Ahead
JF-Expert Member
- Jan 11, 2013
- 2,292
- 2,566
Ndugu tujiandae kwa ujio wa Yesu mara ya pili, mara hii ya pili harudi kama hapo kwanza. Safari hii akirudi anarudi na utukufu mkuu kulinyakua kanisa, ndugu usiwe mbishi hata kipindi cha Nuhu,alijenga safina miaka mingi na watu walimdhihaki mpaka siku ambayo Mungu alileta mvua kubwa watu na vyote vikaangamia.
Hata sasa tunamhubiri Kristo lakini mnadhihaki na kusema siku ya mwisho haipo, siku ya mwisho ni pale unapokufa ndugu usijidanganye mwisho upo fanya maamuzi leo uokoke na Mungu akupe amani duniani na mbinguni.
Mpendwa usijihesabie haki kwa kusema matendo yangu mema pekee yatanipeleka mbinguni, usiseme mimi msabato, mimi ni romani, mTAG, muislamu hivyo nitakwenda tu mbinguni, hapana lazima uokoke kwa kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi yaani kuokoka.
Muhimu: Hakuna shortcut ya kwenda mbinguni ni lazima upitie kwa Yesu Kristo bila Yesu ni jehanamu ya moto ushahidi huu hapa;
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yohana 14:6
Basi mpendwa wangu wokovu kuupata si kazi ngumu kama unavyodhani kazi yako ni moja tu,kumkiri Yesu kwa kinywa chako sawasawa na maelekezo yaliyopo kwenye neno la Mungu hili;
8 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
Warumi 10:8
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Warumi 10:9
Ikiwa unataka kuokoka omba sara hii kwa imani;
Ee Bwana Yesu!naomba unisamehe dhambi zangu,futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu,andika jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele,nakupokea ndani ya moyo wangu uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu,amen!
Ikiwa umeomba sara hii nakuhakikishia umekuwa mwana wa Mungu kwa kuzaliwa kwa mara ya pili kwa njia ya Yesu Kristo.Kuanzia sasa umeokoka,Yesu anasema usitende dhambi tena,nenda kwenye kanisa lolote linaloamini wokovu waambie niliokoka JamiiForum watakusaidia kuukulia wokovu na hakika utamwona Mungu duniani na Mbinguni,Ubarikiwe nimekuandikia haya yote kwa pendo la Mungu.