Embu tutajie vitabu vyake mkuu Kwa uchacheUsiku wa Machi 07.2026 katika jijini la Kigali nchini Rwanda, Mtanzania Yericko Nyerere ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya uandishi bora wa vitabu Barani Afrika, tuzo inayotolewa na 'Shining Stars Africa Awards'
Yericko ambaye pia ni kada wa CHAUMMA alishinda kwa kura 7584 sawa na 53% alikuwa akiwania tuzo hiyo sambamba na waandishi nguli kutoka mataifa mbalimbali kama Bubakar Baldeh wa Gambia akiyepata kura 6365 sawa na 45%, na Savatir kutoka Zambia aliyepata kura 288 sawa na 1%
Hatua ya Yericko Nyerere kutwaa tuzo hiyo, kunamfanya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo 8 za uandishi bora mfululizo kutoka taasisi mbalimbali za uandaaji wa Tuzo Afrika ambapo mwaka jana 2023 alishinda tuzo ya uandishi bora wa vitabu iliyotolewa na 'Zikomo Africa Award' jijini Lusaka nchini Zambia,
Mwaka 2024 alishinda tuzo moja Shining Stars jijini Johanesbarg Afrika kusini, Mwaka huo huo alishinda tuzo ya MVAA kutoka Lagos Nigeria, na Mwaka huo huo 2024 alishinda tuzo mbili za Zikomo ya uandishi bora wa vitabu na Tuzo ya Kiongozi Bora zilizofanyika Johanesbarg Afrika Kusini.
Mwaka 2025 alishinda tuzo ya zikomo ya uandishi bora wa Vitabu hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Na mwaka huu 2026 umeanza kwa Yericko kushinda tuzo ya Shining Stars hafla iliyofanyika Jijini Kigali katika hoteli ya Olympic.
Huyo ndie Yericko Nyerere nje ya siasa zetu za vyama Jijini Dar, tutampinga au tutamkosoa au tutamtukana katika siasa, lakini linapofika suala la kipaji cha uandishi wa Vitabu Afrika hana mpinzani, tumuombee sasa atoke Afrika akapambane tuzo ya dunia huko.View attachment 3554803View attachment 3554805View attachment 3554803
well doneUsiku wa Machi 07.2026 katika jijini la Kigali nchini Rwanda, Mtanzania Yericko Nyerere ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya uandishi bora wa vitabu Barani Afrika, tuzo inayotolewa na 'Shining Stars Africa Awards'
Yericko ambaye pia ni kada wa CHAUMMA alishinda kwa kura 7584 sawa na 53% alikuwa akiwania tuzo hiyo sambamba na waandishi nguli kutoka mataifa mbalimbali kama Bubakar Baldeh wa Gambia akiyepata kura 6365 sawa na 45%, na Savatir kutoka Zambia aliyepata kura 288 sawa na 1%
Hatua ya Yericko Nyerere kutwaa tuzo hiyo, kunamfanya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo 8 za uandishi bora mfululizo kutoka taasisi mbalimbali za uandaaji wa Tuzo Afrika ambapo mwaka jana 2023 alishinda tuzo ya uandishi bora wa vitabu iliyotolewa na 'Zikomo Africa Award' jijini Lusaka nchini Zambia,
Mwaka 2024 alishinda tuzo moja Shining Stars jijini Johanesbarg Afrika kusini, Mwaka huo huo alishinda tuzo ya MVAA kutoka Lagos Nigeria, na Mwaka huo huo 2024 alishinda tuzo mbili za Zikomo ya uandishi bora wa vitabu na Tuzo ya Kiongozi Bora zilizofanyika Johanesbarg Afrika Kusini.
Mwaka 2025 alishinda tuzo ya zikomo ya uandishi bora wa Vitabu hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Na mwaka huu 2026 umeanza kwa Yericko kushinda tuzo ya Shining Stars hafla iliyofanyika Jijini Kigali katika hoteli ya Olympic.
Huyo ndie Yericko Nyerere nje ya siasa zetu za vyama Jijini Dar, tutampinga au tutamkosoa au tutamtukana katika siasa, lakini linapofika suala la kipaji cha uandishi wa Vitabu Afrika hana mpinzani, tumuombee sasa atoke Afrika akapambane tuzo ya dunia huko.View attachment 3554803View attachment 3554805View attachment 3554803
HahahaHiyo Taasisi makao makuu itakuwa mbande
Mbona mnakuwa na akili za kisoda namna hiyo? Hongera huu utapeli? Hivi ukiona hizo sura kwenye picha unaona kama kuna mwandishi hapo? Huyu jamaa anafanya utapeli wa kujipa zawadi siku nyingi. Jaribu ku-goole hiyo taasisi angalau uone kabla ya kuingizwa kwenye mkenge na huyu tapeli.Hongera, Ila aache uzushi, Askofu Mwamakula anasubiri ajibiwe jambo ambalo huyu Bwana alimsingizia
Sijaamua, kujisumbua akili yangu sababu huyo jamaa nilishamua kumpuuza,kumbe hata vitabu ni utapeli tuMbona mnakuwa na akili za kisoda namna hiyo? Hongera huu utapeli? Hivi ukiona hizo sura kwenye picha unaona kama kuna mwandishi hapo? Huyu jamaa anafanya utapeli wa kujipa zawadi siku nyingi. Jaribu ku-goole hiyo taasisi angalau uone kabla ya kuingizwa kwenye mkenge na huyu tapeli.