Yondo Kusala Denise (Yondo Sister), JamiiForums tunakupa heshima zako na tunauthamini mchango wako, hatuna tuzo, ila tuna uzi wako

View attachment 2702740

Yondo Kusala Denise (amezaliwa tar. 1 Januari 1958) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Yondo Sister, ni msanii wa Kikongo. Wengi humwita "Malkia wa Soukous", "Tina Turner" wa muziki wa dansi barani Afrika. Yondo Sister amepata kuwa mwimbaji mkuu katika bendi ya Soukous Stars kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda kufanyakazi kama msanii wa kujitegemea. Uwezo wake wa kuimba iliibuliwa na Lutu Mabangu wakati huo Yondo akiwa kama mnenguaji wa Tabu Ley katika bendi yake ya Rocherettes. Yondo muziki uko katika damu, mzee wake alikuwa akipiga muziki kwa kujifurahisha tu, humo kukajengeka ujasiri wa kutoogopa hadhira. Na mara kadhaa alishiriki katika dansi, polepole na kuja kuwa mwanamuziki kamili na kutoa albamu ya kwanza mwaka 1991.

Yondo Sister amepata kutoa album 6 kwenye studio za Air B. Mas Production na Melodie, T.J.R. Music na zote zilikuwa moto mkali. Album hizo ni:-

FBI (2001)
Agenda (2002)
Dernière Minute(1995)
Deviation (1994)
Bazo (1991)
Planete (1990)
View attachment 2702741
Yondo Sister bado yuko hai nchini kwao Congo DRC akiendelea na shughuli za muziki.

Mungu amjalie umri mrefu wenye afya njema, furaha, amani ya moyo, ma mafanikio ya kila aina na ya kila rangi.

Mshana Jr , Pascal Mayalla, Elli
Sie Gen Z ngoja tusubiri uzi wa kwetu🙂🙂
 
Ilikuwa raha sana enzi hizo.
 
Aiseee hatari sana enzi zile. Nakumbuka those days back, ninasoma Mbeya, nimekata tiketi ya kwenda Mwanza, basi la Subira la kanisa Katoliki Mbeya.

Lami enzi hizo inaishia Isanga, haifiki hata Kawetere. Barabara vumbi balaa, yaanibukiiangalia barabara unaiona iko very smooth, ukiingiza mguu ni vumbi tupu, hadi pajani ndipo uikute sakafu ya barabara.

Basi kuanzia Mbeya hadi Tabora tulipigiwa kanda moja tu, YONDO SISTER album Deviation.

Hakika ni miongoni mwa siku zangu bora kabisa za kukumbukwa. Ilikuwa September mwaka 1994.
Kumbe mtoto! Enzi hizo masters tayari kitambo tupo katikati ya permanent head damage
 
Back
Top Bottom