Yeriko Nyerere: CIA waliamini Mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka ni Mangi Thomas Mariale!

Wengi mnabisha bisha kipumbavu bila kuwa na hoja. Hizo smartphone zenu mnatumia kufanyia nini badala ya kujisomea mambo mbalimbali? Maandiko mengi ya Yericko ni copy & paste kutoka kwa waandishi wengine. Kabla ya social media nilikuwa nikisoma sana gazeti la Rai na baadae Raia mwema. Kule kulikuwa na waandishi nguli tupu. Na makala nyingi za Rai na Raia mwema zipo kwenye kitabu cha Yericko.
Uko sahihii
 
Yeriko anawadanganya wajinga. Kipindi hicho cha ukoloni Uingereza alikuwa na nguvu za kijasusi kuliko hata hao marekani. Waingereza waliijua nguvu ya Nyerere ndo maana wakampa nchi bila kumwaga damu kama kwingine. Julius K Nyerere alikuwa ni akili-kubwa aliwazidi akili machifu wote akiwemo huyo mareale.
Mmmh tungemwagaje damu na hatukua kolon la mwingereza yeye alikua msimamiz tu
 
Yeriko anawadanganya wajinga. Kipindi hicho cha ukoloni Uingereza alikuwa na nguvu za kijasusi kuliko hata hao marekani. Waingereza waliijua nguvu ya Nyerere ndo maana wakampa nchi bila kumwaga damu kama kwingine. Julius K Nyerere alikuwa ni akili-kubwa aliwazidi akili machifu wote akiwemo huyo mareale.
Kilichosababisha wampe nchi bila kumwaga damu sio kwa sababu Nyerere alikua na akili ila ni kwa sababu koloni hili halikua Lao. Walipewa tu kama waangalizi baada ya vita vya kwanza vya Dunia. Kwa hyo hata wao hawakua na full mandate ya koloni hili
 
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

(Soma kielelezo cha nyaraka hiyo chini ya CIA)Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jesuiti za mwaka 1942 ambazo baadae zilikuja kufanyiwa kazi kupitia kwa makasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka...Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia.... Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄

View attachment 3215798
Yeriko hana akili timamu
 
Ni muda wa wakoloni ulikuwa umeisha
 
..Muandishi Mohamed Said anasema Machief walianza kushawishiwa kuhusu Uhuru wakati mipango ya kuanzisha Tanu inafanyika.

..Pia safari ya Mwalimu Nyerere, na Mangi Marealle kwenda UN nadhani ilikuwa mwaka 1955, kwa hiyo inaelekea baadhi ya Machifu hawakuchelewa kuunga mkono harakati za uhuru.
Machifu walikuwa sehemu ya utawala wa Wakoloni, wakiishi maisha ya kifahari wakati huo. Hawakuwa na habari na TANU mwanzoni mwa harakati hadi 1958 baada ya Umma kuonekana unaiunga mkono TANU, hata hivyo walichelewa na Nyerere akafuta Mamlaka zao na mifumo yao kama Mfumo Kabaila wa Nyarubanja huko Bukoba
 
Wakati wa harakati za Uhuru kuanzia 1954 Nyerere alikuwa ameanzisha TANU na katika harakati zake za mwanzo alikumbana na kizingiti cha mkono wa dola ambapo katika baadhi ya sehemu hakuwa anapewa ushirikiano na Machifu ambao walikuwa upande wa Serikali ya Kikoloni. Mwaka 1956 aliteuliwa kuingia katika LEGCO lakini alijiuzuru mwaka mmoja baadae kutokana na kutotambuliwa kwa mchango wake wowote.

Baada ya Mkutano wa Tabora na Uchaguzi wa 1958 wa kura tatu na TANU kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya UTP na TANC basi ilionekana kuwa Machifu wasingeweza kuikwepa TANU. Hata hivyo walikuwa wamechelewa. Na katika kikao chao cha Februali 1959 Saidi Maswenya wa TANU kutoka Maswa na kwa niaba ya Chama Aliwaambia Machifu kuwa ni vyema wakadandia gari wakati muda ukiwa upande wao, vinginevyo wangeachwa. Katika kikao chao kingine mwaka huo Machifu waliamua kutumia ushawishi wao kubagain na TANU iwapo wanaiunga mkono ni maslahi gani wangelipata.

Mwalimu Nyerere aliamua kukata mizizi wa fitna kwa kuitisha kamati yao ya watu 12 ambapo kulikuwa na Chifu Amri Dodo wa Babati, John Maruma wa Rondo, Petro Marealle wa Vunjo, Abdiel Shangali wa Hai, Abdala Fundikira wa Unyanyembe, Haruna Lugusha wa Itetemia, Patrick Kunambi wa Morogoro, Michael Lukumbuzya wa Ukerewe, Kimweri Magogo wa Usambara, Mwami Theresa Ntare wa Kasulu, Adam Sapi wa Kalenga na Humbi Ziota wa Nzega...na akawaambia kuwa katika Utawala mpya hawakuwa na nafasi labda waiunge mkono TANU na pia wagombee ili kuendelea kuwepo katika Halmashauri. Na kuwa hadi kufikia Julai 1962 ingelibidi wawe wamekabidhi ofisi.

Na kweli ilipofika Julai 1962 hawakupata tena mishahara na kazi zao zikafungwa rasmi. Baadhi yao waliendelea kupewa heshima na jamii zao lakini wengi wao walibaki maskini.

Hata hivyo kuna baadhi ya Machifu waliopatana na Mwalimu kama Adam Sapi ambaye aliteuliwa kuwa Mbunge na Spika, Chifu Haruna Lugusha aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Agricultural Society na Michael Lukumbuzya aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanganyika huko India. (Soma. Aspects of Colonial Tanzania cha Prof. Lawrence Mbogoni)
Mkuu Itetemia kwa sasa ni mkoa au mikoa ipi
 
Yeriko anawadanganya wajinga. Kipindi hicho cha ukoloni Uingereza alikuwa na nguvu za kijasusi kuliko hata hao marekani. Waingereza waliijua nguvu ya Nyerere ndo maana wakampa nchi bila kumwaga damu kama kwingine. Julius K Nyerere alikuwa ni akili-kubwa aliwazidi akili machifu wote akiwemo huyo mareale.
Walijua nguvu ya nyerere au wao ndio waliomuandaa pia ili kumkabidhi tanganyika.
 
Yeriko anawadanganya wajinga. Kipindi hicho cha ukoloni Uingereza alikuwa na nguvu za kijasusi kuliko hata hao marekani. Waingereza waliijua nguvu ya Nyerere ndo maana wakampa nchi bila kumwaga damu kama kwingine. Julius K Nyerere alikuwa ni akili-kubwa aliwazidi akili machifu wote akiwemo huyo mareale.
Hakuna cha akili wala nini
Wakoloni hawakuwekeza sana Tanganyika kama ilivyo south afrika ndo maana ilikua rahisi kuachia nchi bila kumwaga damu
 
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

(Soma kielelezo cha nyaraka hiyo chini ya CIA)Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jesuiti za mwaka 1942 ambazo baadae zilikuja kufanyiwa kazi kupitia kwa makasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka...Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia.... Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄

View attachment 3215798
Yeriko Nyerere anajiita jasusi kumbe ni msusi tu,ni moja ya wapenda pesa nyama na pombe za bure.
 
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

(Soma kielelezo cha nyaraka hiyo chini ya CIA)Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jesuiti za mwaka 1942 ambazo baadae zilikuja kufanyiwa kazi kupitia kwa makasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka...Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia.... Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄

View attachment 3215798
Haya ni mauzushi mliyoyazoea na ya kuokoteza
 
Hii takataka toka iwe chawa nishaidharau na maandiko yake...
 
Pumba tupu na plagiarism hakuna kitu hapo 🚮🚮🚮

Screenshot_20241225_150148_Instagram (1).jpg
 
Back
Top Bottom