Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Je hapa alimuomba nani amnusuru na mauti kama yeye ndiye mwenye uwezo?

Mathayo 26:38-39

Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

Na kama kuna Mwingine alikuwa anamuomba kwanini hakumpa hitaji la moyo wake?

Je si ni kwamba kila kitu kilikuwa mikononi mwake, mbona alikataza vita na askari waliokuja kumkamata na muujiza wa uponyaji akafanya? halafu mbele anaomba kwa nani Mungu muujiza gani tena.
 
Na kama kuna Mwingine alikuwa anamuomba kwanini hakumpa hitaji la moyo wake????.
Kwani lowasa akiandamana wakati imepigwa marufuku,akija kukamatwa akaomba kikombe kimuepuka unadhani ndo hatakamatwa?,sheria huwa ni msumeno mkuu
Je si ni kwamba kila kitu kilikuwa mikononi mwake, mbona alikataza vita na askari waliokuja kumkamata na muujiza wa uponyaji akafanya??? halafu mbele anaomba kwa nani Mungu muujiza gani tena.
 
Na kama kuna Mwingine alikuwa anamuomba kwanini hakumpa hitaji la moyo wake????.

Je si ni kwamba kila kitu kilikuwa mikononi mwake, mbona alikataza vita na askari waliokuja kumkamata na muujiza wa uponyaji akafanya??? halafu mbele anaomba kwa nani Mungu muujiza gani tena.
Una uhakika kuwa hakukuwa na mwingine aliyekuwa ana muomba?
Waebrania 5:7

Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
 
Unautafakari uwezo na ukuu wa Mungu Kwa akili na uwezo wa kibinadamu. Yesu alipopaa mbinguni aliwaambia wanafunzi wake atawapelekea msaidizi ambae angewafunulia yote aliyowafundisha ina maana ukitaka kujua mafundisho ya Kristo Yesu nilazima huyo msaidizi ametumwa kwako la sivyo utaishia kuandika ujinga Kama huu ulioandika.MSAIDIZI ALIYEMSEMA YESU NI ROHO MTAKATIFU
 
Kwani wewe unamzungumzia yupi, huyu huyu aliyekuwa anabatizwa.
basi itakuwa yesu alikuwa unhinged,kwani huwezi ukawa unajiita wewe mwenyewe mtoto wangu wakati ni wewe mwenyewe,kuna kitu hakiko sawa ama labda alikuwa anatumia mvinyo kupita kiasi.
Unakumbuka ile siku alipokuwa na njaa kali akaufuata mti ili apate matunda na alipokosa matunda akaulaani mti kwa hasira?

Au siku alipowatuma wafuasi wake wakachukue punda wa mwanakijiji bila ruksa ya menye punda ili apande kuingia jerusalem kama mfalme?wakati hakuwa mfalme
 
Unautafakari uwezo na ukuu wa Mungu Kwa akili na uwezo wa kibinadamu. Yesu alipopaa mbinguni aliwaambia wanafunzi wake atawapelekea msaidizi ambae angewafunulia yote aliyowafundisha ina maana ukitaka kujua mafundisho ya Kristo Yesu nilazima huyo msaidizi ametumwa kwako la sivyo utaishia kuandika ujinga Kama huu ulioandika.MSAIDIZI ALIYEMSEMA YESU NI ROHO MTAKATIFU
Je wewe msaada wa roho mtakatifu unao ili unisaidie kunielewesha?
 
Una uhakika?
Waebrania 5:7

Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
Una uhakika alichoomba hapo alitendewa? Embu endelea 8.
 
Na kama kuna Mwingine alikuwa anamuomba kwanini hakumpa hitaji la moyo wake????.

Je si ni kwamba kila kitu kilikuwa mikononi mwake, mbona alikataza vita na askari waliokuja kumkamata na muujiza wa uponyaji akafanya??? halafu mbele anaomba kwa nani Mungu muujiza gani tena.
Si Kama nitakavyo Mimi Bali Kama utakavyo wewe kikombe ichi kiniepuke.mwelewe YESU katika ombi lake aliomba nn.
 
Yesu Kristo anajulikana katika Quran kama Neno la Mungu.roho ya Mungu kuna maana gani hapo.Mungu aliumba kila kitu kutumia neno.je neno ni nani
Wewe acha kupotosha Quran haiongelei kabisa habari ama historia Quaran ni Muongozo wenye kutoa namna ya kuishi na kuenenda na imani ya kiislamu
 
Unautafakari uwezo na ukuu wa Mungu Kwa akili na uwezo wa kibinadamu. Yesu alipopaa mbinguni aliwaambia wanafunzi wake atawapelekea msaidizi ambae angewafunulia yote aliyowafundisha ina maana ukitaka kujua mafundisho ya Kristo Yesu nilazima huyo msaidizi ametumwa kwako la sivyo utaishia kuandika ujinga Kama huu ulioandika.MSAIDIZI ALIYEMSEMA YESU NI ROHO MTAKATIFU
sawa mkuu,kumbe kabla ya yesu kuondoka huyo roho mtakatifu hakupata kukanyaga duniani,kuna roha mtakatifu version one na version two?
 
Wewe rudi kwanza ukajifunze maneno ya yesu. Yani yesu na huyo baba wawe sawa?

Yohana 14:28

Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
Unajua mkuu Biblia na maneno aliyoyasema Yesu ukienda kichwa kichwa utachanganyikiwa sana kwani kulisoma neno tu haitoshi inapaswa uchanganyanye na imani ndani yake na Mungu akujaalie jicho la kiroho kuyatam bua maandiko maana jinsi unavyojaribu kuyapangua maandiko kwa lugha ya kisheria utakwama na mwisho hatakuwa na mshindi bali wote mtaishia kuchanganyikiwa na Neno la Mungu litabaki kuwa imara na la kuaminiwa.

Yaani hoja ya kumpambanisha Yesu na Baba kuwa nani mkuu ili kudhibitisha uungu wa Yesu au kuubatilisha ni upagani na kufuru kubwa.
 
ha ha ha,mkuu umeanza kutumia hoja ya nguvu,je unakubali kuwa hawa ni wawili na si mmoja?
Ni wamoja mkuu. Hili ni fumbo la imani ndugu yangu na walio na imani ndio walifumbualo. Huwezi kutoka kwenye viloba na uasherati ukalifumbua.
 
Hili kweli hili zigo watu wamebebeshwa yaani Yesu ni Mungu !!! Daah jamani hivi hata gwajima ndivyo anavyoamini hivyo daah hawa jamii wamepotea
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom