Dukeson mimi naomba niiandike hiyo paragraph yote hapa ili wavivu wa kufunua Biblia waisome,this is among my favourite bible verses maana huwa nikimaliza kuisoma nakauka mbavu!
"Wayahudi wakajibu,wakamwambia,je!sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria,tena una pepo?Yesu akajibu,Mimi sina pepo,lakini mimi namheshimu Baba yangu,na ninyi mwanivunjia heshima yangu.Wala mimi siutafuti utukufu wangu;yuko mwenye kutafuta na kuhukumu.Amin,amin nawaambia,mtu akilishika neno langu,hataona mauti milele.
Basi Wayahudi wakamwambia,Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahim amekufa, na manabii wamekufa;nawe wasema, Mtu akilishika neno langu hataonja mauti milele.
Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahim, ambaye amekufa?Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua.
Nikisema ya kwamba simjui,nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua,na neno lake nalishika. Ibrahim, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahim?
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, MIMI NIKO. Basi wakaokota mawe ili wamtupie;lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni."
Hiyo ni Yohana 8:48-59.
Nilipoona Yesu,akiwa kijana mdogo, anawaambia jamaa kuwa alikuwepo kabla ya baba yao IIbrahim aliyeishi na kufa miaka takriban 2000 kabla ya hapo, nilijua kinachofuatia ni wayahudi kuokota vitofari tu😀😀😀
Sasa hebu angalieni context ya hiyo paragraph hapo, ni ujumbe gani mnapata about Jesus?