Yesu Kristo angeishi nyakati hizi angepotezwa mapema sana..... Soma hapa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Nimetafakari sana inawezekanaje kuwa na matukio maovu yanayoendelea huku kukiwa na watu wengi wanaojitambulisha kama wafuasi wa Yesu Kristo ambaye kwa imani yetu alikuwa mtu mwema asiyetenda maovu?

Baada ya tafakuri yangu nimeona ni wazi kwamba Yesu angefanya kazi zake kwa wakati huu asingetoboa hata miezi 6 bila jambo baya kumkuta. Na pia sio Yuda na Petro tu wangemsaliti. Nadhani karibu wote tunaojiita wakristo tungemsaliti mapema sana.

Tuangalie maisha ya Yesu kwa mujibu hasa kwenye baadhi ya tabia na matukio yake ili tuone ni kiasi gani kizazi hiki kingemfanyia ukatili wa kutisha.

1. Yesu alikuwa sio mtu wa blahblah alikuwa anajibu kwa ufupi sana tena maswali yake. Wengi tungemwita mjuaji na kiburi.

2. Aliteua wafuasi waliokuwa wanaume tu. Hapa wale wanaharakati wa 50 kwa 50 wangechonga sana

3. Wengi tungemwona kachanganyikiwa yeye na wafuasi wake kwa kuacha kazi zao na kuanza kueneza injili. Ikumbukwe Yesu alikuwa na ujuzi wa seremala huku wafuasi wake pia wakiwa na profession mbalimbali. Ikumbukwe kwa muda wote wa miaka mitatu ya Yesu kwenye kazi yake haijawahi kutajwa kama alikuwa akijihusisha na kingine chochote kile.

4. Siku alipopindua meza za wanyabiashara ndogondogo hekaluni angepata upinzani mkali sana toka kwa wananchi na kumlaumu hajui shida za wananchi wa hali ya chini. Nina uhakika Yesu asingeunga mkono hawa machinga wanaopanga biashara zao kwenye mazingira hatarishi.

5. Hawa wachungaji na manabii feki wangemchukia mno maana angewapinga hadharani upuuzi wanaoufanya.

6. Wazee wa taarifa za kiitelijensia wangemsumbua sana. Yesu alikuwa akionekana sehemu basi watu watajaa hapo kumsikiliza au kumfuata kila anapoenda. Mfano kundi la watu 5000 waliomfuata ikabidi atende muujiza wa kuwapatia msosi. Kwa ile mikusanyiko huenda FFU wangekuwa wanatoa kichapo mara kwa mara.

7. Angepewa kesi kuhusiana na rushwa kwa mambo aliyokuwa anafanya.

8. Angepata kashfa mitandaoni ya kutembea na yule binti kahaba aliyemtetea.

9. Watu wa udaku wangemwandama sana Mariamu Magdalene kwamba anatoka kimapenzi na mwokozi.

10. Kama ilivyotokea kwa wakati ule basi hata leo angepewa tu kesi ya uhaini au angepotezwa tu na wasiojulikana.

Nimeandika huu uzi kuwasihi waumini wenzangu wa madhehebu ya kikristo tuache unafiki wa kusema tunampenda Yesu huku tukiendelea kufanya maovu tofauti na maelekezo yake.
 
Nimetafakari sana inawezekanaje kuwa na matukio maovu yanayoendelea huku kukiwa na watu wengi wanaojitambulisha kama wafuasi wa Yesu Kristo ambaye kwa imani yetu alikuwa mtu mwema asiyetenda maovu? Baada ya tafakuri yangu nimeona ni wazi kwamba Yesu angefanya kazi zake kwa wakati huu asingetoboa hata miezi 6 bila jambo baya kumkuta. Na pia sio Yuda na Petro tu wangemsaliti. Nadhani karibu wote tunaojiita wakristo tungemsaliti mapema sana.

Tuangalie maisha ya Yesu kwa mujibu hasa kwenye baadhi ya tabia na matukio yake ili tuone ni kiasi gani kizazi hiki kingemfanyia ukatili wa kutisha.
1. Yesu alikuwa sio mtu wa blahblah alikuwa anajibu kwa ufupi sana tena maswali yake. Wengi tungemwita mjuaji na kiburi.
2. Aliteua wafuasi waliokuwa wanaume tu. Hapa wale wanaharakati wa 50 kwa 50 wangechonga sana
3. Wengi tungemwona kachanganyikiwa yeye na wafuasi wake kwa kuacha kazi zao na kuanza kueneza injili. Ikumbukwe Yesu alikuwa na ujuzi wa seremala huku wafuasi wake pia wakiwa na profession mbalimbali. Ikumbukwe kwa muda wote wa miaka mitatu ya Yesu kwenye kazi yake haijawahi kutajwa kama alikuwa akijihusisha na kingine chochote kile.
4. Siku alipopindua meza za wanyabiashara ndogondogo hekaluni angepata upinzani mkali sana toka kwa wananchi na kumlaumu hajui shida za wananchi wa hali ya chini. Nina uhakika Yesu asingeunga mkono hawa machinga wanaopanga biashara zao kwenye mazingira hatarishi.
5. Hawa wachungaji na manabii feki wangemchukia mno maana angewapinga hadharani upuuzi wanaoufanya.
6. Wazee wa taarifa za kiitelijensia wangemsumbua sana. Yesu alikuwa akionekana sehemu basi watu watajaa hapo kumsikiliza au kumfuata kila anapoenda. Mfano kundi la watu 5000 waliomfuata ikabidi atende muujiza wa kuwapatia msosi. Kwa ile mikusanyiko huenda FFU wangekuwa wanatoa kichapo mara kwa mara.
7. Angepewa kesi kuhusiana na rushwa kwa mambo aliyokuwa anafanya.
8. Angepata kashfa mitandaoni ya kutembea na yule binti kahaba aliyemtetea.
9. Watu wa udaku wangemwandama sana Mariamu Magdalene kwamba anatoka kimapenzi na mwokozi.
10. Kama ilivyotokea kwa wakati ule basi hata leo angepewa tu kesi ya uhaini au angepotezwa tu na wasiojulikana.

Nimeandika huu uzi kuwasihi waumini wenzangu wa madhehebu ya kikristo tuache unafiki wa kusema tunampenda Yesu huku tukiendelea kufanya maovu tofauti na maelek
Sijui utanielewa?
 
Nimetafakari sana inawezekanaje kuwa na matukio maovu yanayoendelea huku kukiwa na watu wengi wanaojitambulisha kama wafuasi wa Yesu Kristo ambaye kwa imani yetu alikuwa mtu mwema asiyetenda maovu?

Baada ya tafakuri yangu nimeona ni wazi kwamba Yesu angefanya kazi zake kwa wakati huu asingetoboa hata miezi 6 bila jambo baya kumkuta. Na pia sio Yuda na Petro tu wangemsaliti. Nadhani karibu wote tunaojiita wakristo tungemsaliti mapema sana.

Tuangalie maisha ya Yesu kwa mujibu hasa kwenye baadhi ya tabia na matukio yake ili tuone ni kiasi gani kizazi hiki kingemfanyia ukatili wa kutisha.

1. Yesu alikuwa sio mtu wa blahblah alikuwa anajibu kwa ufupi sana tena maswali yake. Wengi tungemwita mjuaji na kiburi.

2. Aliteua wafuasi waliokuwa wanaume tu. Hapa wale wanaharakati wa 50 kwa 50 wangechonga sana

3. Wengi tungemwona kachanganyikiwa yeye na wafuasi wake kwa kuacha kazi zao na kuanza kueneza injili. Ikumbukwe Yesu alikuwa na ujuzi wa seremala huku wafuasi wake pia wakiwa na profession mbalimbali. Ikumbukwe kwa muda wote wa miaka mitatu ya Yesu kwenye kazi yake haijawahi kutajwa kama alikuwa akijihusisha na kingine chochote kile.

4. Siku alipopindua meza za wanyabiashara ndogondogo hekaluni angepata upinzani mkali sana toka kwa wananchi na kumlaumu hajui shida za wananchi wa hali ya chini. Nina uhakika Yesu asingeunga mkono hawa machinga wanaopanga biashara zao kwenye mazingira hatarishi.

5. Hawa wachungaji na manabii feki wangemchukia mno maana angewapinga hadharani upuuzi wanaoufanya.

6. Wazee wa taarifa za kiitelijensia wangemsumbua sana. Yesu alikuwa akionekana sehemu basi watu watajaa hapo kumsikiliza au kumfuata kila anapoenda. Mfano kundi la watu 5000 waliomfuata ikabidi atende muujiza wa kuwapatia msosi. Kwa ile mikusanyiko huenda FFU wangekuwa wanatoa kichapo mara kwa mara.

7. Angepewa kesi kuhusiana na rushwa kwa mambo aliyokuwa anafanya.

8. Angepata kashfa mitandaoni ya kutembea na yule binti kahaba aliyemtetea.

9. Watu wa udaku wangemwandama sana Mariamu Magdalene kwamba anatoka kimapenzi na mwokozi.

10. Kama ilivyotokea kwa wakati ule basi hata leo angepewa tu kesi ya uhaini au angepotezwa tu na wasiojulikana.

Nimeandika huu uzi kuwasihi waumini wenzangu wa madhehebu ya kikristo tuache unafiki wa kusema tunampenda Yesu huku tukiendelea kufanya maovu tofauti na maelekezo yake.
Namba 4 umeiandika kimkakati sana. Ila waliosoma urusi wamekuelewa.

Namba 5 isingekuwepo kwasababu wachungaji wote na manabii fake wanafanya kazi zao kwa mgongo wa Yesu.
 
Back
Top Bottom