Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
sasa kama alikuwa Mungu, Mungu gani anakamatwa na mwanadamu na kuuliwa msalabani? hivi ilikuwaje wanaadamu akamshinda Mungu nguvu na kumtia mkononi na kumuua? yani mwanadamu ndio amtese Mungu? huyu mwanaadamu gani anayeweza kumzidi nguvu Mwenyezi Mungu? nyie acheni utani bhana,

halafu wakati anateswa alisema Mungu wangu mbona umeniacha, sasa alikuwa anamuomba Mungu gani tena wakati yeye ndio Mungu..

hebu tumieni akili kidogo tu mtajua kuwa yesu sio Mungu. acheni kukaririshwa vitu visivyoingia akilini.

Mimi ni muislamu na katika mafundisho yetu Yesu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, sio mwana wa Mungu wala sio Mungu.
mi ni mkristo naamini Yesu ni mwana wa Mungu lakini siyo Mungu. kusema Yesu ni Mungu kunakanganya sana.
46bed908a68125631b811af0d0fd9174.jpg
 
Nilichoeleza mimi ni kwamba Yesu sio Mungu. Na ndio maana nimetoa andiko la yohana 20:17 yesu akisema kuwa Mungu wake anayemuabudu yeye ndio Mungu wetu sisi sote. Sasa toa wewe ufafanuzi wa yohana 20:17

Following are verses used to show that Jesus is God in flesh. The scriptures used here are from the New American Standard Bible.
  1. John 1:1, "In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God."
    1. John 1:14, "And the Word became flesh, and dwelt among us, and we beheld His glory, glory as of the only begotten from the Father, full of grace and truth."
  2. John 5:18, "For this cause therefore the Jews were seeking all the more to kill Him, because He not only was breaking the Sabbath, but also was calling God His own Father, making Himself equal with God."
  3. John 8:24, "I said therefore to you, that you shall die in your sins; for unless you believe that I am He, you shall die in your sins."
    1. Note: In the Greek, "He" is not there.
  4. John 8:58, "Jesus said to them, 'Truly, truly, I say to you, before Abraham was born, I am.'"
    1. Exodus 3:14, "And God said to Moses, 'I AM WHO I AM'; and He said, Thus you shall say to the sons of Israel, ‘I AM has sent me to you.’"
  5. John 10:30-33, "I and the Father are one." 31 The Jews took up stones again to stone Him. 32 Jesus answered them, "I showed you many good works from the Father; for which of them are you stoning Me?" 33 The Jews answered Him, "For a good work we do not stone You, but for blasphemy; and because You, being a man, make Yourself out to be God."
  6. John 20:28, "Thomas answered and said to Him, "My Lord and my God!"
  7. Col. 2:9, "For in Him all the fullness of Deity dwells in bodily form."
  8. Phil. 2:5-8, "Have this attitude in yourselves which was also in Christ Jesus, 6 who, although He existed in the form of God, did not regard equality with God a thing to be grasped, 7 but emptied Himself, taking the form of a bond-servant, and being made in the likeness of men. 8 And being found in appearance as a man, He humbled Himself by becoming obedient to the point of death, even death on a cross. 9 Therefore also God highly exalted Him, and bestowed on Him the name which is above every name, 10 that at the name of Jesus every knee should bow, of those who are in heaven, and on earth, and under the earth, 11 and that every tongue should confess that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father."
  9. Heb. 1:8, "But of the Son He says, "Thy throne, O God, is forever and ever, and the righteous scepter is the scepter of His kingdom."
    1. Quoted from Psalm 45:6, "Thy throne, O God, is forever and ever; a scepter of uprightness is the scepter of Thy kingdom."
 
Paulo anaweza kua sawa tu,kwa MUNGU yote yawezekana kama alivyoweza kumtengeneza popo.wengine wanamuita ndege na wengine humwita mnyama.yamkini YESU alikua BINADAMU na MUNGU pia
Pia unaposema kwa Mola yote yanawezekana inaonyesha una ufahamu wa kiasi au mdogo juu ya sifa na matendo take.Mathalani Mola hadhulumu,mola halali,Mola hasahau,Mola hakutwi na umauti.Sasa unaposema kila kitu kwake kinawezekana inabidi ubainishe na utupe mifano yakinifu.

Halafu Mola ameshajiwekea utaribu katika kuratibu mambo yake yaani utaratibu katu haubadiliki,mathalani leo mwadamu lazima ule,lazima ulale,lazima ufe na mfano wa hayo huu ni utaratibu ambao ameuweka na kamwe haubadiliki.
 
Yesu Kristo anajulikana katika Quran kama Neno la Mungu.roho ya Mungu kuna maana gani hapo.Mungu aliumba kila kitu kutumia neno.je neno ni nani
Unasema uongo wa wazi.Hivi Qur'an huwa mnaisoma mnasikia kwa watu ?

Muwe mnasoma na ubaya uliyoje kuzungumzia kitu ambacho hauna elimu nacho.Lazima tuchunge misingi ya elimu na misingi ya kuhakiki habari.

Nikikuuliza ni wapi katika Qur'an imeandikwa kwamba Yesu anafahamika kama neno la Mungu huwezi kuniambia na halipo hilo andiko.Kwahiyo umakini ni wa dharura katika kuchukua habari.
 
Nikitoa andiko kuwa MUNGU NI MTU unachakujib tena?acha kusumbua watu na uelewa wako mdogo!!!..SOMA HAPA..View attachment 407375
Halafu uniambie huyo mtu wa vita ni ndio Yesu.Pia kuna kitu kinaitwa karina katika somo la balagha sijui kama unalijua,katika somo muhimu la lugha.

Hapo imetumika balagha,katika kipengele kiitwacho "karina",katika elimu ya balagha.

Ufafanuzi juu ya hilo

Karina ni hali ya kutowezekana katika kitu au tamko lilotumika nadala ya tamko halisi.Nakupa mfano maarufu sana.Nikisema nimemuona simba anashuka kwenye mimbari kwa akili yako ya kawaida na iliyo salama hautafikiria ya kuwa simba mnyama lazima itakupa jibu ya kuwa huyo aidha ni mtu mwenye Simba au mwenye sifa yaani nguvu kama za simba.Hapa inakubalika balagha katika majazi sababu katika hali halisi simba kiuhalisia hawezi kuwa binadamu.

Tukirudi katika tamko lako "Bwana ni mtu wa vita",hiyo ni majazi na limetumika hapo sababu kamwe mtu hawezi kuwa Bwana kama andiko linavyosema.

Kwahiyo andiko hilo ni dhidi yako.Na karina hapo ndio imetoa ile hali wezekano na ndio hilo neno limetumika badala ya neno jingine.

Kama hujaelewa uliza.
 
Toa andiko la kutilia nguvu hoja yako.Sisi huita nakupa bidhaa na risiti yake.

Unapo sema yupo sahihi na mtu anaweza kuwa mtu na wakati huo huo anaweza kuwa binadamu.Lazima ujibu hoja kielimu kama alivyowasilisha mtoa mada.

Kwanza lazima ujue ni zipi sifa bainifu za Mola na ni zipi sifa anuai za mtu.Kisha linganisha kwa akili ya kawaida je ina yumkinika au nimuhali ?
Tatizo lenu mnakariri Mambo hamna hata hata ELIMU KIROHO,situkan QURAN YENU NDIO INASEMA HIVYO,soma,17:85,
1474958394717.jpg
1474958547439.jpg
 

Attachments

  • 1474958538514.jpg
    1474958538514.jpg
    31.3 KB · Views: 98
Nikitoa andiko kuwa MUNGU NI MTU unachakujib tena?acha kusumbua watu na uelewa wako mdogo!!!..SOMA HAPA..View attachment 407375
Halafu sema nachelea hapa tunazungumzia vitu ambavyo usahihi wake ndio unatupa sisi mustakabali wa maisha yetu baada ya kifo.

Ila ningeamua kujibu au kuijadili hoja yako kihuni huni,pia ningeijadili sema naheshimu hilo.Kwani kihuni pia inaelezeka.

Kwahiyo kama mtu ukiamua kusoma kweli basi soma kweli na ujifunze kweli kweli,tuache ujanja ujanja.
 
BORA HUYU KULIKO NINYI,MNA MAFUNDISHO YA **AJABU**/IMANI AMBAYO MNAYAFICHA KUPITIA LUGHA YA *KIARABU** YAAN HATA WATOTO WANAOSOMA**MADRASA**WANGEKUWA WANASOMESHWA *QURAN*KWA LUGHA ZAO ASINGEKUWEM HATA MMOJ,MFANO,View attachment 407536View attachment 407538View attachment 407539View attachment 407540View attachment 407541View attachment 407542View attachment 407543View attachment 407544View attachment 407545View attachment 407546
SASA KUNA KOSA GANI KATIKA HIZI AYA TUKUFU?wewe ni ABNORMAL yaani akili ndogo kupita maelezo
 
Tatizo lenu mnakariri Mambo hamna hata hata ELIMU KIROHO,situkan QURAN YENU NDIO INASEMA HIVYO,soma,17:85,View attachment 407574View attachment 407578
Sasa hapo wapi hapo inaonyesha kwamba mtu ni mungu mzee ?

Acha kuokota okota vitu.Hapo Mtume alikuwa anaulizwa na swahaba zake kuhusiana na mambo ya roho yaani roho ni nini na mfano wa hayo.Ndio akaambiwa na Allah ya kuwa elimu yake anaijua Allah peke yake na sisi hatukupewa elimu isipokuwa kwa uchache yaani elimu ndogo katika ile ilimu yote.

Kaka mimi nimesomeshwa na nimeuliza na sasa naifanyia kazi.Acha ujanja ujanja mzee.

Hata Leo hii ukiangalia suala la roho au kifo linawatatiza wengi isipokuwa wale ambao Allah amewarehemu.

Soma mzee tena usome kweli.
 
Tatizo lenu mnakariri Mambo hamna hata hata ELIMU KIROHO,situkan QURAN YENU NDIO INASEMA HIVYO,soma,17:85,View attachment 407574View attachment 407578
Unajua pia nashangaa mpaka nahisi kama kiswahili hukijui vizuri au unajitoa ufahamu au unayasoma haya maandishi kinyume nyume ? Jambo liko wazi tena jeupe sanaaa.

Au unaniletee mzaha kaka ? Kama unaleta mzaha niambie mzee ?
 
NI KWELI KABISA LAKIN SI KWA KIWANGO HIKIView attachment 407587
Nyinyi mtakuwa ndio wale huwa mnaambiwa ukitaka kumkamata muislamu mwambie katika Qur'an kuna kadha wa kadha uone kama atachomoka,halafu wanasahau kuwapa misingi ya kujibu hoja.

Kwa taarifa yako mzee mimi bado mchanga sana katika elimu ya dini yangu ya UISLAMU,ila namshukuru Allah nilipewa misingi ya kielimu.

Sasa kuna kituko kimoja nilikikuta kwenye blog "kimbilia.blogspot.com" kama sikosei kaweka makala yenye kichwa "Maswali yaliyofanya nitoke katika uislamu",angalia maswali yenyewe sasa ni porojo na mepesi ajabu,tatizo watu hawasomi.

Kwahiyo mzee nakuusia kama unataka unakishi hoja usiwe unachukua vitu nusu nusu kuna watu wamesoma mzee na waelewa vitu huwa hawaachi kitu.

Kama nimekukwaza kwa hali yoyote niwie radhi mzee.
 
View attachment 406746

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo."

Yohana 8:40

Katika andiko hilo YESU kwa kinywa chake yeye mwenyewe amejiita kuwa ni "MTU". Kama kuna mtu ana ushahidi wowote katika biblia YESU akijiita MUNGU, basi nami hapo nitaamini kuwa YESU Mungu.

Hata hivyo, mnaweza kusema pia, kuwa YESU alikuwa Mungu na Pia alikuwa mtu. Hata hivyo tukitazama sifa mbalimbali za mungu kama zilivyo tajwa au ainishwa na biblia, utaona hata kiduchu YESU hana sifa hizo.

Mathalani.

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza.."

Hesabu 23:19

Tumeona katika Yohana 8:40 Yesu akijiita Mtu, na hapa katika hesabu tunaambiwa Mungu si mtu, sasa wewe unayemuita Yesu Mungu umepata wapi?

NANI KAFUNDISHA YESU NI MUNGU?

"tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; "

Tito 2:13

Hayo maneno katika kitabu cha Tito, kimsingi ni barua ya kimisionari aliyo andika Paulo kwa watu wa Tito, kama tuonavyo katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Paulo anawaambia watu wa Tito kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maneno haya ya Paulo yanakwenda kinyume kabisa na maneno ga Yesu mwenyewe aliyo yasema katika Yohana 8:40 lakini kinyume kabisa na mafundisho ya kinabii kutoka katika kitabu cha Hesabu 23:19.

YESU ANASEMAJE KUHUSU PAULO?

Awali ya yote Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu na hakuwahi kumuona Yesu Kristo. Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni aliwahi kusema maneno haya.

"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi"

Yohana 16:1-3

Hapa Yesu anatabiri kuwa wanafunzi wake watakuja kuuliwa, anatabiri wakristo na wafuasi wa kanisa lake watakuja kuuliwa, na akasisitiza huyo atajaye wauwa wanafunzi wake hamjui yeye wala Baba(Mungu)

Nani huyo aliyeua wanafunzi wa Yesu? Jawabu ni Sauli ambaye ni Paulo.

"Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu."

Matendo 9:1-3

Kwa hivyo Mtu aliyetajwa na Yesu katika injili ya Yohana 16:1-3 kuwa atawaua wanafunzi wa Yesu si mwingine Paulo, na katika kitabu cha matendo tunaoneshwa ukatili wa Paulo kwa wanafunzi wa Yesu. Hata hivyo, Bwana Yesu anaendelea na utabiri wake juu ya Paulo katika aya hii.

"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo"

Yohana 8:44

Katika aya hiyo Bwana Yesu anasema huyo Paulo si kwamba ni muuaji tu, lakini pia mtu muongo sana. Na uongo mkubwa alio ufanya Paulo ni pale aliposema kakutana na Yesu na kisha akajifanya kipofu.

"Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda"

Matendo 9:3-7

Baaada ya Paulo kuwaua sana wanafunzi wa Yesu na kuwatesa sana ili waache mafunzo ya Yesu, lakini wanafunzi wa Yesu waligoma na walikataa katakata kuachana na mafunzo Yasu. Pia naomba mjue, mafunzo ya Yesu yalikuwa mwiba kwa serikali(Dola ya Rumi) na Paulo alikuwa anatumiwa na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa Yesu wanaachana na ukristo/uyaudi.

Pamoja na juhudi hizo za Paulo lakini alishindwa, hivyo njia aliyo amua kuitumia si nyingine bali ni kujiunga na wanafunzi wa kristo. Na ili aaminike ndipo hapo alipotengeneza stori ya kumuona Yesu na maagizo ya upofu, lakini kubwa zaidi alimnunua Anania ili msaidie kufanikisha lengo lake. Kwa kumtumia Anania na kwa kudanganya kwake kuwa kamuona Yesu, wanafunzi wa Yesu walimkubali.

Na hapo ndipo Paulo alipoanza kuyachakua mafunzo ya Yesu, na ndio maana ukristo wa sasa si ule alio ufundisha Yesu.

YESU NA MFARISAYO.

"Ewe FARISAYO KIPOFU, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote."

Mathayo 26:23

Paulo msomi mkubwa alikuwa Farisayo, lakini Yesu alisema nini juu mafarisayo? Kama tulivyo ona, Yesu anawaona mafarisayo kama vipofu, lakini kubwa katika andiko hili Yesu anamtabiri pia Paulo na maigizo yake ya upofu.

"Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu"

Matendo 23:6

Kwanza Paulo amekiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni farisayo. Lakini hiyo haitoshi Paulo alijitia upofu aso kuwa nao.

"Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi."

Matendo 9:8-9

Katika aya hizi tunaona kuwa Paulo amekiri kuwa Farisayo lakini pia tunaona Paul yuko katika maigizo ya upofu. Yote haya mawili yanakamilisha unabii wa Yesu pale aliposema

"Ewe farisayo kipofu.."

Mathayo 26:23

Katika aya hizo inatajwa sifa kuu au tabia kubwa ya Mafarisayo, na ambayo imethibiti(ilitimia) kwa Paulo. Sifa hiyo si nyingine bali UNAFIKI.

Paulo alikuwa mnafiki, yaani alijifanya muumini wa mafundisho Yesu ili mradi apate kuwapotosha wanafunzi wa Yesu, na hili kwakweli kafanikiwa sababu hakuna hata kanisa moja ambalo linafuata mafunzo ya asili ya Yesu. Kila kanisa lina kituko chake.

MWISHO.

Kwa kifupi huku nikizingatia maelezo yangu yote ya huko juu, kuwa YESU SI MUNGU, lakini hakumaanishi kuwa hakuna wanao muita au wanao amini Yesu Mungu. La kuzingatia kama tukiambiwa kauli ipi ya kushika kati ya YESU mwenyewe na ya Paulo kwa vyovyote vile tunatakiwa kushika kauli ya Yesu.

Kauli zote za Paulo ambazo hazipingani na za Yesu, kauli hizo tutazifuata, lakini kauli yoyote ya Paulo inayo pingana na Yesu, kauli ya Paulo itapuuzwa na kuanguka, alafu watu wote wanatakiwa wafuate kauli ya Yesu.

Hakuna kauli ya Yesu anayo alijiita Mungu, lakini zipo nyingi akijiita Mtu au mwana wa adamu. Na siku zote alijitafautisha na Mungu. Yesu anakata mzizi wa fitina katika andiko hili.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma"
Yohana 17:3

Nasema YESU SI MUNGU, na Paulo ana kesi ya kujibu kwa kudanganya ulimwengu, na kwa kuharibu mafundisho ya Yesu na kubwa zaidi kwa kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu na wafuasi wake.

Katika kuendeleza urongo wa Paulo, watu wameambukizwa urongo, sasa wanatusambazia picha na sanamu za wacheza sinema na kisha wanataka tuziheshimu kama Yesu, kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

TUJADILI!

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 Morogoro.

Bwana Dotto, naona umenukuu vifungu vingi kwa ajili ya kututhibutishia kuwa YESU si Mungu na Paulo ni mwongo.

Nilichogundua kwako ww ni msomaji mzuri wa biblia lakini naona unaitafasili kwa maono yako wewe Kama Dotto na si kwa kuongozwa na hekima ya Mungu. Kwa taarifa yako YESU hakuja kwa ajili ya wale waliokuwa wakimcha Mungu, Bali kwa wale waliokuwa wamepotea na kuzama katika uovu akiwamo Paulo na sisi wote ambao tulikuwa hutuijui kweli ya Mungu.

kwa habari ya Paulo inaonyesha ni jinsi gani neno la Mungu limetimia na Paulo aliyekuwa mpinga KRISTO sasa amekuwa ndio msemaji Mkuu wa YESU. Huo ndio mpango wa Mungu kuwa wale wote wenye dhambi wapate kutubu na kumwamin YESU kuwa ndio BWANA na mwokozi wao na wayasimulie matendo Makuu ya MUNGU.( mtu mzima hamwitaji daktari Bali wagonjwa)
 
Unasema uongo wa wazi.Hivi Qur'an huwa mnaisoma mnasikia kwa watu ?

Muwe mnasoma na ubaya uliyoje kuzungumzia kitu ambacho hauna elimu nacho.Lazima tuchunge misingi ya elimu na misingi ya kuhakiki habari.

Nikikuuliza ni wapi katika Qur'an imeandikwa kwamba Yesu anafahamika kama neno la Mungu huwezi kuniambia na halipo hilo andiko.Kwahiyo umakini ni wa dharura katika kuchukua habari.
Kumbe hata Quran hujui we mlaini sana ngoja tukufundishe,usipotosheka sema tuongezeee,YESU NI NENO(MUNGU),hata kweny quran
1474960144725.jpg
1474960155217.jpg
1474960171651.jpg
1474960187866.jpg
 
Nyinyi mtakuwa ndio wale huwa mnaambiwa ukitaka kumkamata muislamu mwambie katika Qur'an kuna kadha wa kadha uone kama atachomoka,halafu wanasahau kuwapa misingi ya kujibu hoja.

Kwa taarifa yako mzee mimi bado mchanga sana katika elimu ya dini yangu ya UISLAMU,ila namshukuru Allah nilipewa misingi ya kielimu.

Sasa kuna kituko kimoja nilikikuta kwenye blog "kimbilia.blogspot.com" kama sikosei kaweka makala yenye kichwa "Maswali yaliyofanya nitoke katika uislamu",angalia maswali yenyewe sasa ni porojo na mepesi ajabu,tatizo watu hawasomi.

Kwahiyo mzee nakuusia kama unataka unakishi hoja usiwe unachukua vitu nusu nusu kuna watu wamesoma mzee na waelewa vitu huwa hawaachi kitu.

Kama nimekukwaza kwa hali yoyote niwie radhi mzee.
Msamehe yaani inaonyesha hata mende IQ yake kubwa kuliko yeye
 
Nyinyi mtakuwa ndio wale huwa mnaambiwa ukitaka kumkamata muislamu mwambie katika Qur'an kuna kadha wa kadha uone kama atachomoka,halafu wanasahau kuwapa misingi ya kujibu hoja.

Kwa taarifa yako mzee mimi bado mchanga sana katika elimu ya dini yangu ya UISLAMU,ila namshukuru Allah nilipewa misingi ya kielimu.

Sasa kuna kituko kimoja nilikikuta kwenye blog "kimbilia.blogspot.com" kama sikosei kaweka makala yenye kichwa "Maswali yaliyofanya nitoke katika uislamu",angalia maswali yenyewe sasa ni porojo na mepesi ajabu,tatizo watu hawasomi.

Kwahiyo mzee nakuusia kama unataka unakishi hoja usiwe unachukua vitu nusu nusu kuna watu wamesoma mzee na waelewa vitu huwa hawaachi kitu.

Kama nimekukwaza kwa hali yoyote niwie radhi mzee.
Samahani sana sikujua kama wewe ni MCHANGA katika uislam,sorry kwa kukuover dose,NITAFUTIE SHEKHE,[emoji2] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Hapa sijui yesu alikuwa akimlilia mungu yupi amwokoe wakati yeye ndo mungu.

Hapa.

Na sijui ni Mungu yupi anayesemwa katika wingi??? wakati mnatuaminisha Mungu ni mmoja, agawanyiki wala kuzidishwa...sasa kwa nini kwenye hiki kitabu chenu anatumia wingi....Mungu mmoja nafsi tatu..baba, mwana na roho mtakatifu.....

And We have created you in pairs (male and female, tall and short, good and bad, etc.).(8)----An-Naba 78:8
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom