Na pia kuna verse nyingi sana zinazopinga kuwa Yesu sio Mungu. Na tena anayepinga ni kauli za yesu mwenyewe. Kwahiyo biblia inajichanganya au? Embu mkuu toa ufafanuzi wa haya maandiko mawili kwanza tuone je yesu muongo nini?
Marko 12:28-29
Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
Yohana 20:17
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.