Yericko aelewe Adui wa CHADEMA ni adui wa MBOWE. CHADEMA ni moja ya Legacy ya Mbowe na sidhani mbowe ni Mjinga kiasi atake ife

Yericko aelewe Adui wa CHADEMA ni adui wa MBOWE. CHADEMA ni moja ya Legacy ya Mbowe na sidhani mbowe ni Mjinga kiasi atake ife

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Mbowe hata awe na hasira kiasi gani. Bado hawezi kuukata mtoto WA mwanaye kisa ameunyea.

CHADEMA ni moja ya Mambo ambayo yamempa heshima Freeman Mbowe.

Mwenyekiti Mbowe ametumia ujana wake wote kuikuza na kuieneza CHADEMA hapa Tanzania.

Asilimia tisini ya watu hapa Tanzania na nchi jirani, tumemjua MBOWE kupitia CHADEMA.

Mimi kama Mtibeli nafahamu Mbowe ni mtu mwenye utulivu, akili, na mwenye uwezo. Ninaamini hata kete ya yeye kugombea uenyekiti mwaka Jana hakupenda.
Ni aidha kwa shinikizo, au kwa kulaghaiwa na Machawa wanaonufaika na uenyekiti wa Mbowe.

Katika watu waliomuabisha Mbowe na kutaka kumvunjia heshima Mwenyekiti Mbowe, ni wale waliomshauri aendelee kugombea.

Mwenyekiti Mbowe ni miongoni mwa Wazee katika nchi hii ambao Mtibeli nimejifunza baadhi ya mambo kutoka kwake katika mambo ya kisiasa. Hasa siasa za mipango, mikakati na kusogeza kete kuelekea kingi.

Kama Mbowe unahasira au namna yoyote inayokufanya ususe au ukate tamaa. Basi elewa kuwa Baba hasusi.
Bahati nzuri wewe ni Baba na huenda ni Babu katika familia yako.

Adui wa CHADEMA kisayansi na kihistoria atakuwa ndiye Adui wa MBOWE.

Kwa sababu mafanikio ya CHADEMA ni legacy kwa Mbowe. Kuanguka kwa Chadema ni kuangusha Legacy ya Mbowe.

Naamini, ikitokea Chadema imekuja kushika Dola. Mbowe atakuwa miongoni mwa watu watakaofurahia rekodi hiyo. Hata familia Yake, watoto na wajukuu watajivunia Jambo hilo.

Kwenye suala la CHADEMA kwa Mbowe ni ishu Personal. Ishu binafsi.

Haya
 
Kwa ufupi n kwamba chadema n mali ya Mbowe?
 
Anachofanya Msusi kina baraka ya Mbowe ,ukitaka kujua hilo angalia maneno ya James Mbowe na Ukimya wa Mbowe.
 
Chadema ya Mbowe kuna ujanja ujanja mwingi sana ,hata ile ishu ya akina Halima yule Mzee anajua ninikilitokea sema ni wale wamama wametunza heshima yake ndogo iliyobakia.

Kuna riwaya Yangu inatitle "nitakufa na heshima Yangu"
I
 
chadema ya sasa yamoto sana ccm ijiangalie taratibu inageuziwa kibra
 
Nachojua CHADEMA ndo imempa Maisha makubwa mbowe .

Yaani kiufupi ndo ilikuwa biashara yake kubwa .

Kwahiyo kuukosa uenyekiti kwake ilikuwa hasara kubwa .

Chauma ni script iliyoratibiwa na Mbowe mwenyewe .

Kwahiyo ameijenga Chadema na chadema imemjenga yeye is about win , win situation.
 
Hamjambo!

Mbowe hata awe na hasira kiasi gani. Bado hawezi kuukata mtoto WA mwanaye kisa ameunyea.



Kwenye suala la CHADEMA kwa Mbowe ni ishu Personal. Ishu binafsi.

Haya
ni muhimu sana chadema kufanya na kufikiri siasa za kistaarabu zinazojali utu na heshima ya kila moja, na sio kutwa kucha kujadili visasi na visa vya kujengeana lawama na dhana ambazo hazina athari zozote kisiasa, kijamii au kiuchumi.

nadhani ni vizuri sana kujadili masuala muhimu ya taifa letu kuliko kung'ang'ana na kushabikia watu ambao kwa namna moja ama nyingine wameshatekeleza wajibu wao kwa taifa hili.

wewe je?
wajibu wako kwa taifa lako ndio hizi porojo ama?🐒
 
Hamjambo!

Mbowe hata awe na hasira kiasi gani. Bado hawezi kuukata mtoto WA mwanaye kisa ameunyea.
Kwa hiyo Chadema waliunyea mkono wa Mbowe?
CHADEMA ni moja ya Mambo ambayo yamempa heshima Freeman Mbowe.

Mwenyekiti Mbowe ametumia ujana wake wote kuikuza na kuieneza CHADEMA hapa Tanzania.

Asilimia tisini ya watu hapa Tanzania na nchi jirani, tumemjua MBOWE kupitia CHADEMA.
Inawezekana lakini wengi tu (hasa vijana wa mjini Dar) walimjua kabla hajaingia kwenye siasa.
Mimi kama Mtibeli nafahamu Mbowe ni mtu mwenye utulivu, akili, na mwenye uwezo. Ninaamini hata kete ya yeye kugombea uenyekiti mwaka Jana hakupenda.
Ni aidha kwa shinikizo, au kwa kulaghaiwa na Machawa wanaonufaika na uenyekiti wa Mbowe.
Hakuna mtu mwenye ubavu wa kumshinikiza Mbowe. Mbowe aliamua kugombea kulinda heshima yake baada ya kuchafuliwa sana na kambi ya aliyekuwa makamu wake ( akiwemo Msigwa). Aidha, kelele za kumtaka asigombee ndio zilimfanya agombee maana asingefanya hivyo historia ingesema kuwa alimuogopa Makamu wake. Mbowe aliona ni bora ashindwe akipambana kuliko kwa kufyata mkia.
Katika watu waliomuabisha Mbowe na kutaka kumvunjia heshima Mwenyekiti Mbowe, ni wale waliomshauri aendelee kugombea.
Hakuwa na choice. Strategy ya kumchafua na kumtaka aachie ngazi ndio kulimfanya agombee. Waliomvunjia heshima ni wale walio mpakazia na kumuita msaliti aliyelambishwa asali na Abduli. Hao pamoja na viongozi wenzake walionyamaza wakati vijana wa mtandaoni wana mtukana. Kuna wengine walifikia hatua ya kumuita muongo. Hao ndio waliomvunjia heshima.
Mwenyekiti Mbowe ni miongoni mwa Wazee katika nchi hii ambao Mtibeli nimejifunza baadhi ya mambo kutoka kwake katika mambo ya kisiasa. Hasa siasa za mipango, mikakati na kusogeza kete kuelekea kingi.
Sawa.
Kama Mbowe unahasira au namna yoyote inayokufanya ususe au ukate tamaa. Basi elewa kuwa Baba hasusi.
Bahati nzuri wewe ni Baba na huenda ni Babu katika familia yako.
Ndio mnajua sasa? Hili jambo ni dogo. Waliomtukana na kuendesha vita dhidi ya waliokuwa kwenye kambi yake ndio wanastahili kumuomba msamaha. Yeye hana shida nao kama alivyoonyesha katika msiba wa mkwe wake. Viongozi wa sasa wasimame hadharani, na wauambie umma kuwa Mbowe hakuwahi kulamba asali na sio msaliti. Wasipofanya hivyo, vijana wao wataendelea kumtukana na kumvunjia heshima wakati wao wanaangalia. Wawakemee wakina Hilda na wawaambie ukweli kuwa Mbowe sio saizi yao. Wasipofanya hivyo, atakuwa na haki ya kujikita kwenye biashara zake na sio siasa.
Adui wa CHADEMA kisayansi na kihistoria atakuwa ndiye Adui wa MBOWE.

Kwa sababu mafanikio ya CHADEMA ni legacy kwa Mbowe. Kuanguka kwa Chadema ni kuangusha Legacy ya Mbowe.
Mbona humu kila siku wimbo ni kuwa Mbowe aliwachelewesha na alikuwa anaihujumu Chadema! Chadema ikianguka legacy yake itabakia pale pale maana wote wanajua alipoifikisha. Sasa hivi adui wa Mbowe wako ndani ya Chadema. Hao ndio wanaotakiwa kuhakikisha Chadema inaendelea kusimama ili kuonyesha kuwa Mbowe aliwachelewesha.
Naamini, ikitokea Chadema imekuja kushika Dola. Mbowe atakuwa miongoni mwa watu watakaofurahia rekodi hiyo. Hata familia Yake, watoto na wajukuu watajivunia Jambo hilo.
Mbowe atafurahia kwa sababu itatimiza ndoto zake za kuing'oa CCM.
Kwenye suala la CHADEMA kwa Mbowe ni ishu Personal. Ishu binafsi.

Haya
Sidhani kama ni ishu personal. Mbowe ni pragmatic. Hata Nyerere aliwahi sema kuwa CCM sio mama yake. Hivyo hivyo kwa Mbowe. Sidhani kama ataendelea kuing'ang'ania Chadema kama ataona dhahiri kuwa inaenda kubaya na hakuna ambae yuko tayari kumsikiliza. Ataweza kufanya vifuatavyo:
a) kukiachia kife bila kufanya lolote.
b) Kujaribu kukijenga upya kama wanachama wake watamuomba.
c) kujiunga na kukijenga chama kingine cha siasa kama alivyofanya Maalim.
Yote hayo yanawezekana. Uamuzi ni wake na hamna wa kumshurutisha.

Amandla...
 
Kwa hiyo Chadema waliunyea mkono wa Mbowe?
a wa kumshurutisha.

Amandla...

Nyerere hakuwa muasisi wa TANU.
Waasisi wa TANU Wanajulikana.
Nyerere alialikwa tuu.

Mbowe ni miongoni mwa vijana wa mwanzoni kabisa katika kukijenga CHADEMA.
So huwezi mfananisha Mbowe na Nyerere katika mambo ya Kichama.
Nyerere lazima aseme CCM/TANU sio Mama yake kwa sababu alishakikuta chama kipo zaidi ya miaka 20 kinaendelea na harakati zake.

Alafu Kingine hakuna anayemshurutisha ajihusishe na CHADEMA au asijihusishe.

Nilichoandika ni maoni binafsi, na jinsi Mbowe anavyotakiwa akione CHADEMA.

Inaonekana wewe ni miongoni mwa waliomshauri aingie kwenye kinyang'anyiro ili apatwe na aibu iliyompata.

Mcheza Ngoma mzuri jukwaani ni Yule anayejua Muda sahihi wa kuondoka.

Kwamba agombee ili isionekane anamuogopa Lisu😂😂 yaani kuna watu mnawaza kwa namna ya ajabu Sana.
Sasa Mbowe Mwenyekiti, amewakuza hao kina Lisu, Lema, Zitto, Mnyika, Msigwa. Leo Mbowe afikirie mawazo ya kitoto kama hayo kwamba nitaonekana nawaogopa.

Awaogope kwa Lipi? Watu aliowalea yeye mwenyewe. Aliowapigania yeye mwenyewe. Leo agombee ionekane hakuwaogopa😆
Sidhani kama hiyo ingekuwa sababu ya maana.
Ninyi mlimpotosha. Mliamua kumvunjia heshima yake.

Siku aliyoitisha Press nilimuona. Hakuwa na nia ya kuendelea na uenyekiti. Na kama angekuwa na NIA angesema Siku ileile na sio mpaka akajifikirie.

Suala la kuvunjiwa Heshima;
Kama mimi ningekuwa Mbowe watu wakwanza kuwaona wamenivunjia Heshima ingekuwa ni Wale wanaonishauri niendelee kugombea huku wakijua jukwaani nipo kwenye peak na Natakiwa kuondoka watu wakiwa kwenye kilele cha kunihitaji.
Hao ndio waliomvunjia Heshima.

Kama Mbowe asingegombea unafikiri angerushiwa maneno ya kashfa na wapinzani wake?
Kuambia yeye nu Mugabe, au Museveni wakati yupo kwenye CHADEMA yaani chama cha demokrasia na maendeleo hiyo pekee sio heshima.

Nyerere mwenyewe alikuwa smart alijua wakati wa kung'atuka.
Unang'atuka wakati watu wanakuhitaji. Hiya inakulindia heshima na thamani
 
Mbowe hakua na mpango wa kugombea uenyekiti .

Alishawishiwa na matapeli wapenda nyama na bia za bure kama akina Yericko Nyerere

Wenyewe wanakuambia alikuwa anampango.

Hivi mtu kama Mbowe, mfanyabiashara, mkubwa, kiongozi wa upinzani kwa miaka 20, anauzoefu wa kutosha, aitishe Press ashindwe kusema atagombea au hatagombea. Mpaka akajifikirie.

Ni kwamba hakutaka kugombea.
Kwa sababu hakuwa na sababu ya kuchelewesha jibu ambalo amekuwa akiliishi kwa miaka 20
 
Nyerere hakuwa muasisi wa TANU.
Waasisi wa TANU Wanajulikana.
Nyerere alialikwa tuu.
Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka 1953. Kabla yake Rais wa TAA alikuwa Dr. Kyaruzi. TAA ilibadilishwa kuwa TANU mwaka 1954 wakati Nyerere akiwa bado ni Rais wake. Sasa, shehe, tuambie nani alimkaribisha Rais wa TAA kujiunga na TANU?
Mbowe ni miongoni mwa vijana wa mwanzoni kabisa katika kukijenga CHADEMA.
So huwezi mfananisha Mbowe na Nyerere katika mambo ya Kichama.
Nyerere lazima aseme CCM/TANU sio Mama yake kwa sababu alishakikuta chama kipo zaidi ya miaka 20 kinaendelea na harakati zake.
Uongo mwingine. Nyerere hakuikuta TANU bali TANU ni matokeo ya uongozi wake wa TAA akishirikiana na wanachama wengine.
Alafu Kingine hakuna anayemshurutisha ajihusishe na CHADEMA au asijihusishe.
Kuna maandiko mengi humu ndani ambayo yalimtaka Mbowe aachie ngazi na asijishughulishe na mambo ya Chadema. Mbowe aligoma kufanya hivyo.
Nilichoandika ni maoni binafsi, na jinsi Mbowe anavyotakiwa akione CHADEMA.
Wewe ni nani kumtaka Mbowe aione Chadema kwa namna unayotaka wewe?
Inaonekana wewe ni miongoni mwa waliomshauri aingie kwenye kinyang'anyiro ili apatwe na aibu iliyompata.
Mbowe hakupata aibu. Mpaka sasa namna alivyoendesha ule uchaguzi
unatumika kama mfano wa kuigwa. Na yeye kukubali matokeo ni mfano mwingine kwa viongozi wa vyama vya siasa. Badala ya aibu, Mbowe amejionyesha kuwa ni mtu wa integrity ya kiwango cha juu.
Mcheza Ngoma mzuri jukwaani ni Yule anayejua Muda sahihi wa kuondoka.
Sio kwa kufukuzwa. Mbowe ameondoka kwa kushindwa katika uchaguzi wa wazi na wa halali. Ule ndio ulikuwa muda sahihi wa yeye kuachia ngazi.
Kwamba agombee ili isionekane anamuogopa Lisu😂😂 yaani kuna watu mnawaza kwa namna ya ajabu Sana.
Sasa Mbowe Mwenyekiti, amewakuza hao kina Lisu, Lema, Zitto, Mnyika, Msigwa. Leo Mbowe afikirie mawazo ya kitoto kama hayo kwamba nitaonekana nawaogopa.

Awaogope kwa Lipi? Watu aliowalea yeye mwenyewe. Aliowapigania yeye mwenyewe. Leo agombee ionekane hakuwaogopa😆
Kulikuwa na shinikizo kubwa la kumtaka asigombee. Unadhani wafuasi wa Lissu wasingesema kuwa hakugombea kwa sababu alimuogopa Lissu. Kugombea kwake ndio kumethibitisha kuwa hakumuogopa.
Sidhani kama hiyo ingekuwa sababu ya maana.
Ninyi mlimpotosha. Mliamua kumvunjia heshima yake.

Siku aliyoitisha Press nilimuona. Hakuwa na nia ya kuendelea na uenyekiti. Na kama angekuwa na NIA angesema Siku ileile na sio mpaka akajifikirie.
Yote ya kufikirika. Mbowe sio mtu wa kukupuruka. Alijua uamuzi wake wa kugombea jinsi ungeathiri familia yake na wafuasi wake ndio maana akachukua muda wa kushauriana nao. Ni ishara ya ukomavu.
Suala la kuvunjiwa Heshima;
Kama mimi ningekuwa Mbowe watu wakwanza kuwaona wamenivunjia Heshima ingekuwa ni Wale wanaonishauri niendelee kugombea huku wakijua jukwaani nipo kwenye peak na Natakiwa kuondoka watu wakiwa kwenye kilele cha kunihitaji.
Hao ndio waliomvunjia Heshima.
Unajirudia rudia.
Kama Mbowe asingegombea unafikiri angerushiwa maneno ya kashfa na wapinzani wake?
Wangeshindwa vipi kumkashifu wakati walianza kumkashifu akiwa bado ni Mwenyekiti wa Chadema?
Kuambia yeye nu Mugabe, au Museveni wakati yupo kwenye CHADEMA yaani chama cha demokrasia na maendeleo hiyo pekee sio heshima.

Nyerere mwenyewe alikuwa smart alijua wakati wa kung'atuka.
Unang'atuka wakati watu wanakuhitaji. Hiya inakulindia heshima na thamani
Nyerere hakutukanwa kama alivyotukanwa Mbowe. Heshima ya Mbowe ingepungua kama angeondoka kwa sababu ya matusi. Yeye alibaki, akaendesha uchaguzi wa haki na wazi na aliposhindwa akaondoka. Ajabu ni kuwa pamoja na kuondoka kwake bado mnamfuata fatal kinafik. Kwa ninj mnamfuatilama kama mnaamini alijikosesha heshima kwa kuto kung'atuka? Si muacheni aendelee na maisha yake pamoja na aibu yake?

Wanafik wakubwa!

Amandla...
 
Back
Top Bottom