Yesu alikuwa mfanyabiashara, Mohammed alikuwa mfanyabiashara: Kwanini wafanyabiashara wakristo na waislam wengi sio waaminifu?

Yesu alikuwa mfanyabiashara, Mohammed alikuwa mfanyabiashara: Kwanini wafanyabiashara wakristo na waislam wengi sio waaminifu?

Au labda niulize swali.Furniture alikuwa anamtengenezea Nani Kama hakuwa nawateja?
Assumption yako hapa ni biashara ilikuwa yake. Na kuwa alikuwa na wateja. Let say hakuwa na biashara alikuwa anamsaidia baba yake kwenye kufanya kazi na hakujihusisha na wateja in whatever way, huyo ni fundi au mfanyabiashara? Au labda kama alijifunza akafanya kidogo akapotelea hekaluni kufundisha huko?

Najua hizi ni speculations lakini yote haya pia yanawezekana na strongly suggested kama nilivyoonesha kwenye other post. Sasa kwa kuwa mko dogmatic kuwa alikuwa anafanya biashara (mwezako kasema kabisa kuwa lazima anajua marketing et al) sasa mtuletee andiko. Ni hilo tu...!
 
Yesu hakuwa mfanyabiashara, alikuwa anajishughulisha na fenicha kwa sababu mzee wake alikuwa fundi, kwa hiyo ni kama kazi za nyumbani tu. Kwanza hata useremara wenyewe alikuwa anazuga tu ili miaka isogee aanze kuchapa injili watu watubu dhambi zao wamrudie Mungu.

unajua waisrael tamaduni yao ilikuwa mtoto unarithi na kujifunza ujuzi kwa baba yako ndio maana yesu tena mtoto mkubwa wa kiume ilikuwa lazima awe fundi seremala kusema alikuwa anamsaidia tu inaweza kuwa kweli lakini nikuulize kitu, mda katikati ya baba yake kafariki na yeye kuanza kuhubir injili alikuwa anafanya nini kwa akili zako unadhani mtu ambaye maisha yake yote kajifunza useremala tu. Note dingi yake alianza kuvuta kabla ya yy kuanza kuhubir
 
unajua waisrael tamaduni yao ilikuwa mtoto unarithi na kujifunza ujuzi kwa baba yako ndio maana yesu tena mtoto mkubwa wa kiume ilikuwa lazima awe fundi seremala kusema alikuwa anamsaidia tu inaweza kuwa kweli lakini nikuulize kitu, mda katikati ya baba yake kafariki na yeye kuanza kuhubir injili alikuwa anafanya nini kwa akili zako unadhani mtu ambaye maisha yake yote kajifunza useremala tu. Note dingi yake alianza kuvuta kabla ya yy kuanza kuhubir
Hapo kweny kuitunz familia yke baada ya mzee wake kufariki Nina swali.Yesu alioanza huduma akiwa nawanafunzi wake,alikuwepo Yuda ambaye pamoja namajukumu mengine Ila ndo alikuwa mtunza fedha.Je,pesa walizitoa wapi ili zitunzwe na kuratibiwa na Yuda?
 
Labda neno "mfanyabiashara" ndio linatupa shida.
Hivi mfano mimi nikiwa fundi radio au fundi viatu ni mfanya biashara au sio mfanyabiashara?
 
Injili inapoanzia hadi Yesu alipopaa.Usome kwa kutulia.
yani nisme tangu injili ilipoanza hadi mwisho ,acha ukichaa bas,nipe kipengele cha hilo andiko nikasome kama huna kaa kimya ficha unjinga wako mbele za watu
 
Hebu tuweke sawa hapa. Yesu hakuwa mfanyabiashara, na wala hakuja duniani kwa lengo hilo. Yesu alikuja duniani kwa lengo moja tu, nalo ni ukombozi. Mambo mengine aliyofanya, alifanya kama binadamu anavyofanya shughuli za kila siku, maana alikuja duniani kama binadamu, lakini akiwa na Uungu.

Kuzaliwa katika familia ya Yosefu, ukoo wa Daudi, ilimpasa kufuata mila na desturi za ukoo huo, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali. Baba yake (mrithi) alikuwa seremala, na kama ilivyo ada, mafundi seremala huuza samani wanazotengeneza ili kujipatia kipato. Hivyo, kuna wakati Yosefu alimtuma Yesu kupeleka samani hizo mahali zilipohitajika.

Akiwa katika umri mdogo, Yesu aliishi maisha ya kawaida kama walivyoishi wazazi wake (Yosefu na Maria). Inasemekana, wakati mwingine walikutana na wakati mgumu, hata samani alizotengeneza Yosefu hazikupata wateja na kupelekea kushindwa kununua chakula, hivyo wote kulala njaa. Hivyo, Yesu kama binadamu (maana ni Mungu pia), aliishi kama binadamu wengine.
familia ya yesu walikua matajiri hii inaonyesha biashara yao ilikua ni kubwa na ya mafanikio,yesu alipotaka kuuawa na herodi,familia ilienda kujificha nchi za nje( Misri) kwa kipindi hicho kumudu kwenda nchi za nje na ukamudu maisha ya huko mpaka herode alipofariki hao sio masikini
 
Kwani ukiwa mwana wa Daktari lazima weww uwe daktari? Biblia inayema alikuwa Mwana wa Seremala ikimaanisha kuwa Seremala ni Yoseph na sii Yesu
ficha upumbavu wako basi umeonyeshwa maandiko mawili alikua mwana wa seremala,na jingine (Marko) alikua seremala ,acheni upumbavu basi wa kujifanya vipofu
 
Nasubiri mstari...!
Sio maelezo na speculation but mstari unaoonesha Yesu alifanya biashara. Vinginevyo ukubaliane na wanaosema chochote kuhusu Yesu ambacho hakiko kwenye Biblia!
Ni sawa na kusema MO kumiliki kiwanda cha Vinywaji ni nesi. Nikikwambia ni mfanyabiashara utake uthibitisho
 
Yesu sio Mkristo,Watu unaowazungumzia ni tofauti. Hata kama wanafuata mafundisho yake, sawa, ila sio maisha yake.
 
Back
Top Bottom