Yes!! English never loved us, not to this extent

Halafu kinafundishwa kuanzia darasa la tatu mpaka mavyuoni lakini bado hali ndiyo hiyo. Unajua inaweza kuwafanya watu wa Mataifa mengine wafikiri Watanzania wana tatizo la uelewa?
 
🤣🤣🤣 Upo sahihi ,, mimi kinachoniuma kuona wasomi kabisa watu wamekaa miaka zaidi ya 15 ,, wakisoma tena kwa hii lugha ,, wanaruhusu vitu kama hivi vitokee
Like the father, like the son!
 
What the english itself says?
 
acha kutetea ujinga mkuu.
 
Halafu kinafundishwa kuanzia darasa la tatu mpaka mavyuoni lakini bado hali ndiyo hiyo. Unajua inaweza kuwafanya watu wa Mataifa mengine wafikiri Watanzania wana tatizo la uelewa?
shida ni wanaofundisha kiingereza wenyewe hawajui kiingereza
 
acha kutetea ujinga mkuu.
Sitetei ujinga mkuu lakini kilichoandikwa pale kipo sawa tu na kinaeleweka vizuri zaidi kwa jamii yetu ya kitanzania ambayo kiingereza hakizungumzwi sana.

Huenda pia aliyeandika hana misamiati ya kutosha ya lugha ya kiingereza.

Lakini pia ningekuwa mimi nisingeandika kama vile.
 
sawa mkuu
 
Aliyeandika anakosaje misamiati ya kuandika na huku kasoma hadi Chuo?
 
Aliyeandika anakosaje misamiati ya kuandika na huku kasoma hadi Chuo?
Nadhani unajua kabisa mkuu kwamba sio kila aliyefika chuo anaweza kuwa na misamiati mingi ya kiingereza anayoweza kutumia kuleta ujumbe bila mkanganyiko.
 
Nadhani unajua kabisa mkuu kwamba sio kila aliyefika chuo anaweza kuwa na misamiati mingi ya kiingereza anayoweza kutumia kuleta ujumbe bila mkanganyiko.
Sijakukatalia mkuu. Hilo nalifahamu. Hata mavyuoni wakati mwingine wahadhari (baadhi) wameonekana kubabaika kwenye suala la lugha. Issue ni hii:
1. Ni halali hilo kutokea?
2. Kuna haja ya kuendelea kumfundisha kwa lugha ya Kiingereza kama wahitimu wenyewe ndiyo wanakuwa hivyo?
3. Si bora tu sasa Kiingereza kingeondolewa kwenye mitaala ijulikane kuwa Tz hawafubdishwi hiyo lugha?
4. Unafahamu kuwa kuna darasa la saba wanaoongea Kizungu kizuri baada ya kwenda English course ya miezi kadhaa kuzidi baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu?
 
Lakini pia mleta mada kichwa cha chapisho lako kina walakini kama ilivyo kwenye sentensi iyobeba mada nzima.

"English never loved us"
English- ni lugha ya Uingereza, ni watu wa Uingereza

Kwa namna kichwa kinavyosomeka kabla ya kwenda kwenye mada kuu, itatafsiriwa kama "Waingereza hawajawahi kutupenda" na sio " Kiingereza hakijawahi kutupenda". Kivipi kiumbe kisichohai kikapenda? Only living things can have feelings.

Kwa sababu content iliyo kwenye chapisho hili imeandikwa kwa Kiswahili na kichwa cha chapisho kimeandikwa kwa kiingereza, mtumiaji wa lugha ya kiingereza asiyejua kiswahili ataelewa hii mada tofauti kabisa na anayejua Kiswahili na kiingereza kwa wakati mmoja.
 
Hapana mkuu kiuhalisia haikutakiwa kuwa hivyo.
Kuendelea kutumia lugha ya kiingereza mashuleni inatakiwa kuendelea ila mfumo wa matumizi ya lugha hiyo huko mashuleni ndio ubadilishwe.

Kiswahili kama somo na kiingereza kama somo viendelee kuwepo lakini masomo mengine yanayobaki yafundishwe kwa lugha ya kiingereza.

Tunakiabudu sana Kiswahili lakini muda huo pia tunategemea kiingereza kuendesha nchi. Hili ni tatizo
 
Okay imeelezea kasayansi kidogo ,, mimi siyo mwalimu wa kiingereza lakini ntajaribu kukuelekeza kwa kadri navyoelewa hii lugha

Katika lugha ya kiingereza kuna

Direct speech
Hapa mtendaji mkuu ( subject au actor) anakuwa mwanzo afu mtendewa (object au receiver) anakuwa mwishinoni ..

Mfano ,,, john kicks a ball

John ni mtendaji (subject au actor)
A ball ni mtendewa (receiver au object)

Popote ukiona sentensi ipo hivi basi ni direct speech ..

Indirect speech ..
Hapa mtendewa ( receiver au object anakuwa mwanzo na mtendaji( actor au object )
Mfano
The ball is kicked by john

The ball ni mtendewa (object au receiver )

John ni mtendaji ( subject au actor)

Sasa katika hii lugha ya kiingereza
Mfumo huu wa pili (indirect speech ) mara nyingi hutumika pindi unapokuwa hutaki kutaja jina la mtendaji au pindi unapokuwa humjui mtendaji aliyefanya jambo au tukio..

Mfano unaweza kuandika
The ball is kicked
Hapo nimeamua kutomtaja mpigaji au simjui aliyepiga mpira .. japo mto anaweza kukuuliza by who ??

Sasa tuje kwenye mada yetu

H.i.v is killed
Hii ni inderect sentence
Ikiwa na maana H.i.v imeuwawa au imetokomezwa ,,, kweli sentensi hii ipo sahihi lakin haina maana kwanini kwasababu
H.i.v bado ipo , na ni ugonjwa hatari hivyo ni wazi aliendika hapa hakuelewa alichokiandika..

Sijui kama nipo sahihi wengine wanaweza kuja kujazia pale nilipokosea
 
Kuna jamaa alipost FB,halafu picha inaonesha mke wa jamaa anamnyonyoa kuku aliyechinjwa manyoya,jamaa akaandika..
"We are waiting hen until cooking"
 
I reserve my comments till further notice
 

Attachments

  • IMG-20240713-WA0009.jpg
    182.3 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…