Yerusalemu: Kikombe Kinachowalevya Mataifa

Hiin
HIi nadharia yako ni ya kusadikika .
Hivi wewe una dini yeyote unayoiamini? Maana hili jambo kwa mtu yeyote anaona dhahiri kiini cha .mgogoro huu ni imani za kidini. Mleta mada amerejea maandiko mbalimbali ya biblia kuonesha jinsi mgogoro ulivyo. Iran kwa mfano sio mwarabu lakini ni waislamu na wanawaunga mkono Wapalestina kwa sababu tu ni waislamu wemzao. Hao waara u wa mataifa mengine nao ni hivyo hivyo wanaungaxmkono palestina kwa sababu za kidini zaidi. Kama waarabu wangekuwa wakristo kwa kiasi kikubwa wasingeunga mkono wapestina blindly.


Ukiacha sababu za kidini mwenye haki ni Israel kwa sababu kuondoka kwao enzi hizo kutawanyika duniani na baadae ardhi yao kukaliwa na wapalestina hakuwaondolei haki waisraeli kuchukua ardhi yao.
 
Umeanza vizuri sana kwenye upande wa historia lakini umekuja kuharibu kwenye ngonjera na hekaya za abunuwasi za Kibibilia

Bibilia imewafanya watu wazima na akili zao kuamua kuziweka akili hizo mfukoni linapokuja swala la IMANI na kuwa kama Wapumbavu

Asilimia kubwa wanaishabikia Israel kwasababu tu wanaamini ni taifa teule la Mungu kwa mujibu wa hekaya za Bibilia........ This is bullshit
 

Mkuu hebu fafanua hiyo HAKI ya waisrael dhidi ya wapalestina
 

Kwa namna mnavyo mueleza Mungu alivyo basi hawezi kuwa na maneno yasio na logic kiasi hicho mkuu

Barua aandike Paulo halafu yawe ni maneno ya Mungu?
 
Hongera kwa andiko hili. Umelifanyia sana kazi. Lakini usisahau kuongeza na zile baraka ambazo Isaka alimpa Yakobo.
 
Code:
Tatu: Vyanzo tutakavotumia ni Historia, Biblia, Quran na akili ya kawaida.
Isaka alimzaa Esau na Yakobo(mapacha),Yakobo alimfanyia unyang'anyi wa baraka za Isaka kwa Esau.Esau alijiapiza kumuua Yakobo na Yakobo akakimbilia kwa mjomba wake.
Yakobo alipewa jina jingine na Mungu na akaitwa Israel,na nikizazi chake tu ndiyo waitwa wana wa Israel.

Ikiwa,Esau na kizazi chake siyo wana wa Israel na siyo waisrael.Je,Esau na kizazi chake wanaitwaje?,nchi yao ni ipi?Race yao ni ipi hapo mashariki ya kati?Ikiwa ahadi ya Mungu ni kwa Isaka,kwa nini Esau siyo sehemu ya ahadi?.

Naomba majibu ya maswali yangu hayo manne.
 
Mkuu hebu fafanua hiyo HAKI ya waisrael dhidi ya wapalestina
Mungu aliyeumba dunia ndiye aliyewqpa waisraeli hiyo nchi. Ila kuna vipindi walikiwa wanaadhibiwa kwa kupelekwa utumwani uhamishoni kwa, kumuasi Mungu wao. Hivyo wakati hawapo watu wengine waarabu waliingia na kukaa huko. Lakini hii haimaanishi kuwa ile sio mali yao waisraeli. Kama waarabu wangekuwa wakristo wangeelewa.
 
You nailed it [emoji817]
 

Huu ujinga ndio unao wapa kiburi Wayahudi mkuu

Hekaya za Mungu ni za kutunga tu kama Hadithi za Shigongo..... HAKUNA MUNGU

Kwanza hao wayahudi wenyewe wanawachukia wakristo kuliko wanavyo wachukia waislam ila cha ajabu Wakristo ndio wakwanza kujipendekeza kwa wayahudi
 
Hadithi kama hizi ndio zinawakosesha utu wapumbavu nyinyi.
Anayetukana bila kusikiliza hatumii hekima. Iwe radhi kama andiko limekuudhi. Kule mjini huwa watu "omba omba" wanakaaga barabarani wakiomba msaada. Watu wengi kuna wakati wanapita na kujifanya hawaoni.

Basi kama andiko hili linakutia kichefuchefu na kuchechua nyongo basi pita ujifanye kama hujaliona kama vile kwa omba omba!
 
God of the Bible.
The God who knows timelines, The God who knows the past, present and future.
 
Kuhusu Mungu kuwepo au asiwepo hilo wewe utaamua mwenyewe.


Ila ni kweli wayahudi kuna mahala wanakosea. Na hapo ndipo walipokesea. Hata wanafunzi wa Yesu Kristo walipoanza kuhubiri kwa watu wa mataifa wayahudi wa kikiristo waliwakataza kuwa injili ni ya wayahudi tu.


Hawakujua kuwa Mungu alipomuita Ibrahim "baba wa mataifa" kuwa wao Israel Mungu atawatumia kuokoa dunia nzima (hii ndio imani ya kikristo kama wewe ni mkristo. Na ndo mpango wa Mungu toka pale Edeni alipotoa unabii kuwa uzao wa mwanamke utamponda kichwa nyoka.....)

Jambo hili limefichwa hata sasa kwa waisrael walio wengi ambao bado hawajamkubali Yesu Kristo.

Somo hili ni lirefu ila ntajaribu kulielezea hapa kama utakua tayari.

Ukisoma kitabu cha Warumi 11. Hili swala limeongelewa kwa kina

Basi, nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mimi binafsi ni Mwisraeli, mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini. Mungu hakuwakataa watu wake aliowateua tangu mwanzo.
Waroma 11:1‭-‬2

Basi, nauliza: Je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa? Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa mengine, ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu. Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao wa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri kwamba kuingizwa kwa idadi yao kamili kutakuwa ni baraka zaidi.
Waroma 11:11‭-‬12

Basi, sasa nawaambieni nyinyi watu wa mataifa mengine: Maadamu mimi nimekuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine, ninajivunia huduma yangu, nipate kuwafanya wananchi wenzangu wawaonee nyinyi wivu, na hivyo nipate kuwaokoa baadhi yao. Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka! Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Nyinyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini. Basi, msiwadharau wale waliokatwa kama matawi! Na, hata kama kuna la kujivunia, kumbukeni kwamba si nyinyi mnaoitegemeza mizizi, bali mizizi ndiyo inayowategemeza nyinyi. Sawa! Yalikatwa kwa sababu ya kukosa imani, bali wewe unasimama kwa imani yako. Lakini usijivune; ila uwe na tahadhari. Kwa maana, ikiwa Mungu hakuwahurumia Wayahudi ambao ni kama matawi ya asili, je, unadhani atakuhurumia wewe? Ona, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa. Nao Wayahudi, hali kadhalika; wakiacha utovu wao wa imani, watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.
Waroma 11:13‭-‬15‭, ‬17‭-‬18‭, ‬20‭-‬23

Hapo unaona kuwa wayahudi ndio kwa kiburi walikataa habari za Kristo ila ipo siku watakubali.

Na kama ulisoma andiko la kwanza utaona kuwa vita hii ya sasa (au itakayotokea baadae) inaeza kupelekea waisrael kuzungukwa na mataifa na kupigwa vibaya mno hadi kufikia Jerusalem. Na pindi watakapokuwa wanamaliziwa basi ndipo Kristo atarudi tena!

Unabii huo unasema:
Neno la Mwenyezi-Mungu kuhusu Israeli. Mwenyezi-Mungu aliyezitandaza mbingu, aliyeiweka misingi ya dunia na kumpa mwanadamu uhai asema hivi: “Nitaufanya mji wa Yerusalemu kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yaliyo kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi. Mji wa Yerusalemu utakaposhambuliwa, hata miji yote ya Yuda itashambuliwa. Siku hiyo nitaufanya mji wa Yerusalemu kuwa kama jiwe zito kwa watu wote: Yeyote atakayelinyanyua atajiumiza mwenyewe. Watu wa mataifa yote duniani wataushambulia mji huo.
Zekaria 12:1‭-‬3

Unabii unaelezewa zaidi jinsi Jerusalem itakavopigwa:


Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu. Mwenyezi-Mungu atayakusanya mataifa yote ili kuushambulia mji wa Yerusalemu. Mji utatekwa, nyumba zenu zitatekwa nyara, na wanawake wenu watanajisiwa.

Nusu ya wakazi wa mji watapelekwa uhamishoni, lakini nusu itakayosalia haitachukuliwa nje ya mji. Kisha Mwenyezi-Mungu atatoka na kuyapiga vita mataifa hayo, kama afanyavyo daima siku za vita.
Zekaria 14:1‭-‬3


“Siku hiyo, nitayaangamiza mataifa yote yanayotaka kuushambulia mji wa Yerusalemu. Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza. Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu mjini Yerusalemu kama maombolezo ya kumwombolezea Hadad-rimoni katika mbuga za Megido.
Zekaria 12:9‭-‬11

Hapo unaona kuwa Mungu mwenyewe itabidi awaokoe watu wake la sivyo watamalizwa. Hizo siku zinaeza kuwa nyakati hizi au zijazo. Hatujui ndo maana tunaambiwa 'tukeshe tukiomba'


Anyway, kama wewe pia ni mwanafunzi wa Biblia utatambua kuwa Wayahudi ni wabishi hata Musa walimgeuka jangwani pamoja na kuona miujiza yote. Mara nyingi walimwacha Mungu na walipigwa na kupelekwa utumwani.

Ila Mungu siku zote aliwarudia. Hata kama hawamtaki.

---------

Ishu ya kujipendekeza kwa wakristo.

Inaezekana kuna wanaojipendekeza ndio.

Lakini mkristo yoyote yule inampasa ajue neno hili (warumi 11 kama nlivoelezea apo juu) pia ukumbuke ahadi ya Mungu kwa Ibrahim ambaye ndie baba wa Israel na ndie baba wa wakristo kwa imani

soma Wagalatia 3:29
Ikiwa nyinyi ni wa Kristo, basi ni wazawa wa Abrahamu, na mtapokea yale aliyoahidi Mungu.

Sasa basi huezi kujilaani mwenyewe.

Mkristo yeyote ni vyema akawaombea Israel wamjue Kristo na kuwa karibu nao. Ndio kuna mahali wanakosea ila hupaswi kuwashabikia wanapokesea.

Cha muhimu jua imani yako imetokea wapi na ina maana gani ili kuepuka kujipendekeza.

Naamini nimekujibu comment yako
 
Kwa namna mnavyo mueleza Mungu alivyo basi hawezi kuwa na maneno yasio na logic kiasi hicho mkuu

Barua aandike Paulo halafu yawe ni maneno ya Mungu?
Sasa mkuu Mungu si anatumia watu. Au ulitaka Mungu aandike mwenyewe? Anyway alishawahi kufanya hivyo. Lakini bado watu hawakuamini. Mungu akishuka nani atakayeza kusimama?

Pia maandiko yako. Mtu mwenye hekima hapingi tu.

Kama kuna imani mbili basi chukua vitabu vyake vyote. Soma kwa makini kila kimoja bila kuwa na upendeleo. Ukimaliza vyote mwanzo mwisho kila kimoja utajua kipi kiko sahihi ama vyote au vyote ni makosa. Ila kupinga bila kufanya utafiti wa kina sio busara sana
 
Kuna wanaosema binadamu walitokea kwa nyani wengine kwa Adam. Wasukuma na wengine walitoka kwa Adamu naamini hivyo. Mwenzangu sijui upo upande gani?
Mbona hawajatajwa hapo kwa watoto wa Abraham,wao ni wa nani
 
Ndo nimesema apo kuna makundi mawili

La kwanza linasema binadamu wote wametoka kwa nyani au zinjathropus

Wengine wanasema binadamu wote wametoka kwa Adamu
Mbona hawajatajwa hapo kwa watoto wa Abraham,wao ni wa nani
 
Yatupasa kujua kuwa hakuna Ukristo bila Wayahudi. Waliomkataa Kristo ni Wayahudi. Waliompokea Kristo kwanza, na kueneza ujumbe wa Kristo kwa Mataifa ni Wayahudi.

Na tufahamu kuwa Wayahudi hawajamkataa masiha bali ufahamu wao ndio uliofungwa hata wasimkubali kristo kuwa ndiye masiha aliyetabiriwa. Hii haina tofauti na yale yaliyomtokea Mtume Paulo. Mtume Paulo aliilinda kwa nguvu zake zote dini yake kwa kadiri ya mafundisho aliyopewa. Alipambana na wafuasi wa Kristo akiamini anampambania Mungu wa Ibrahim, wa Isaka na Yakobo. Alipopewa ufahamu, na kufunuliwa yaliyofichika, alihamisha nguvu zake zote kutoka imani yake ya kale, na kwenda kwenye Ukristo.

Yumkini, ndivyo itakavyokuwa kwa hawa wana wa Yakobo. Siku watakapofunuliwa kuwa masiha aliyetabiriwa na Nabii Isaya, ambaye wamekuwa wakimsuburia, ndiye Kristo Yesu, nguvu yao yote wataielekeza kwa masiha. Katika jicho la imani, hayo yatakapotimia, hakuna atakayeisogelea Jerusalem kwa nia ya kuiangamiza maana itakuwa moja kwa moja chini ya ulinzi wa Mungu mwenyewe.
 
Ni kweli baada ya vita ya Zekaria 12 na 14. Katika miaka elfu moja ya utawala wa Mungu duniani kutakua na amani. Lakini bado Shetani atajaribu tena kwa mara ya mwisho kuvamia Jerusalem

Wakati miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake. Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani. Walipita katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watakatifu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza. Naye Ibilisi aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka madini ya kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.
Ufunuo 20:7‭-‬10

Basi inatupasa tuwemo pamoja na Kristo.
 
Isaka alimzaa Esau na Yakobo(mapacha),Yakobo alimfanyia unyang'anyi wa baraka za Isaka kwa Esau.Esau alijiapiza kumuua Yakobo na Yakobo akakimbilia kwa mjomba wake.
Yakobo alipewa jina jingine na Mungu na akaitwa Israel,na nikizazi chake tu ndiyo waitwa wana wa Israel.

Ikiwa,Esau na kizazi chake siyo wana wa Israel na siyo waisrael.Je,Esau na kizazi chake wanaitwaje?,nchi yao ni ipi?Race yao ni ipi hapo mashariki ya kati?Ikiwa ahadi ya Mungu ni kwa Isaka,kwa nini Esau siyo sehemu ya ahadi?.

Naomba majibu ya maswali yangu hayo manne.
 
Kwanza mantiki ya swali lako inaweza isiwe sawa sawa kwa jinsi ulivouliza. Kwa maana ukihoji kwa nini Esau hayupo kwenye baraka za Israel basi itakubidi pia uhoji kwa nini Ishmael asiwe na baraka ya Isaka. Na kumbuka Ibrahim alikua na watoto wengine na mke wake wa pili, Keturah, baada ya Sarah kufariki. Kwa nini hao watoto wasiwe na baraka ya Israel?



Swali lipo kwenye Biblia. Kama wewe ni mkristo basi ukisoma Biblia inasema haya maswali yote.



Kwanza tujue kwa kuhusu Isaka na Ishmael.

Kumbuka Mungu aliingia agano na Ibrahim kuwa kupitia Sara ndipo baraka itatokea.

Ibrahim alipozaa na Hagar alikua nje ya agano. Japo na hayo bado Mungu alimbariki huyo Ishmael.


Kumbuka Hagar alikua kijakazi. Alipompata Ishmael alianza kumdharau Sara na Ishmael alikua akimdharau Isaka. Na ikawa ugomvi. Ilibidi waondoke.


Ibrahim alimuombea baraka kwa Mungu:


Mwanzo 17:18‭-‬21

Basi, Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti ungekubali ahadi yako hiyo imhusu Ishmaeli.” Mungu akamjibu, “La! Ila mkeo Sara atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita Isaka Nitaliimarisha agano langu kwake na wazawa wake, kuwa agano la milele. “Na, kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Nitambariki, nitamjalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Ishmaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya kuwa baba wa taifa kubwa. Lakini agano langu litathibitika kwa Isaka ambaye Sara atakuzalia mwakani wakati kama huu.”





Na kumbuka baraka tunayoingelea apa ni kuwa kupitia uzao wa Ibrahim Mungu ataleta mpango wake wa kuokoa wanadamu na dhambi hii inakuja pamoja na kupewa nchi ya Kanani na pia kuwa taifa kubwa lenye mafanikio.


Kwa kifupi Uzao wa Ibrahim ulikua na nia ya kumleta Yesu Kristo kama ondoleo la dhambi. Na hivyo haiezekani kuwa na uzao wawili bali mmoja. Haiezekani Esau na Yakobo/Israel wote wamlete Masihi. Na ndio maana ni mmojawapo tu alitakiwa kuwa sehemu ya ahadi.


Huyu Isaka ndiye aliyemzaa Yakobo na Esau.


Esau alikua mtu wa mishe mishe za nyikani. Yakobo alikua anafanya kazi zake nyumbani zaidi. Esau alikua na kiburi pia kutokana na nguvu zake za uwindaji alikua akijiamini sana na hakujali sana mambo ya muhimu kama haki yake ya mzaliwa wa kwanza.


Aliuza haki yake kwa dengu ili asizimie njaa. Kibri na dharau zilikua zinamzingua.


Hii ndio watu wengi wanajua


Lakini zaidi ya hayo Esau hakua na heshima kwa wazazi wake. Alienda kuoa wake kutoka mataifa mengine na hao wake inaonekana walikua mwiba kwa wazazi wake.


Mwanzo 26:34‭-‬35

Esau alipokuwa na umri wa miaka arubaini, alioa wake wawili Wahiti: Yudithi bintiye Beeri, na Basemathi bintiye Eloni. Wanawake hao waliyafanya maisha ya Isaka na Rebeka kuwa machungu.


Wote tunajua kati ya kitu Mungu hapendi ni dharau na kujivuna. Pia Mungu anataka tuheshimu wazazi. Ukisoma kisa cha Esau na Yakobo utaona tofauti ya hawa wawili. Yakobo alikua mtii kusikiliza wazazi kila walichomuambia na Esau alikua kijeba na hakusikiiliza sana mawaidha yao hasa kwenye ishu ya kuoa. Kama vile alivofanya Samson.


Ukirudi kwenye kisa cha kuuza haki ya kuzaliwa wa kwanza


Mwanzo 25:27‭-‬34

Watoto hao wakakua; Esau akawa mwindaji hodari, mpenda maisha ya mbugani, na Yakobo akawa mtu mtulivu, mpenda maisha ya nyumbani. Basi, Isaka akampenda Esau kwa sababu alipenda kula mawindo yake, lakini Rebeka akampenda Yakobo.


Siku moja, Yakobo alipokuwa anapika dengu, Esau alirudi nyumbani kutoka mawindoni ana njaa sana. Kwa hiyo akamwambia Yakobo, “Nafa njaa; tafadhali, nigawie chakula hicho chekundu nile.” (Ndiyo maana walimpanga jina Edomu yaani mwekundu). Yakobo akajibu, “Kwanza niuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” Esau akasema, “Sawa! Niko karibu kufa; haki yangu ya mzaliwa wa kwanza itanifaa nini?” Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Basi, Esau akamwapia na kumwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.


Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na dengu kiasi. Esau akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo ndivyo Esau alivyoidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.


Hapo unaona jinsi Esau alivouza mwenyewe haki yake.


Wakti baba yake Isaka anaelekea kufa alimtuma amletee nyama ya mawindo atafune afurahi ambariki. Ila mama mtu alikua na mpango wake ambao wengi tunajua mwisho wa siku Yakobo ndipo alipopewa baraka zile.



Mwanzo 27:27‭-‬29

Basi, Yakobo akamkaribia baba yake na kumbusu, na baba yake aliposikia harufu ya mavazi yake, akambariki akisema, “Tazama, harufu nzuri ya mwanangu ni kama harufu ya shamba alilobariki Mwenyezi-Mungu! Mungu akumiminie umande wa mbinguni; akupe ardhi yenye rutuba, nafaka na divai kwa wingi. Jamii za watu zikutumikie, na mataifa yakuinamie kwa heshima. Uwe mtawala wa ndugu zako, watoto wa kiume wa mama yako wakuinamie kwa heshima. Kila akulaaniye na alaaniwe, kila akubarikiye na abarikiwe!”




Esau aliporudi na mawindo babaye alimuambia baraka nishazitoa. Hapa ndipo Esau alipogundua alizingua na alilia kwa uchungu apate angalau ata kabaraka cha kukombeleza.

Baba yake alimuambia haya:



Mwanzo 27:31‭-‬40

Esau pia akatengeneza chakula kitamu, akampelekea baba yake, akamwambia, “Haya baba, inuka ule mawindo yangu mimi mwanao, ili upate kunibariki!” Isaka akauliza, “Wewe ni nani?” Naye akamjibu, “Ni mimi mwanao Esau, mzaliwa wako wa kwanza.” Hapo Isaka akatetemeka mno, akasema, “Ni nani basi yule aliyewinda na kuniletea mawindo, nami nimekwisha kula kabla hujaja? Tena nimekwisha mbariki; naam, amekwisha barikiwa!”



Esau alipoyasikia maneno ya baba yake, akaangua kilio cha uchungu. Kisha akamwambia baba yake, “Ee baba yangu, nibariki na mimi, tafadhali!” Lakini Isaka akasema, “Ndugu yako alikuja kwa hila, naye amechukua baraka yako.” Esau akasema, “Ndio maana anaitwa Yakobo! Amechukua nafasi yangu mara mbili. Kwanza alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua baraka Zangu.” Kisha akamwuliza baba yake, “Je, hukunibakizia baraka yoyote?” Isaka akamjibu, “Nimekwisha mfanya Yakobo kuwa mtawala wako, na kumpa ndugu zake wote kuwa watumishi wake. Nimempatia nafaka na divai. Nikufanyie nini sasa, wewe mwanangu?”


Esau akamwambia baba yake, “Baba, kwani una baraka moja tu? Nibariki hata mimi, ee baba!” Hapo Esau akalia kwa sauti kubwa. Ndipo Isaka, baba yake, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na ardhi yenye rutuba, na mbali na umande wa mbinguni. Utaishi kwa upanga wako, na utamtumikia ndugu yako; lakini utakapoasi utaivunja kongwa yake shingoni mwako.”



Hizo ndo baraka alizopewa


-------

Kuhusu hao kina Esau ni kina nani sasa. Baadi wanasema ni mataifa ya kiarabu na ulaya. Ukifatilia historia yao utaelewa zaidi.


Hapa nimejaribu kujibu kwenye upande wa kiroho zaidi.


Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…