Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Kwamjibu wa bible jehova pia ni mwana wa mungu,hapo ndo uone hawa waandishi walikuwa wanajiandikia tu,
shetani pia ni mwana wa mungu,ukisoma ayub kama sikosei katika kusanyiko la wana wa mungu shetani nae alikuwepo,mungu akamwuliza unatokea wapi bana?",
shetan akamjibu natoka matembezi huko duniani.
Mungu akamwuliza unamuonaje mtumishi wangu ayub?
Shetani akamjibu,"pale hamna kitu,vipi tumtest imani yake.......
Aliyekwambia shetani amejiumba ni nani wewe? shetani ni kiumbe cha Mungu je si mwana wa Mungu? Au unajiandikia tu wewe?
 
Umesema kuwa yesu alikuwa ana mcha Mungu, baba wa mbinguni. Nimekuuliza kati ya huyo baba na yesu nani mkuu. Toa jibu
Nikakujibu mkuu kuliko ni mwenye mamlaka, hujaelewa wapi?
 
Wana wa Mungu aliye hai,thread hii imejaa upotoshaji,ni vigumu sana kuleta maswali ya kwenye mijadala ya dini then wewe uwe unajibu kwa kuandika.

Mleta mada ananikumbusha miaka ya 90,"Yahaya mpe miki",kuna mambo ameandika ni ya kweli kwa mfano paul kuwa farisayo na kuwa alikuwa akilitesa kanisa lakini kwa kuwa kuna uongo katika maelezo yake ,logically ni uongo.Nina majibu ya maswali yake lakini ni kupoteza muda kwani tutaandika magazeti hapa.Ushauri wangu tujifunze kunyamaza.

Yesu ni Mungu,ukubali ukatae.Wengi mmekalia vitabu vya dini wenzenu tunapata updates Mungu anasema na kanisa kila wakati.Tumeona mengi,nyie huko mliko mnajua wenyewe na mungu wenu.

Angalizo kwa Christians.Hizi ni siku za mwisho,elimu za upotofu ni nyingi,ningeuacha ukristo miaka ya 90 ,lakini nilichogundua jamaa wanasoma maandiko nusu kisha wanaweka yaliyo yao.

Mteule songa mbele,Mungu akusaidie ujue haya niyasemayo ni hakika na kweli,shetani ana muda mchache sana sasa siku hizi wengi tunapoteza muda na hawa wasio amini,je roho mtakatifu anakushuhudia uwaelimishe?Tujifunze kumwomba Mungu atuongoze.Kuna watu wapo hapa kukurudisha nyuma,na kuunajisi moyo wako.

Kuwa makini hata na maneno unayowajibu je yanapendeza mbele za Mungu.Biblia ilisha sema "mambo ya imani kwake yeye asiye amini ni kama upumbavu".

Nenda kahubiri injiri mtaani na si kwa hawa wanaotaka kubishana,utapoteza nguvu zako bure na utaishia kuunajisi moyo wako.Shetani kwa kuwa amegundua wakristo wengi hawasomi neno,amekuwa akilitumia neno hilo hilo la kwenye biblia kuwapata kwa kulipotosha.Mara ya mwisho umesoma biblia yako lini?Ndugu safari ya mbinguni siyo rahisi kama ambavyo wengi wanadhani,kuikana nafsi si kitu kidogo.

Je biblia haijasema mazungumzo mabaya uhalibu tabia njema?Tuwe makini kuna mambo madogo madogo yatatukosesha mbingu kama hatutakuwa makini.

Je huwa unachelewa kazini?je unadanganya kuhusu muda unao ingia kazini?Unamkosea Mungu,tuziangalie njia zetu,hizi thread zingine ni upepo tu.
 
Aliyekwambia shetani amejiumba ni nani wewe??????shetani ni kiumbe cha Mungu je si mwana wa Mungu??? Au unajiandikia tu wewe?????
Shetani aliitwa mwana Mungu ila sio Mungu. Alkadharika hata yesu aliitwa mwana wa mungu naye sio Mungu.
 
Umesema kuwa yesu alikuwa ana mcha Mungu, baba wa mbinguni. Nimekuuliza kati ya huyo baba na yesu nani mkuu. Toa jibu
Hakuna mkuu wote ni wakuu jombaaa
 
LEARN TO USE THE POWER OF BEING SILENT
 
Shetani aliitwa mwana Mungu ila sio Mungu. Alkadharika hata yesu aliitwa mwana wa mungu naye sio Mungu.
Hivi ni ambavyo wewe unafikiri.

Ila Yesu ni Mungu.

Kuhusu shetani mueleweshe huyo sheikh mwenzio naona haelewi hata anaandika nini.
 
Nikakujibu mkuu kuliko ni mwenye mamlaka.hujaelewa wapi???
Jibu swali kama nilivyokuuliza usianze kona kona. Naona unaanza kupinda pinda. Haya twende unavyotaka wewe; kati ya yesu na huyo baba nani mwenye mamlaka?
 
Hivi ni ambavyo wewe unafikiri.

Ila Yesu ni Mungu.

Kuhusu shetani mueleweshe huyo sheikh mwenzio naona haelewi hata anaandika nini.
Basi wewe unayesema yesu ni mungu umelaanika.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

Yeremia 17:5
Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana
 
Hakuna mkuu wote ni wakuu jombaaa
Wewe rudi kwanza ukajifunze maneno ya yesu. Yani yesu na huyo baba wawe sawa?

Yohana 14:28

Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
 
Jibu swali kama nilivyokuuliza usianze kona kona. Naona unaanza kupinda pinda. Haya twende unavyotaka wewe; kati ya yesu na huyo baba nani mwenye mamlaka?
Mwenye mamlaka ni Mungu.
 
Mwenye mamlaka ni Mungu.
Sasa kama baba ambaye ndio Mungu ana mamlaka kuliko yesu kwanini ulisema yesu alijibadilisha na kutoka kwenye Mungu na kuwa binadamu ilihali bado alipokuwa duniani alikuwa tegemezi? Tumiaga na akili kufikiria. Sawa?
 
Basi wewe unayesema yesu ni mungu umelaanika.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

Yeremia 17:5
Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana

Nakubali kulaanika, kwa kauli yangu.

Unajaribu kueleza kile ambacho hujaelewa au unataka watu wafuate usichokielewa????

Ulitaka Yesu atumie kauli gani hapo wakati wa kuwaaga????
 
Aliyekwambia shetani amejiumba ni nani wewe??????shetani ni kiumbe cha Mungu je si mwana wa Mungu??? Au unajiandikia tu wewe?????

kwahiyo shetani na yesu ni mtu na kakake? Au labda yesu ndo babake na shetani? au yesu na shetani ni wamoja?,maana katika ufunuo tunasoma yesu akijiita nyota ya asubuhi ambayo maana yake ni Lucifer na kwa tafsiri lucifer ni shetani,
halafu katika isaya tunasoma kuwa nyota ya asubuhi ,yaani lucifer alitupwa duniani baada ya kutaka kujifananisha na Mungu, akatua duniani kama nyoka na kuwadanganya kina adamu,halafu baadae tunaona huyohuyo nyoka akiwambwa mtini na moses ili kika mwisrael akimtizama apone na asife,
wakati huohuo yesu anapigwa na wayahudi kwa kutaka kujifananisha na mungu naye pia anatundikwa mtini na wanasema ili uokoke lazima umtizame kwamaana ya umkubali yesu ndo utaokoka,
hii mfanano kati ya yesu na Lucifer,na yesu mwenyewe akijiita Lucifer tunapata conclusion kuwa huyu ni kitu kimoja,au?
 
Nakubali kulaanika, kwa kauli yangu.

Unajaribu kueleza kile ambacho hujaelewa au unataka watu wafuate usichokielewa????

Ulitaka Yesu atumie kauli gani hapo wakati wa kuwaaga????
Mimi kama sikuelewa kuhusu Mungu wake yesu ndio Mungu wetu sote basi wewe nieleweshe. Haya sema kuhusu yohana 20:17
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom