Siyo muda huyu jamaa anapewa kitengo maana Samia anawapenda sana wapambee
--------------
Kada wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na mwandishi wa vitabu, Yericko Nyerere, ameituhumu Jumuiya ya Ulaya (EU) akiitaja kuwa sehemu ya wanaopaswa kuchunguzwa kuhusu matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 nchini Tanzania, akidai kwamba EU “imehusika sana kuchochea yaliyotokea.”
Akizungumza na Jambo TV, Yericko amesema kuwa endapo kutahitajika uchunguzi wa kimataifa, basi EU haitakiwi kuwa sehemu ya vyombo vitakavyoshiriki, kwa sababu kwa maoni yake “ni sehemu ya watuhumiwa,” akisisitiza kuwa yeye binafsi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa hatua za jumuiya hiyo zimechangia kuzorota kwa hali ya kisiasa nchini.
Amesema hayo akirejea mjadala unaoendelea baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhutubia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, hotuba ambayo iligusa masuala ya majeraha ya kisiasa na misukosuko ya baada ya uchaguzi.
Katika mahojiano hayo, Yericko amesema kuwa tayari serikali imeshakiri yaliyotokea akirejea hotuba ya Rais Samia wakati wa kufungua Bunge, pamoja na kuunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea kipindi cha uchaguzi.
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi, mamlaka ya kuunda tume za uchunguzi ni ya Rais pekee, na kwamba hakuna sehemu ya Katiba inayoeleza utaratibu wa namna tume hizo zinavyopaswa kuundwa, jambo analoliona kama “pengo la kisheria” linalopaswa kujadiliwa katika mchakato wa katiba mpya.