Yericko ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano mkuu CHADEMA Taifa alikuwa akiwania tuzo hiyo sambamba na waandishi nguli kutoka mataifa mbali kama Laone Kabelo kutoka Botswana, Lolato Moalosi kutoka Botswana, Bankhe Shabangu kutoka Swazland na Grettelle Gazah kutoka Zimbabwe
Hatua ya Yericko Nyerere kutwaa tuzo hiyo, kunamfanya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo mbili (2) za uandishi bora mfululizo ambapo mwaka jana (2023) alishinda tuzo ya uandishi bora wa vitabu iliyotolewa na 'Zikomo Africa Award' jijini Lusaka nchini Zambia.