InafikirishaWapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hajatokea. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Kwanini Lopelope hajatokea?”
Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)
Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.
Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.
Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua atawanyakua wote waliotubu dhambi zao na kumwamini, na kuwapeleka mbinguni.
Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tujiweke tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; na dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Wapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hajatokea. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Kwanini Lopelope hajatokea?”
Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)
Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.
Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.
Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua atawanyakua wote waliotubu dhambi zao na kumwamini, na kuwapeleka mbinguni.
Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tujiweke tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; na dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Duniani kuna mengi. Kua uyaone!Wahuni si watu wazuri. Muhimu kuwa macho na usalama wake pia.
Duniani kuna mengi. Kua uyaone!
2 Petro 3:9Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.
1 Wathesalonike 4:16-17Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni, wote waliotubu dhambi zao na kumwamini.
1 Wakorintho 15:51Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni, wote waliotubu dhambi zao na kumwamini.
Nakua mtazamaji kwenye hili la LopelopeDuh, unasubiri Yesu aje uwe mtazamaji tutakavyokuwa tukipaa mbinguni na wewe ukibaki duniani kwenye dhiki kuu?!!
AmenWapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hakuonekana. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Lopelope amezingua! Kwanini hajatokea?”
Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)
Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.
Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.
Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni, wote waliotubu dhambi zao na kumwamini.
Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tuwe tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; kisha dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Hili tukio litakuwa Breaking News katika vyombo vyote vya habari.1 Wathesalonike 4:16-17
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."
Waliokufa katika Kristo maana yake ni watu waliofariki wakiwa wameokoka. Kwa maneno mengine, ukitubu dhambi zako na kumwamini Kristo, ukifa, unahesabika umekufa katika Kristo. Kwahiyo waliokufa katika Kristo ndio watakaofufuliwa kwanza siku Yesu akija.Setfree Hiyo aya maana yake nini