Yesu atakuja kama Lopelope alivyofanya leo!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Wapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hakuonekana. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Lopelope amezingua! Kwanini hajatokea?”

Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)

Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.

Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.

Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni, wote waliotubu dhambi zao na kumwamini.

Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tuwe tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; kisha dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
 
Wapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hajatokea. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Kwanini Lopelope hajatokea?”

Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua atawanyakua wote waliotubu dhambi zao na kumwamini, na kuwapeleka mbinguni.

Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tujiweke tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; na dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Inafikirisha
 
Wahuni si watu wazuri. Muhimu kuwa macho na usalama wake pia.
 
Biblia inasema usiku wa manane.

Kwa hiyo Polepole anaingia at 00.00?

One hour to go, right?
 
Duniani kuna mengi. Kua uyaone!

Wanasema jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza. Hadi atakapotokea Polepole sidhani ni sahihi kufanya speculation.

Kolimba, Mwaikambo, Sokoine na hata Nyerere wànajulikana kuweka miadi kwa siku ambazo kwa mshangao hawakuziishi.

Yote Kwa yote, futungo si watu wazuri.
 
Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.
2 Petro 3:9
"Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali anawavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote watubu."
 
Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni, wote waliotubu dhambi zao na kumwamini.
1 Wathesalonike 4:16-17
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."
 
1 Wakorintho 15:51
"Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika."
 
Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku.
Ufunuo 22:12
"Tazama, naja upesi, na malipo yangu yako pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo."
 
Wapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hakuonekana. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Lopelope amezingua! Kwanini hajatokea?”

Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)

Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.

Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.

Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni, wote waliotubu dhambi zao na kumwamini.

Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tuwe tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; kisha dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Amen
 
1 Wathesalonike 4:16-17
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."
Hili tukio litakuwa Breaking News katika vyombo vyote vya habari.
 
Setfree Hiyo aya maana yake nini
Waliokufa katika Kristo maana yake ni watu waliofariki wakiwa wameokoka. Kwa maneno mengine, ukitubu dhambi zako na kumwamini Kristo, ukifa, unahesabika umekufa katika Kristo. Kwahiyo waliokufa katika Kristo ndio watakaofufuliwa kwanza siku Yesu akija.
 
Ufunuo 22:20
"Yeye ashuhudiaye haya asema, Naam, naja upesi. Amina. Njoo, Bwana Yesu."
 
Back
Top Bottom