Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Msanii wa Bongo Flava, YJ Kiboko, ameibuka na kufunguka kuhusu taharuki inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ikimhusisha yeye na aliyekuwa mke au mpenzi wake, Chanuo.
YJ Kiboko ameeleza kuwa amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakimuuliza kuhusu maneno na matusi anayotolewa na Chanuo, jambo linalomuumiza sana kwani amekuwa akimheshimu na kumpenda kwa dhati.
Akiweka wazi chanzo cha mgogoro huo, YJ Kiboko amesimulia kuwa akiwa kwenye mizunguko yake aliliona gari alilompa Chanuo, na baada ya kumtuma kijana wake kuangalia, alimshuhudia mtu maarufu akishuka kwenye gari hilo.
Alipompigia simu Chanuo, alidanganya kuwa yuko nyumbani, lakini baada ya kufanya uchunguzi alibaini meseji za mapenzi kwenye mtandao wa Instagram zikionyesha kuwa mwanamume huyo alikuwa akiingizwa hata katika nyumba aliyomwangia.
YJ Kiboko ameeleza majuto yake kwa kudai kuwa alimsaidia Chanuo kuanzia chini mpaka akapendeza na kujulikana na watu, lakini badala ya shukrani ameishia kumvunja moyo, kumdhalilisha, na kumpotezea muda pamoja na gharama kubwa alizotumia.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa anao ushahidi wote kwenye simu yake na kwamba vitendo vya usaliti alivfanyiwa vinamfanya ahisi kama yuko kwenye ndoto.