Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Acha utoto wewe kama kweli yeye mungu mbona alivyokuwa msalabani akasema mungu wangu mungu wangu mbona umeniacha kama yeye ni mungu na huyu aliye kuwa anamlalamikia ni nani?nikuongeze kitu kingine mungu gani anakaa tumboni miez 9,anakula anakunywa a naenda haja dah .umeharibiwa akili na vitabu walivyotunga wajanja.lete hoja nikuelewa Acha kufikiri kwa ma kalio ww aafu unakuja hapa kutokwa povu we unaona umejiiibu Acha uk******laza
Hivi wewe hasa unataka nini?. Yeye aliuweka mdomo anashindwaje kula?. Alyeuweka m***ndu atashindwaje kun**a?. Acha zako wewe.
 
Nawaza tu
1. Kwa kuwa Yesu ni Mungu na Mungu huyo alizaliwa na bikira Maria basi nathubutu kusema bikira Maria ni mkubwa kuliko Yesu(Mungu) maana mtoto kwa mama atabaki kuwa mtoto tu.Hivyo utukufu wa juu kabisa ni wake Maria maana ndo aliyemzaa Mungu wenu.
2.Kwa mujibu wa maandiko yenu, Yesu alikufa na siku ya tatu akafufuka.Hiyo ina maana kuwa dunia ilikaa siku 3 bila Mungu. Je nani aliiongoza dunia kwa muda huo wa siku 3?
4.Ninavyofaham uwezo wa Mungu hauna limit, ana uwezo wa kujua ya jana ,leo na kesho, hivyo Yesu(kama kweli ni Mungu) kabla ya ujio wake duniani alishaona kitakachomtokea.Kwani alikubali kuja kudhalilika? Kwanini aliionesha dunia kuna watu wana uwezo zaidi yake (waliomtesa msalabani) ilhali ye ni Mungu muweza wa yote.
3.Kama kweli yeye Yesu ni Mungu kwanini alikuja dunian? Kwanini alishindwa kuuumba kiumbe chenye uwezo wa kufanya hiyo kazi iliyomleta yeye duniani? Haoni kuwa kitendo cha yeye kuja duniani na kuteswa kama viumbe wengine dhaifu kimechangia kupunguza imaani kwa baadhi ya watu (mfano Mimi siamini kabisa Mungu muweza wa yote anaweza kuteswa na kiumbe alichokiumba mwenyewe)
Maswali ni mengi lkn acha niishie hapa [emoji124]
Uliza swali hili kwa nini Yesu alikuja duniani?. Kuliko kumwaga upumbavu humu.
 
Uliza swali hili kwa nini Yesu alikuja duniani?. Kuliko kumwaga upumbavu humu.


Halafu najiuliza...Mungu tena atakujaje duniani, wkt yeye yupo kila mahali anakuona ndie alieumba mbingu na nchi?
 
Wacha kudanganya , WEWE KAMA SI MCHUNGAJI MWENYE NJAA KALI, MAXI SHIMBA UTAKUWA NI MWANAFUNZI WAKE


sura alhadeed haisemi hivyo ,

unajaribu KUCHUKUWA AYA ZA QURAN NA KUZICHANGANYA NA ZA BIBLIA , UNAMPAKAZIA YESU UUNGU


KATAFUTE MAVI YA KUKU UBANJE


HII HAPA NI SURA AL H`ADIID

57 - AL -H'ADIID

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.


1.Kinamsabihi kumtakasa Mwenyezi Mungu kila kiliomo ndani ya mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.


2.
Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye uweza wa kila kitu.


3.
Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.


4.
Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akakaa vyema juu ya enzi. Anayajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni, na yanayo panda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayo yatenda.


5.
Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake. Na mambo yote yanarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu.


6.
Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku. Na Yeye ni Mwenye kuyajua yaliomo vifuani.


7.
Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na toeni katika alivyo kufanyeni nyinyi kuwa ni waangalizi wake. Basi walio amini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa.


8.
Na mna nini hata hamumuamini Mwenyezi Mungu na hali Mtume anakuiteni mumuamini Mola wenu Mlezi? Naye amekwisha chukua ahadi yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini.


9.
Yeye ndiye anaye mteremshia mja wake Aya zinazo bainisha wazi ili akutoeni gizani muingie kwenye nuru. Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole, Mwenye kurehemu.


10.
Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa miongoni mwenu wenye kutoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walio toa baadae na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.


11.
Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie mardufu, na apate malipo ya ukarimu.


12.
Siku utakapo waona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao, na kuliani kwao: Furaha yenu leo - Bustani zipitazo mito kati yake mtakaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.


13.
Siku wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake watapo waambia walio amini: Tungojeni ili tupate mwangaza katika nuru yenu. Waambiwe: Rejeeni nyuma yenu mkaitafute nuru! Utiwe baina yao ukuta wenye mlango - ndani yake mna rehema, na nje upande wake wa mbele kuna adhabu.


14.
Watawaita wawaambie: Kwani vile hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkasitasita, na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni. mpaka ilipo kuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.


15.
Basi leo haitapokelewa kwenu fidia, wala kwa wale walio kufuru. Makaazi yenu ni Motoni, ndio bora kwenu; na ni marejeo maovu yalioje!


16.
Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu.


17.
Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.


18.
Kwa hakika wanaume wanao toa sadaka, na wanawake wanao toa sadaka, na wakamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, watazidishiwa mardufu na watapata malipo ya ukarimu.


19.
Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, hao ndio Masidiqi na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao. Na walio kufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni.


20.
Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na magh**** kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.


21.
Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyo wekewa walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.


22.
Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.


23.
Ili msihuzunike kwa kilicho kupoteeni, wala msijitape kwa alicho kupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna akajifakhirisha.


24.
Ambao wanafanya ubakhili, na wanaamrisha watu wafanye ubakhili. Na anaye geuka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.


25.
Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.


26.
Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu. Basi wapo miongoni mwao walio ongoka, na wengi katika wao ni wapotovu.


27.
Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Na tukajaalia katika nyoyo za walio mfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyo takiwa kuufuata. Basi wale walio amini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wapotovu.


28.
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na muaminini Mtume wake, atakupeni sehemu mbili katika rehema yake, na atakujaalieni muwe na nuru ya kwenda nayo. Na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.


29.
Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uweza wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu.
Haya tumekusoma ila wengine tunaamin kitabu kitakatifu nacho ni bible baaas
 
Kwahiyo Yesu amegawanyika sehemu ngapi? Katika kugawanyika huko je ana uwezo na mamlaka yaliyo kamili au ni tegemezi? Kama ni tegemezi je anamtegemea yupi zaidi ya yeye mwenyewe.

Yohana 17:3-4

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye
Yesu ni mwana wa Mungu. Mungu ana nafsi tatu Baba, Mwana na Roho mtakatifu wote ni umoja..
 
Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele YOHANA 3:16 Mwana wa MUNGU ni MUNGU
 
Acha upotoshaji
Yesu hakuhitaji kujitambulisha kuwa Yeye ni Mungu japo alifanya hivo. Ila Mungu mwenyewe alimutamtambulisha kuwa ni Mungu. Kabla ya kuanza huduma hapa duniani Mungu alianza kwa utambulisho juu ya nani anawahudumia;

Mathayo 3:17 Biblia inasema sauti toka juu mbinguni ilisikika kusema "Huyu ndiye mwanangu Mpendwa ninaependezwa nae, msikilizeni yeye".

Utambulisho huu haukutokea tu wakati baada ya kuzaliwa. Utambulisho wa kuwa Yesu ni Mungu atakayekuja duniani ulitabiriwa miaka takribani 600 kabla kutokea duniani kwa sura ya mwanadamu wa kawaida. Nabii isaya 7:14 anandika "Tazama bikira atachukua mimba naye atazaa mtoto wa kiume na ataitwa IMANUELI yaani MUNGU PAMOJA NASI".

Neno emnauel lilitafsiriwa kuwa maana yake ni Mungu ambaye yuko pamoja na sisi wanadamu. Na ndivyo ilivyotokea Bikira maria akamzaa mwana wa kiume kama ilivyotabiriwa. Utabiri huu ulirudiwa na Mathayo wakati wa kuzaliwa Yesu ( MATHAYO 1:23-25 ) Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”
Injili ya Yohana inarudi nyuma zaidi hata kabla ya Isaya. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo"(Yn. 1: 1-3)
. Kwa lugha rahisi ni kwamba hapo mwanzo kulikwako YESU, naye YESU alikuwako kwa MUNGU, naye YESU alikuwa MUNGU. na vyote vilivyoumbwa viliumbwa na yeye. Lakini pia Yesu ktk mambo mengi aliyosema na kutenda yalimtambulisha kuwa yeye ni Mungu. Mojawapo ni hii "Wakusanyikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo kati yao" Mwenye uwezo wa kuwepo mahali popote ni MUNGU peke yake.

MTOA MADA, NAKUSHAURI UMKUBALI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO
 
Pamoja.na mafundisho yoote, hata mimi akili yangu imekataa kukubali kuwa Yesu ni Mungu,imekataa hasa, naji force tu. Na kariibu ntafanya maamuzi.
 
Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele YOHANA 3:16 Mwana wa MUNGU ni MUNGU
yeah,mwana wa mungu ni mungu na mungu ndo mwanawa mungu kwa maana ya emanueli..

Ila kama huna roho mtakatifu huwezi kuelewa,mpaka roho mtakatifu akuingie kama alivyomwingia bikira maria
 
Acha upotoshaji
Yesu hakuhitaji kujitambulisha kuwa Yeye ni Mungu japo alifanya hivo. Ila Mungu mwenyewe alimutamtambulisha kuwa ni Mungu. Kabla ya kuanza huduma hapa duniani Mungu alianza kwa utambulisho juu ya nani anawahudumia;
Mathayo 3:17 Biblia inasema sauti toka juu mbinguni ilisikika kusema "Huyu ndiye mwanangu Mpendwa ninaependezwa nae, msikilizeni yeye".
Utambulisho huu haukutokea tu wakati baada ya kuzaliwa. Utambulisho wa kuwa Yesu ni Mungu atakayekuja duniani ulitabiriwa miaka takribani 600 kabla kutokea duniani kwa sura ya mwanadamu wa kawaida. Nabii isaya 7:14 anandika "Tazama bikira atachukua mimba naye atazaa mtoto wa kiume na ataitwa IMANUELI yaani MUNGU PAMOJA NASI". Neno emnauel lilitafsiriwa kuwa maana yake ni Mungu ambaye yuko pamoja na sisi wanadamu. Na ndivyo ilivyotokea Bikira maria akamzaa mwana wa kiume kama ilivyotabiriwa. Utabiri huu ulirudiwa na Mathayo wakati wa kuzaliwa Yesu ( MATHAYO 1:23-25 ) Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”
Injili ya Yohana inarudi nyuma zaidi hata kabla ya Isaya. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo"(Yn. 1: 1-3). Kwa lugha rahisi ni kwamba hapo mwanzo kulikwako YESU, naye YESU alikuwako kwa MUNGU, naye YESU alikuwa MUNGU. na vyote vilivyoumbwa viliumbwa na yeye. Lakini pia Yesu ktk mambo mengi aliyosema na kutenda yalimtambulisha kuwa yeye ni Mungu. Mojawapo ni hii "Wakusanyikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo kati yao" Mwenye uwezo wa kuwepo mahali popote ni MUNGU peke yake.
MTOA MADA, NAKUSHAURI UMKUBALI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO
mtoa mada ni mwanakondoo mwenzako,sema yeye alishajielewa siku nyingi,haoni shida kujadili vitu kama hivi
 
Acha upotoshaji
Yesu hakuhitaji kujitambulisha kuwa Yeye ni Mungu japo alifanya hivo. Ila Mungu mwenyewe alimutamtambulisha kuwa ni Mungu. Kabla ya kuanza huduma hapa duniani Mungu alianza kwa utambulisho juu ya nani anawahudumia;
Mathayo 3:17 Biblia inasema sauti toka juu mbinguni ilisikika kusema "Huyu ndiye mwanangu Mpendwa ninaependezwa nae, msikilizeni yeye".
Utambulisho huu haukutokea tu wakati baada ya kuzaliwa. Utambulisho wa kuwa Yesu ni Mungu atakayekuja duniani ulitabiriwa miaka takribani 600 kabla kutokea duniani kwa sura ya mwanadamu wa kawaida. Nabii isaya 7:14 anandika "Tazama bikira atachukua mimba naye atazaa mtoto wa kiume na ataitwa IMANUELI yaani MUNGU PAMOJA NASI". Neno emnauel lilitafsiriwa kuwa maana yake ni Mungu ambaye yuko pamoja na sisi wanadamu. Na ndivyo ilivyotokea Bikira maria akamzaa mwana wa kiume kama ilivyotabiriwa. Utabiri huu ulirudiwa na Mathayo wakati wa kuzaliwa Yesu ( MATHAYO 1:23-25 ) Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”
Injili ya Yohana inarudi nyuma zaidi hata kabla ya Isaya. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo"(Yn. 1: 1-3). Kwa lugha rahisi ni kwamba hapo mwanzo kulikwako YESU, naye YESU alikuwako kwa MUNGU, naye YESU alikuwa MUNGU. na vyote vilivyoumbwa viliumbwa na yeye. Lakini pia Yesu ktk mambo mengi aliyosema na kutenda yalimtambulisha kuwa yeye ni Mungu. Mojawapo ni hii "Wakusanyikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo kati yao" Mwenye uwezo wa kuwepo mahali popote ni MUNGU peke yake.
MTOA MADA, NAKUSHAURI UMKUBALI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO
hiyo aya ya isaya 7:14 haimuhusu yesu mkuu,ila kwasababu inasaidia kukufariji basi endelea kuamini hivyo for your peace of mind.
 
Nilichoeleza mimi ni kwamba Yesu sio Mungu. Na ndio maana nimetoa andiko la yohana 20:17 yesu akisema kuwa Mungu wake anayemuabudu yeye ndio Mungu wetu sisi sote. Sasa toa wewe ufafanuzi wa yohana 20:17

Hapo Yesu aliongea akiwa ktk hali ya ubinadamu kamili,..jee Mungu hawezi maajabu hayo?¿
 
Alikuja kwa walio wake lakini wakamkataa Bali wale waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa mungu.. Ndio wale waliaminilo jina lake..
 
Sasa kama ana uwezo wa kila kitu kwa nini atumie nguvu kujibadilisha binadamu ili watu wamwelewe kwa nini asitumie seconds tu kuwafanya binadamu wabadilike?
Mbona allah anatumia waislamu kufanya jihadi kuua makafiri.. Kwenye Quran anasema ataadhibu makafir kupitia mikono yenu.. Kwa nini asiadhibu yeye nwenyewe.? Kwa nini watu wajilipue kwa kufanya jihadi wakati alah anaweza kutumia seconds tu kutengeneza bomu.
 
Sisi Waislamu tunaamini kwamba Bwana Yesu a.s. alikuwa Nabii wa Mungu.

Na manabii wote ni watukufu na wapendwa wa Mwenyezi Mungu. Kuhusu ukoo wa Bwana Yesu Kristo Masihi Mwana wa Mariamu a.s. Qur'an Tukufu inaeleza kwamba:

A. Masihi bin Mariamu siye ila ni Mtume tu, bila shaka mitume wote wamekwisha fariki kabla yake, na mama yake ni mwanamke mkweli. (Qur'an 5:76).

B. (Ewe Mariam) baba yako hakuwa mtu m’baya wala mama yako hakuwa asherati. (Qur'an 19:29).


Kwa hiyo sawa na mafundisho ya dini ya Kiislamu tunamheshimu Nabii Isa a.s. (Yesu Kristo) na vile vile wazee wake.

Sisi tunashangaa sana wakati tunaposoma Biblia, tunaona Biblia inamfedhehesha Yesu Kristo vibaya sana.

Licha ya kuwa Mtume wa Mungu sawa na Biblia, Bwana Yesu haonekani hata mtu mwenye ukoo safi, bali tunalazimika kumtafautisha Isa a.s. na Yesu.

Biblia inasema kwamba:

1. Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi mwana wa Ibrahim. (Mathayo 1:1).

2. Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu. (Mathayo 1:5) Rahabu alikuwa kahaba (Yoshua 2:1).

3. Yuda alimzaa Peresi na Zera kwa Tamari (Mathayo 1:3). Tamari alikuwa kahaba na mzinifu. (Mwanzo
38:13-18).

4. Daudi alimzaa Sulemani kwa yule mke wa URIA (Mathayo 1:6). Beth Sheba mkewe URIA alipata mimba ya zinaa. (2 Samuel 11:2-5).


Hawa mabibi wote wa Yesu Kristo walikuwa makahaba na wazinifu. Lakini sisi hatukubaliani na Biblia bali tunaona kwamba ni taka taka zilizoongezwa katika Biblia.

Na kama Wakristo wanang’ang’ania usahihi wa Biblia, basi wajuwe kwamba Biblia inasema:

“Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana. (Kumb. la Torati 23:2).

Enyi ndugu Wakristo! Kama mnaona kwamba Biblia bado ni sahihi basi mjue kwamba Yesu ni kizazi cha
wazinifu, hawezi kuingia katika mkutano wa Mungu.

Kama hawezi hata kuingia katika mkutano wa Mungu, ninyi mnamtegemea nani?
Kama sisi ambavyo hatuikubali Quran tunaona takataka Na huyo mtume wenu tunamuona fake
 
View attachment 406746

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo."

Yohana 8:40

Katika andiko hilo YESU kwa kinywa chake yeye mwenyewe amejiita kuwa ni "MTU". Kama kuna mtu ana ushahidi wowote katika biblia YESU akijiita MUNGU, basi nami hapo nitaamini kuwa YESU Mungu.

Hata hivyo, mnaweza kusema pia, kuwa YESU alikuwa Mungu na Pia alikuwa mtu. Hata hivyo tukitazama sifa mbalimbali za mungu kama zilivyo tajwa au ainishwa na biblia, utaona hata kiduchu YESU hana sifa hizo.

Mathalani.

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza.."

Hesabu 23:19

Tumeona katika Yohana 8:40 Yesu akijiita Mtu, na hapa katika hesabu tunaambiwa Mungu si mtu, sasa wewe unayemuita Yesu Mungu umepata wapi?

NANI KAFUNDISHA YESU NI MUNGU?

"tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; "

Tito 2:13

Hayo maneno katika kitabu cha Tito, kimsingi ni barua ya kimisionari aliyo andika Paulo kwa watu wa Tito, kama tuonavyo katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Paulo anawaambia watu wa Tito kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maneno haya ya Paulo yanakwenda kinyume kabisa na maneno ga Yesu mwenyewe aliyo yasema katika Yohana 8:40 lakini kinyume kabisa na mafundisho ya kinabii kutoka katika kitabu cha Hesabu 23:19.

YESU ANASEMAJE KUHUSU PAULO?

Awali ya yote Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu na hakuwahi kumuona Yesu Kristo. Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni aliwahi kusema maneno haya.

"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi"

Yohana 16:1-3

Hapa Yesu anatabiri kuwa wanafunzi wake watakuja kuuliwa, anatabiri wakristo na wafuasi wa kanisa lake watakuja kuuliwa, na akasisitiza huyo atajaye wauwa wanafunzi wake hamjui yeye wala Baba(Mungu)

Nani huyo aliyeua wanafunzi wa Yesu? Jawabu ni Sauli ambaye ni Paulo.

"Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu."

Matendo 9:1-3

Kwa hivyo Mtu aliyetajwa na Yesu katika injili ya Yohana 16:1-3 kuwa atawaua wanafunzi wa Yesu si mwingine Paulo, na katika kitabu cha matendo tunaoneshwa ukatili wa Paulo kwa wanafunzi wa Yesu. Hata hivyo, Bwana Yesu anaendelea na utabiri wake juu ya Paulo katika aya hii.

"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo"

Yohana 8:44

Katika aya hiyo Bwana Yesu anasema huyo Paulo si kwamba ni muuaji tu, lakini pia mtu muongo sana. Na uongo mkubwa alio ufanya Paulo ni pale aliposema kakutana na Yesu na kisha akajifanya kipofu.

"Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda"

Matendo 9:3-7

Baaada ya Paulo kuwaua sana wanafunzi wa Yesu na kuwatesa sana ili waache mafunzo ya Yesu, lakini wanafunzi wa Yesu waligoma na walikataa katakata kuachana na mafunzo Yasu. Pia naomba mjue, mafunzo ya Yesu yalikuwa mwiba kwa serikali(Dola ya Rumi) na Paulo alikuwa anatumiwa na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa Yesu wanaachana na ukristo/uyaudi.

Pamoja na juhudi hizo za Paulo lakini alishindwa, hivyo njia aliyo amua kuitumia si nyingine bali ni kujiunga na wanafunzi wa kristo. Na ili aaminike ndipo hapo alipotengeneza stori ya kumuona Yesu na maagizo ya upofu, lakini kubwa zaidi alimnunua Anania ili msaidie kufanikisha lengo lake. Kwa kumtumia Anania na kwa kudanganya kwake kuwa kamuona Yesu, wanafunzi wa Yesu walimkubali.

Na hapo ndipo Paulo alipoanza kuyachakua mafunzo ya Yesu, na ndio maana ukristo wa sasa si ule alio ufundisha Yesu.

YESU NA MFARISAYO.

"Ewe FARISAYO KIPOFU, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote."

Mathayo 26:23

Paulo msomi mkubwa alikuwa Farisayo, lakini Yesu alisema nini juu mafarisayo? Kama tulivyo ona, Yesu anawaona mafarisayo kama vipofu, lakini kubwa katika andiko hili Yesu anamtabiri pia Paulo na maigizo yake ya upofu.

"Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu"

Matendo 23:6

Kwanza Paulo amekiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni farisayo. Lakini hiyo haitoshi Paulo alijitia upofu aso kuwa nao.

"Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi."

Matendo 9:8-9

Katika aya hizi tunaona kuwa Paulo amekiri kuwa Farisayo lakini pia tunaona Paul yuko katika maigizo ya upofu. Yote haya mawili yanakamilisha unabii wa Yesu pale aliposema

"Ewe farisayo kipofu.."

Mathayo 26:23

Katika aya hizo inatajwa sifa kuu au tabia kubwa ya Mafarisayo, na ambayo imethibiti(ilitimia) kwa Paulo. Sifa hiyo si nyingine bali UNAFIKI.

Paulo alikuwa mnafiki, yaani alijifanya muumini wa mafundisho Yesu ili mradi apate kuwapotosha wanafunzi wa Yesu, na hili kwakweli kafanikiwa sababu hakuna hata kanisa moja ambalo linafuata mafunzo ya asili ya Yesu. Kila kanisa lina kituko chake.

MWISHO.

Kwa kifupi huku nikizingatia maelezo yangu yote ya huko juu, kuwa YESU SI MUNGU, lakini hakumaanishi kuwa hakuna wanao muita au wanao amini Yesu Mungu. La kuzingatia kama tukiambiwa kauli ipi ya kushika kati ya YESU mwenyewe na ya Paulo kwa vyovyote vile tunatakiwa kushika kauli ya Yesu.

Kauli zote za Paulo ambazo hazipingani na za Yesu, kauli hizo tutazifuata, lakini kauli yoyote ya Paulo inayo pingana na Yesu, kauli ya Paulo itapuuzwa na kuanguka, alafu watu wote wanatakiwa wafuate kauli ya Yesu.

Hakuna kauli ya Yesu anayo alijiita Mungu, lakini zipo nyingi akijiita Mtu au mwana wa adamu. Na siku zote alijitafautisha na Mungu. Yesu anakata mzizi wa fitina katika andiko hili.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma"
Yohana 17:3

Nasema YESU SI MUNGU, na Paulo ana kesi ya kujibu kwa kudanganya ulimwengu, na kwa kuharibu mafundisho ya Yesu na kubwa zaidi kwa kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu na wafuasi wake.

Katika kuendeleza urongo wa Paulo, watu wameambukizwa urongo, sasa wanatusambazia picha na sanamu za wacheza sinema na kisha wanataka tuziheshimu kama Yesu, kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
.

NIPMEIPATA HII KWENYE RESEARCH ZANGU NAONA ITAKUSAIDIA NDUGU YANGU

Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!

Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom