Kwa mujibu wa Biblia Takatifu!; wewe no kafir, mpinga Kristo, na MTU wa jehannam..habari ndio hiyo babu jinga...
UMEISHIWA , HUWEZI KUJIBU HOJA
Nakuelimisha zaidi
Paulo Na Ukristo
• Biblia yamdhihirisha Mungu anayeabudiwa na Wakristo
• Paulo alivyoibadilisha majina "miungu-Zeu" na "Herme" ya Wapagani na kuiita "Yesu"!
• Afundisha desturi na sifa zao kuwa ni moja
Uhusiano kati ya mungu wa Ukristo na miungu ya upagani
Sambamba na imani hiyo ya watu wa mataifa au wapagani, ya kuamini miungu-watu (akina Zeu na Herme) wanayoiamini kuwa na desturi ya kujigeuza kuwa mfano wa wanadamu maandiko ya Biblia tukufu yanafundisha pia kuwa, muasisi wa dini ya Kikristo, Bwana Paulo naye baadae aliihubiri miungu hiyo ya wapagani lakini kwa jina lingine. Uthibitisho wa hilo tunaupata kwenye mafundisho yake mwenyewe (Paulo) yafuatayo:
"Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibuni. Lakini nikikawia upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo Kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaamniwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu". (1 Timotheo 3:14-16)
"Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa Yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu, kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu." (Wafilipi 2:5-7)
Cha msingi anachofundisha Bwana Paulo hapo juu ni kwamba, hapo mwanzo Yesu (a.s.) alikuwa hana tofauti yoyote na Mungu, kwa maana kwamba alikuwa ni Mungu kamili! Baadae akaona kuna umuhimu pia awe mtumwa; kwa hiyo akaamua kuuvua Uungu wake na kuuvaa mwili akawa mwanadamu kamili japokuwa roho yake iliendelea kubaki kuwa Mungu!
Aidha, kwa lugha ya jumla anachotueleza Bwana Paulo hapo juu ni kwamba, kipindi fulani Yesu (s.a.) alikuwa Mungu kamili na kipindi kingine alijibadilisha akawa mwanadamu kamili japokuwa Uungu wake ukabaki nao rohoni! Kwa uchache, hivi ndivyo Bwana Paulo (muasisi wa Ukristo) afundishavyo kuhusu Mungu.
Hata hivyo, mafundisho hayo ya Bwana Paulo kwamba Yesu ni Mungu japokuwa ni mwanadamu kamili, yanapingwa vikali na mafundisho sahihi ya Bwana Yesu mwenyewe (a.s.) kama ifuatavyo:
"Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndio hii, sikia Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndio hii. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ile Yeye, na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia. Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo". (Marko 12:28-34)
"Yesu akamwambia. Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu". (Yohana 20:17)
Hapa Bwana Yesu (a.s.) anawafundisha wanadamu wafahamu kwamba Mungu wake na wao ni mmoja tu na daima hakuna mwingine.
Sambamba na ukweli wa mafundisho yake hayo, ni jambo lilowazi kabisa pia kwamba, hakuna mahali popote ndani ya maandiko matakatifu ambamo Bwana Yesu (a.s.) katika maisha yake yote alimowahi kukaririwa akidai Uungu japo kwa kutania. Kinyume chake tunaona mara nyingi alikaririwa akifundisha wazi wazi kuwa Yeye ni mtu (Tazama Yohana 8:40) na kusisitiza mara kwa mara kwamba yeye daima ni mwanadamu kamili (Tazama Mathayo 11:19)
Aidha, kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye (Yesu a.s.) ni mtu na ni mwanadamu kamili kama mwenyewe alivyofundisha hapo juu, tumeona jinsi Mungu (Yehovah au Allah s.w.t.) anavyokataa kata-kata kwamba Yeye kamwe si mtu na wala si mwanadamu kwa kila hali (rejea Hesabu 23:19)
Kwa shuhuda hizo basi ni wazi kuwa Mungu aliyekuwa akimhubiri Bwana Paulo hapo ni ile ile miungu ya wapagani (akina Zeu na Herme). Kwa kutumia jina la "Yesu", hasa kwa kuzingatia desturi aliyomsifia kuwa nayo mungu wake huyo ya kujigeuza kuwa mfano wa wanadamu i sawa na imani ile ya watu wa mataifa au wapagani katika miungu yao hiyo (Zeu na Herme).
Mafundisho kama hayo ya Bwana Paulo yamepelekea leo kuwababaisha wanadamu wamdhani Yesu kuwa ni Mungu wakati si kweli.
Sambamba na mafundisho yake hayo juu ya desturi hiyo ya miungu hiyo ya kipagani katika kutilia mkazo kwamba mungu wa dini yake ya Kikristo kwamba ana desturi ya kujibadilisha badilisha, Bwana Paulo alidiriki kudai kuwa mungu wake huyo aliyemwita "Yesu" pia wakati mwingine huwa anakuwa jabali! Uthibitisho wa dai lake hilo tunaupata katika kauli yake ifuatayo:
"Kwa maana ndugu zangu sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu, wote wakapita kati ya bahari, wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo". (1 Wakorintho 10:1-4)
Katika maelezo yake hayo juu, mwamba anaoukusudia hapo Bwana Paulo anaodai eti ulikuwa ni Kristo, yaani Yesu, ni lile jabali lililokuwa katika Horebu ambalo Nabii Musa (a.s.)kama Biblia ifundishavyo alilipiga kwa fimbo yake kisha maji yakatoka na watu wakapata kunywa (Tazama Kutoka 17:6).
Kwa maelezo yake hayo, yaonyesha dhahiri Bwana Paulo anakiri kwamba Bwana Yesu (a.s.) aliwahi kutandikwa bakora na Nabii Musa (a.s.)! Ingawa Nabii Musa (a.s.) haonekani kabisa katika zama zake akiwa pamoja na Nabii Yesu (a.s).
Kwa ujumla, mafundisho hayo ya Bwana Paulo yanalenga wazi katika kuonyesha sifa kubwa ya Mungu anayemhubiri kwamba ni pamoja na kujibadilisha-badilisha katika maumbile tofauti! Ambapo desturi hiyo (ya kujibadilisha-badilisha) haipatikani isipokuwa katika imani ya wapagani juu ya miungu yao, ndivyo waiaminivyo kuwa ina sifa hiyo (kama tulivyoona hapo awali).
Na ni katika mafundisho kama hayo ya Paulo ndipo unapopatikana dhahiri shahiri uhusiano halisi wa imani ya mungu-mtu kati ya dini yake ya Kikristo na dini ya kipagani.
Kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa asili ya Mungu anayeabudiwa na Wakristo inatokana na imani ya miungu-watu ya kipagani kama ile akina Zeu na Herme.