Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Hivi wewe hasa unataka nini?. Yeye aliuweka mdomo anashindwaje kula?. Alyeuweka m***ndu atashindwaje kun**a?. Acha zako wewe.
 
Uliza swali hili kwa nini Yesu alikuja duniani?. Kuliko kumwaga upumbavu humu.
 
Uliza swali hili kwa nini Yesu alikuja duniani?. Kuliko kumwaga upumbavu humu.


Halafu najiuliza...Mungu tena atakujaje duniani, wkt yeye yupo kila mahali anakuona ndie alieumba mbingu na nchi?
 
Haya tumekusoma ila wengine tunaamin kitabu kitakatifu nacho ni bible baaas
 
Yesu ni mwana wa Mungu. Mungu ana nafsi tatu Baba, Mwana na Roho mtakatifu wote ni umoja..
 
Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele YOHANA 3:16 Mwana wa MUNGU ni MUNGU
 
Acha upotoshaji
Yesu hakuhitaji kujitambulisha kuwa Yeye ni Mungu japo alifanya hivo. Ila Mungu mwenyewe alimutamtambulisha kuwa ni Mungu. Kabla ya kuanza huduma hapa duniani Mungu alianza kwa utambulisho juu ya nani anawahudumia;

Mathayo 3:17 Biblia inasema sauti toka juu mbinguni ilisikika kusema "Huyu ndiye mwanangu Mpendwa ninaependezwa nae, msikilizeni yeye".

Utambulisho huu haukutokea tu wakati baada ya kuzaliwa. Utambulisho wa kuwa Yesu ni Mungu atakayekuja duniani ulitabiriwa miaka takribani 600 kabla kutokea duniani kwa sura ya mwanadamu wa kawaida. Nabii isaya 7:14 anandika "Tazama bikira atachukua mimba naye atazaa mtoto wa kiume na ataitwa IMANUELI yaani MUNGU PAMOJA NASI".

Neno emnauel lilitafsiriwa kuwa maana yake ni Mungu ambaye yuko pamoja na sisi wanadamu. Na ndivyo ilivyotokea Bikira maria akamzaa mwana wa kiume kama ilivyotabiriwa. Utabiri huu ulirudiwa na Mathayo wakati wa kuzaliwa Yesu ( MATHAYO 1:23-25 ) Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”
Injili ya Yohana inarudi nyuma zaidi hata kabla ya Isaya. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo"(Yn. 1: 1-3)
. Kwa lugha rahisi ni kwamba hapo mwanzo kulikwako YESU, naye YESU alikuwako kwa MUNGU, naye YESU alikuwa MUNGU. na vyote vilivyoumbwa viliumbwa na yeye. Lakini pia Yesu ktk mambo mengi aliyosema na kutenda yalimtambulisha kuwa yeye ni Mungu. Mojawapo ni hii "Wakusanyikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo kati yao" Mwenye uwezo wa kuwepo mahali popote ni MUNGU peke yake.

MTOA MADA, NAKUSHAURI UMKUBALI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO
 
Pamoja.na mafundisho yoote, hata mimi akili yangu imekataa kukubali kuwa Yesu ni Mungu,imekataa hasa, naji force tu. Na kariibu ntafanya maamuzi.
 
Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele YOHANA 3:16 Mwana wa MUNGU ni MUNGU
yeah,mwana wa mungu ni mungu na mungu ndo mwanawa mungu kwa maana ya emanueli..

Ila kama huna roho mtakatifu huwezi kuelewa,mpaka roho mtakatifu akuingie kama alivyomwingia bikira maria
 
mtoa mada ni mwanakondoo mwenzako,sema yeye alishajielewa siku nyingi,haoni shida kujadili vitu kama hivi
 
hiyo aya ya isaya 7:14 haimuhusu yesu mkuu,ila kwasababu inasaidia kukufariji basi endelea kuamini hivyo for your peace of mind.
 
Nilichoeleza mimi ni kwamba Yesu sio Mungu. Na ndio maana nimetoa andiko la yohana 20:17 yesu akisema kuwa Mungu wake anayemuabudu yeye ndio Mungu wetu sisi sote. Sasa toa wewe ufafanuzi wa yohana 20:17

Hapo Yesu aliongea akiwa ktk hali ya ubinadamu kamili,..jee Mungu hawezi maajabu hayo?¿
 
Alikuja kwa walio wake lakini wakamkataa Bali wale waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa mungu.. Ndio wale waliaminilo jina lake..
 
Sasa kama ana uwezo wa kila kitu kwa nini atumie nguvu kujibadilisha binadamu ili watu wamwelewe kwa nini asitumie seconds tu kuwafanya binadamu wabadilike?
Mbona allah anatumia waislamu kufanya jihadi kuua makafiri.. Kwenye Quran anasema ataadhibu makafir kupitia mikono yenu.. Kwa nini asiadhibu yeye nwenyewe.? Kwa nini watu wajilipue kwa kufanya jihadi wakati alah anaweza kutumia seconds tu kutengeneza bomu.
 
Kama sisi ambavyo hatuikubali Quran tunaona takataka Na huyo mtume wenu tunamuona fake
 

NIPMEIPATA HII KWENYE RESEARCH ZANGU NAONA ITAKUSAIDIA NDUGU YANGU

Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!

Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…