Yeriko Nyerere: CIA waliamini Mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka ni Mangi Thomas Mariale!

Yeriko Nyerere: CIA waliamini Mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka ni Mangi Thomas Mariale!

Pamoja na kukosa credibility ila alilolisema Yericko Nyerere kweli kabisa, kama Nyerere hakuwahi ku clear mess, basi kikao kilichofuatia kilikuwa kimkabidhi Marealle dola ya Tanganyika, habari za kuwa alitaka utawala wa kanda moja tu ni uongo, ila alipendekeza Tanganyika iwe governed kutokea kaskazini, na sababu kuu ilikuwa ni kwamba watu wa kaskazini ndiyo waliokuwa wameelimika kiasi kwa kipindi hicho, pia mazingira yalikuwa rafiki kwa serikali kujiendesha kutokana na maendeleo ya miundombinu iliyokuwepo kaskazini enzi hizo, Tanga ndio uliokuwa mji mkubwa zaidi tanganyika kwa kipindi hicho, familia ya Marealle ipo well off, hadi sasa, wakimiliki biashara kubwa kubwa na investment nyingi tu.
 
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

(Soma kielelezo cha nyaraka hiyo chini ya CIA)Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jesuiti za mwaka 1942 ambazo baadae zilikuja kufanyiwa kazi kupitia kwa makasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka...Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia.... Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄

View attachment 3215798
Huyu jamaa kachanganyikiwa baada ya basha wake kushindwa uchaguzi
 
Machifu walikuwa sehemu ya utawala wa Wakoloni, wakiishi maisha ya kifahari wakati huo. Hawakuwa na habari na TANU mwanzoni mwa harakati hadi 1958 baada ya Umma kuonekana unaiunga mkono TANU, hata hivyo walichelewa na Nyerere akafuta Mamlaka zao na mifumo yao kama Mfumo Kabaila wa Nyarubanja huko Bukoba

..tatizo la Machifu ni kutokuchaguliwa kwa njia ya demokrasia.

..Wananchi walianza kuliona tatizo hilo na ndio maana Wachagga Council wakaamua kwamba Mangi Mkuu awe mtu yeyote mwenye sifa na apigiwe kura.

..madai kwamba Machifu waliishi kama wakoloni ni kuwachafua kwani hata viongozi wa Tanu waliishi kama gavana, PC, na DC, wa kikoloni.
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina


UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Mbona Wakikuyu wanapewa Madaraka?
Ndio mana Unaona Tribalism iko at the peak kule, Hata Msukuma Kuwa mkuu wa Nchi wa A mistake hii nchi tuwaache makabila Madogo kabisa ndio yashike Power ya Juu kama Wamwera, Wasambaa, Wakwere, Watu wa visiwani, Wamakonde hii Nchi Umpe Mushi au Rweyemamu hapatakalika mtu kama Mwera au Mkwere anakuwa Mkuu wa Nchi na Ndugu zake hata Elimu hawana hivo lazima aunde serikali ya Wote, We huoni Magu Tu kila sehemu palianza Kujaa Wasukuma Kwa sababu kabila ni Majority haifai
 
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale.

(Soma kielelezo cha nyaraka hiyo chini ya CIA)Lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.

Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jesuiti za mwaka 1942 ambazo baadae zilikuja kufanyiwa kazi kupitia kwa makasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka...Wazo lililoshinda ndio shirika lenye nguvu dunia.... Roma ikisema mashauri yote yamekwisha....

Yeriko Nyerere ameweka Taarifa Ukurasani kwake X

Mlale unono

Kwako Madaraka Nyerere 😄

View attachment 3215798
Mareale yupi huyo aliueaminiwa?
Mareale alikuwa anafanya lobying eneo lao liwe nchi inayojitegemea. Mareale hakuwahi kuingia katika duru la siasa za Tanganyika
 
Mwalimu alitumia ujanja ujanja - ni kweli Mangi ilikuwa achukue hii nchi.
 
Nyerere was very smart yule mzee! Entire Nyerere's family is very smart!
Hawa kina Steve Mengere na huyu muabudu mizimu hakuna kitu ovyo kabsa!
Nyerere wa Playstore 🚮 🚮 🚮
 
Wakati wa harakati za Uhuru kuanzia 1954 Nyerere alikuwa ameanzisha TANU na katika harakati zake za mwanzo alikumbana na kizingiti cha mkono wa dola ambapo katika baadhi ya sehemu hakuwa anapewa ushirikiano na Machifu ambao walikuwa upande wa Serikali ya Kikoloni. Mwaka 1956 aliteuliwa kuingia katika LEGCO lakini alijiuzuru mwaka mmoja baadae kutokana na kutotambuliwa kwa mchango wake wowote.

Baada ya Mkutano wa Tabora na Uchaguzi wa 1958 wa kura tatu na TANU kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya UTP na TANC basi ilionekana kuwa Machifu wasingeweza kuikwepa TANU. Hata hivyo walikuwa wamechelewa. Na katika kikao chao cha Februali 1959 Saidi Maswenya wa TANU kutoka Maswa na kwa niaba ya Chama Aliwaambia Machifu kuwa ni vyema wakadandia gari wakati muda ukiwa upande wao, vinginevyo wangeachwa. Katika kikao chao kingine mwaka huo Machifu waliamua kutumia ushawishi wao kubagain na TANU iwapo wanaiunga mkono ni maslahi gani wangelipata.

Mwalimu Nyerere aliamua kukata mizizi wa fitna kwa kuitisha kamati yao ya watu 12 ambapo kulikuwa na Chifu Amri Dodo wa Babati, John Maruma wa Rondo, Petro Marealle wa Vunjo, Abdiel Shangali wa Hai, Abdala Fundikira wa Unyanyembe, Haruna Lugusha wa Itetemia, Patrick Kunambi wa Morogoro, Michael Lukumbuzya wa Ukerewe, Kimweri Magogo wa Usambara, Mwami Theresa Ntare wa Kasulu, Adam Sapi wa Kalenga na Humbi Ziota wa Nzega...na akawaambia kuwa katika Utawala mpya hawakuwa na nafasi labda waiunge mkono TANU na pia wagombee ili kuendelea kuwepo katika Halmashauri. Na kuwa hadi kufikia Julai 1962 ingelibidi wawe wamekabidhi ofisi.

Na kweli ilipofika Julai 1962 hawakupata tena mishahara na kazi zao zikafungwa rasmi. Baadhi yao waliendelea kupewa heshima na jamii zao lakini wengi wao walibaki maskini.

Hata hivyo kuna baadhi ya Machifu waliopatana na Mwalimu kama Adam Sapi ambaye aliteuliwa kuwa Mbunge na Spika, Chifu Haruna Lugusha aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Agricultural Society na Michael Lukumbuzya aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanganyika huko India. (Soma. Aspects of Colonial Tanzania cha Prof. Lawrence Mbogoni)

Duh, eti Nyerere alianzisha TANU
 
Back
Top Bottom