Yesu hakuwa na Kanisa wala pesa, hakuacha hata hao wakristo. Je, hawa wanapata wapi haya wanayofanya?

Yesu hakuwa na Kanisa wala pesa, hakuacha hata hao wakristo. Je, hawa wanapata wapi haya wanayofanya?

Kwa waliosoma na kuelewa habari za Yesu watakubaliana nami yafuatayo:

Mosi, alikuwa maskini au lofa wa kawaida mwana wa seremala ambaye kama angerudi leo na kukuta wanaomhubiri na utajiri wao haramu, angezimia mbali na kuwakaripia hata kuwachapa.

Pili, hakuwahi kuwa na wala kuingia kanisani.
Tatu, aliingia kwenye masinagogi na kuhubiri humo.
Nne, aliacha wanafunzi na si wakristo.

Tano, hadi anaondoka, hakuwahi kusikia neno ukristo.
Sita, hakujitangaza kuwa alikuwa akitenda miujiza kama hawa majizi wa sasa wanaomtumia na kumsingizia.

Saba, alisema wazi kuwa alikuja kwa ajili ya kabila 12 za Israel ingawa tapeli Sauli baadaye Paulo alikuja na kugeuza kila kitu kiasi cha kuunda dhehebu ndani ya dhehebu.

Nane, hakupenda sifa wala ujiko kama haya majizi ya sasa yanayotumia runinga kuwaibia mazwazwa.

Tisa, hakuwahi kushirikiana na serikali kwa vile alijua uhovyo na uovu wake.

Kumi, hakuacha uislam ambao nao ulimdandia kujifanya unamtambua ili kuwanasa wakristo.

Kumi na moja, alipenda kukaa na watu wa tabaka la chini na siyo wakwasi na wenye madaraka.

Kumi na mbili, hauandika wala kuacha biblia.

Je wewe unasemaje?
Unatarajia Yesu kwenda kanisa lipi wakati hapakuwa na kanisa? Isitoshe kanisa sio jengo bali ni watu. Yesu ndiye aliyeanzisha kanisa na anaendelea kulijenga na kuliendeleza!
 
Sio kweli.. Unaongea usichokijua
Wewe mtu mweusi uliekutwa unakula mbegu na mizizi huko maporini, na kutwaliwa kama mtumwa, halafu ukafundishwa kuamini kitu hakihusiana kabisa na mila zako, ndio leo hii unajua baada kujua kuvaa nguo maana ulikuwa umevaa magome ya miti
 
Unatarajia Yesu kwenda kanisa lipi wakati hapakuwa na kanisa? Isitoshe kanisa sio jengo bali ni watu. Yesu ndiye aliyeanzisha kanisa na anaendelea kulijenga na kuliendeleza!
Kama halikuwepo zaidi ya wanafunzi wake, kwanini lianzishwe baada yake? Yeye alisema kanisa ni watu zaidi ya mmoja wanapokutanika na siyo jengo. Kwanini majengo sasa? Kwanini maduka ya kuchuuza roho za watu?
 
Yesu hakuwa lofa, alikuwa seremala kabda hajaingia kwenye injili, na seremala walikuwa na fedha nzuri nyakati hizo...lofa anakuwa na mshika fedha(mfuko),unadhani kulisha wanaume 12 na wale wamama ni hela kidogo?
 
Maneno haya kazungumza mwenyewe yesu ama?
Biblia yote vitabu 66 sura 1189, na mistari 31101 imeandikwa na Yesu mwenyewe kupitia wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hakuna mwanadamu aliyeweza andiko Biblia maana pasipo na Roho sisi hatuwezi lolote.
 
Nyerere aliitwa baba wa Taifa baada ya kufa, watu waliitwa walutheli baada ya Martini Luther kuondoka, watu wasingeweza kuitwa wakristo wakati Kristo mwenyewe yupo, Ni baada ya kuondoka ndio wanaulizana, hawa ni akina nani, wanajibiwa ni wafuasi wa yule aliyeitwa Kristo
 
Wewe mtu mweusi uliekutwa unakula mbegu na mizizi huko maporini, na kutwaliwa kama mtumwa, halafu ukafundishwa kuamini kitu hakihusiana kabisa na mila zako, ndio leo hii unajua baada kujua kuvaa nguo maana ulikuwa umevaa magome ya miti
Biblia imeweka wazi tuwe moto au Baridi sio vuguvugu maana yake wanadadamu tunaongozwa na Roho wa Mungu ah roho wa shetani. Ukiona Mtu anajifanya kupinga mambo ya imani ujue ndani yake wanaongozwa na roho wa shetani
 
Maneno haya kazungumza mwenyewe yesu ama?
B8blia yote au maneno yote ya kwenye Biblia yaliandikwa au kusemwa na Yesu mwenyewe kupitia wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Pasipo na Roho mwanadamu hawezi lolote.
 
Nguvu hii tuieekeze kwenye uzalishaji yaani tulazimishe uzalishaji mali iwe kilimo ama ufugaji hata ujasiliamali mdogomdogo wa kutengeneza sabuni au hata Vijiti vya kuwashia moto. Amini tutasonhesha Taifa letu kuwa na uchumi imara zaidi
 
Yesu hakuwa lofa, alikuwa seremala kabda hajaingia kwenye injili, na seremala walikuwa na fedha nzuri nyakati hizo...lofa anakuwa na mshika fedha(mfuko),unadhani kulisha wanaume 12 na wale wamama ni hela kidogo?
Kwani hivyo vyakula alinunua kama kweli alifanya hivyo?
 
B8blia yote au maneno yote ya kwenye Biblia yaliandikwa au kusemwa na Yesu mwenyewe kupitia wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Pasipo na Roho mwanadamu hawezi lolote.
Porojo Kama porojo zingine.
 
Kwani wewe imani hiyo inakuhusu nn kwamba wewe una akili kuliko wakristo wote duniani
 
Kwani hivyo vyakula alinunua kama kweli alifanya hivyo?
Sasa mkuu,utadhurula na lile kundi bila kula? Lazima alikua na means...na mtunza hazina alikuwapo. Kuna pahala Yesu alidaiwa Kodi akawatuma wanafunzi wakachukue kwenye kinywa Cha samaki(ATM) walipe Kodi.
Baba yake na yeye walikuwa ni seremala,mama yake mtu catering (kumbuka kule kana shughuli aliyokuwa anafanya mama Yesu alipoenda na Yesu na akafanya muujiza wa kwanza). So hakutokea familia ya kinyonge.
Hapo bado hazina yake ya dhahabu,manemane n.k alizopewa na mamajusi,hujiulizi kwanini vazi la Yesu askari waling'ang'ania(askari wanazingua toka kitambo 😂😂)? Lilikua la thamani kitambaa chake
 
Ukristo ni Nini, Ukristo maana yake ni "Wafuasi wa Kristo"

Yesu wa Nazareth ni nani?

Mnamo miaka ya Karne ya Kwanza AD Wayahudi katika nchi ya Judea walikuwa wamekuwa chini ya Wakoloni wa aina Mbili Warumi na Wagiriki mwisho wa Utawala wa Ugiriki, Wayahudi walishirikiana na Warumi kuwatoa wa Wagiriki katika Mapinduzi ya Wamakabayo na kuunda Nchi inaitwa "Hasmonean dynasty" iliyodumu karibu Miaka 100 ikiwa kama vassal state ya Roman Empire baadae Warumi wakama wanataka na hiyo nchi Ndio wakaunda Puppet kingdom inaitwa Herodean kingdom.

Katika kipindi Cha Tawala za Kigeni Wayahudi walianza kuwa na muhamko kuwa Messiah atakuja na kuwakoboa kutoka kwenye Ukoloni.

Katika kipindi hichi Wayahudi waligawanyika katika makundi 5-6 (Moja wapo liliitwa Wakristo) na kulikuwa Watu wengi walikuwa wanajiita Messiah, ila alikuwepo Kiongozi mmoja wa Kiyahudi anaitwa "Yesu wa Nazareth" yeye alikuwa hakubaliani na Idea ya kupigana na Dola ya Rumi sababu ni lost war, pili alikuwa anaamini ukombozi wa mwanadamu unaanzia ndani ya mtu mwenyewe na sio community (Kila mtu abebe msalaba wake), Yeye alikuwa anaamini kuwa Sheria/Amri kubwa kwa mwanadamu ni Kuwapenda Watu wengine kama anavojipenda, So alipata wafuasi wengi ambao walikusanya taarifa za Maisha na mafundisho yake na wakaunda Jumuiya sehemu mbali mbali wakawa wanatumiana Barua, wakaunda Taasisi za kuwakutanisha Wakristo wakijadili Imani na Maisha kwa Ujumla mwisho wa siku wakawa wameunda Kanisa/Ukristo kama ulivo leo
 
Biblia imeweka wazi tuwe moto au Baridi sio vuguvugu maana yake wanadadamu tunaongozwa na Roho wa Mungu ah roho wa shetani. Ukiona Mtu anajifanya kupinga mambo ya imani ujue ndani yake wanaongozwa na roho wa shetani
Bibilia ndio ndio nini?
Au unamaanisha lile kitabu la hekaya za kale?
Babu yako wa babu yako nae pia ana hizo hekaya za shujaa wake mwenye ngozi nyeusi kama yake

1736372780282.png
 
Wewe mtu mweusi uliekutwa unakula mbegu na mizizi huko maporini, na kutwaliwa kama mtumwa, halafu ukafundishwa kuamini kitu hakihusiana kabisa na mila zako, ndio leo hii unajua baada kujua kuvaa nguo maana ulikuwa umevaa magome ya miti
Kuchagua ni kwako, uamini au usiamini lakini kweli inasemwa. Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima.
 
Kuchagua ni kwako, uamini au usiamini lakini kweli inasemwa. Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima.
Babu zetu waliuuzwa wazimawazima, lakini siwalaumu kwa sababu walizidiwa nguvu za nyenzo kama bunduki
Kuna waliojanjaruka kama Mtemi Mirambo na Mkwawa
Lakini watu kama nyinyi ndio majanga, mmeuzwa kiakili......
 
Back
Top Bottom