina mkono Sudan kwenye civil war.
Iran na Uturuki sio Waarabu ila wanajihusisha nao mambo mengi. Mara Uturuki inaishambulia Syria, mara Iran inalazimisha influence Iraq na Syria ili kuweka buffer dhidi ya mahasimu zake.
Egypt, Syria na Jordan huwezi walaumu kuwa makini, waliwahi pigwa hivihivi kwa sifa za kijinga. Hawa Waarabu wengine kina Saudi walivaa kanzu wakala upepo wakatoa msaada wa maombi na fedha kidogo huku Jordan, Egypt na Syria zinapigana zikashindwa. Kama wanataka na wao Qatar, Algeria, et al wapeleke majeshi yao yawapiganie Palestina. Nani anataka kufanywa chambo.
Jordan iko safe ikiwa upande wa Israel kuliko hao Waarabu wengine, kwanza ni trade partner wake mkubwa. Then Israel inaheshimu makubaliano yao, Syria na Iraq ziliwahi ishambulia Jordan kisa Wapalestina zaidi ya milioni wanaoishi uko na wasumbufu kama ni kwao vile. Waarabu wanataka kuiua Jordan kisa Wapalestina, ungekuwa royal family ya Jordan ungekubali?
Lebanon hiyo Wapalestina wameiua kiuchumi. Egypt yenyewe inawakataa inawajua.
NEMA ina mambo mengi yanafichwa na headlines za Gaza.
Mengi ulioongea ni propaganda ambazo hazina ukweli,na sijui mkuu hizi stori umezipata wapi!?
Aiseee!
*Saudi Arabia sababu ya kuishambulia Yemeni ni kwasababu ilitaka kumsimika Mansour asalie kuwa kiongozi wa Yemeni,Houthi waligoma na kupambana mpaka 2021 waliposuluhishwa Iran akiwemo,balozi za Iran na Saudi Arabia zikafunguliwa.
Walichoulizwa Houthi wanataka nini walisema hawataki USA inteference in Yemeni through Saudi Arabia.
Ugomvi ukaisha na mpaka sasa Iran officials na Yemeni Officials wanaenda Saudi Arabia na wanakaribishwa.
*Alshabaab hawakuwahi na hawadhaminiwi na Qatar,huu uongo wa wazi,Alshabaab waliwahi kuwa na uhusiano na Alqaeda ya Osama bin Ladain,silaha sasa hivi wanapata kwa kuvamia serikali na kwa black market na kwa piracy,kama Qatar wangekua wanahusika kwanini Alshabaab wafanye piracy kupata kipato??
Na ugomvi wa Alshabaab ni wa kikabila pale Somalia,wanataka kabila lao ndio liongoze Somalia,sasa ugomvi wa kikabila unahusu nini Qatar?
Muslim Brotherhood ya Morsi ilikua inatawala Egypt,sasa unaposema Qatar ilikua inaifadhili Muslim Brotherhood kiasi Egypt ikaitenga unanishangaza,maana Muslim brotherhood ilikua ikiitawala Egypt kupitia Muhammed Morsi kabla ya Elsisi kumpindua Morsi kupitia usaidizi wa USA.
Civil war ya Sudan ni ujinga wa serikali ya Sudan na kundi lake la mercenary RSF,msisingizie mataifa ya watu yaliyotulia huko.
*Iran haikuwahi kulazimisha kuweka buffer Syria na Iraq,bali kuna viongozi wengi wa Iraq wanaikubali Iran.
Tukija Syria Bashar ndiye aliyehitaji usaidizi wa Iran ila Iran haikumlazimisha Bashar aungane naye.
Na Iran ilipeleka jeshi Syria kwaajili ya kuzuia makundi hasimu dhidi ya Bashar La Assad baada ya Assad kutaka na kuridhia.
*Turkiye haiishambulii Syria bali kundi la PKK la wakurdi wanaosumbua amani ndani ya mipaka ya Syria na Turkiye.
*Palestina haikuwahi kuua uchumi wa Lebanon,uchumi wa Lebanon una sababu nyingi ya kuporomoka ikiwemo vita ya Israel na Hizbollah 2006
Kuhusu Iraq kuivamia Jordan nitaenda kufuatilia.
Waarabu sababu ya kuungana sio tu kisa Gaza,bali washajiona hawako salama wakiwa chini ya mbawa za USA na Israel.
Ndio maana wameanza kuisogeza karibu Iran,hakuna mwaka Qatar iliwahi ikaribisha Iran kufanya maonesho ya silaha ila baada ya vikwazo vya silaha kuisha dhidi ya Iran,mwaka huu Qatar kaikaribisha Iran kufanya maonesho ya silaha.
Pindi Houthi inashambulia Red sea meli zinazopita kuelekea Israel hakuna mwaarabu aliyelaani hata mmoja na Oman alikataa bandari yake itumike dhidi ya Houthi.
Saudi Arabia alikataa kwenda kinyume na Houthi na alikaa pembeni.
Unadhani waarabu wajinga?
Unadhani hawakumbuki aliyoyafanya USA na Israel 1958 pale Syria kwa kutengenesa crisis??
Unadhani hawakumbuki Muammar Gaddafi na Saddam Hussein walivyogeukwa??
Unadhani hawajui kuwa USA ndio iliyofadhili kupinduliwa kwa Muhammed Morsi??
Wanajua yote ndio maana wanajitahidi kuangalia wanarudije pamoja kama arab league.