Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
- Thread starter
- #21
Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka 1953. Kabla yake Rais wa TAA alikuwa Dr. Kyaruzi. TAA ilibadilishwa kuwa TANU mwaka 1954 wakati Nyerere akiwa bado ni Rais wake. Sasa, shehe, tuambie nani alimkaribisha Rais wa TAA kujiunga na TANU?
Uongo mwingine. Nyerere hakuikuta TANU bali TANU ni matokeo ya uongozi wake wa TAA akishirikiana na wanachama wengine.
Kuna maandiko mengi humu ndani ambayo yalimtaka Mbowe aachie ngazi na asijishughulishe na mambo ya Chadema. Mbowe aligoma kufanya hivyo.
Wewe ni nani kumtaka Mbowe aione Chadema kwa namna unayotaka wewe?
Mbowe hakupata aibu. Mpaka sasa namna alivyoendesha ule uchaguzi
unatumika kama mfano wa kuigwa. Na yeye kukubali matokeo ni mfano mwingine kwa viongozi wa vyama vya siasa. Badala ya aibu, Mbowe amejionyesha kuwa ni mtu wa integrity ya kiwango cha juu.
Sio kwa kufukuzwa. Mbowe ameondoka kwa kushindwa katika uchaguzi wa wazi na wa halali. Ule ndio ulikuwa muda sahihi wa yeye kuachia ngazi.
Kulikuwa na shinikizo kubwa la kumtaka asigombee. Unadhani wafuasi wa Lissu wasingesema kuwa hakugombea kwa sababu alimuogopa Lissu. Kugombea kwake ndio kumethibitisha kuwa hakumuogopa.
Yote ya kufikirika. Mbowe sio mtu wa kukupuruka. Alijua uamuzi wake wa kugombea jinsi ungeathiri familia yake na wafuasi wake ndio maana akachukua muda wa kushauriana nao. Ni ishara ya ukomavu.
Unajirudia rudia.
Wangeshindwa vipi kumkashifu wakati walianza kumkashifu akiwa bado ni Mwenyekiti wa Chadema?
Nyerere hakutukanwa kama alivyotukanwa Mbowe. Heshima ya Mbowe ingepungua kama angeondoka kwa sababu ya matusi. Yeye alibaki, akaendesha uchaguzi wa haki na wazi na aliposhindwa akaondoka. Ajabu ni kuwa pamoja na kuondoka kwake bado mnamfuata fatal kinafik. Kwa ninj mnamfuatilama kama mnaamini alijikosesha heshima kwa kuto kung'atuka? Si muacheni aendelee na maisha yake pamoja na aibu yake?
Wanafik wakubwa!
Amandla...
Nyerere hakutukanwa kwa sababu alijua muda wa kushuka jukwaani.
Waliomshauri ndio walimkosea heshima. Tunajua binadamu kuna wakati anakuwa hayupo sawa. Alishauriwa vibaya. Na sasa naamini anagundua Hilo pia kwamba ninyi mliomshauri ndio mliamua kumvua nguo.