Yondo Sister yupo hai? Naombeni historia yake

Yondo Sister yupo hai? Naombeni historia yake

Japo miaka hii watanzania tunajifanya "much know" lakini wacongo wametutesa sana, tena miaka mingi hususan 1980s na 90s, nyumba zote zilipambwa kwa Radio Cassete. Dah! kweli utu uzima umeshaingia lol!
 
Congo ilipaswa kuwa ndio the powerful Country in Africa kwa kila kitu!!
Wakongo amkeni sasa acheni kukata mauno tu!!
 
Hapana, sijawekeza. Unajua miaka ile ya 1996 kurudi nyuma kiukweli muziki wa dansi Tanzania( vijana jazz, ddc mlimani park, bimalee, washirika, ottu/juwata-msondo, maquis, na bendi nyingine) zilikuwa peak sana kimuzingi, na kwa kweli wakongo nao wakikuwa ni moto wa kuotea mbali kimuziki, Bongo flavor haikuwepo, kwa hiyo mpango mzima ilikuwa ni muzik wa dansi toka Tanzania au Zaire( Congo DR ya sasa).

kaka chaza we mkali unaweza kunipa historia kamil mkuu?
 
yuko nchi gan uyu mwanamama mauno wa enzi hzo!...afu madame umeadimika kule kwe2 ukubwani!

Mie mbona nipo.
Siku hizi napatikana kidogo maana nimejiweka MMU, manake kuna watu wanatudis wanawake.
 
Yondo Sister hajafa.
Bado yuko hai na mtoto wake yule mmoja na pekee wa kike tunakaa nae huku Kinondoni Manyanya.
Jumapili iliyopita alikuja kumtembelea mwanae, ila amezeeka zeeka.

mtoto wake nitamtambuaje nikiangalia zile nyimbo zake? anaitwa nani? na anaishi na nani hapo? kashaolewa au bado? operesheni kimbunga haijamkumba?
Nalog off
 
Namkubali huyo jamaa, hata katika wimbo Wapi Yo ameufanyia heshima ya aina yake lakini Diblo Dibala ni mchawi halisi wa Guitar. Ukisikiliza/ukiangali kibao cha Matchatcha Laisser Paisser

Mkuu Dally Kimoko anatisha ,sikiliza Bilalala-Pepe Kalle, Kin Night au Nairobi Night.
 
yupo hai mkuu. zamani ndio walivumisha amekufa si unajua wabongo

kweli mkuu hata mimi nakumbuka.ni enzi zetu zileee za kudanganyana.thanks to whoever invented google....ila mimi napenda kujua alipo mwanamziki GATO.ilivumishwa miaka ile eti alikutwa na madawa ya kulevya na akafungwa.nam google ila info zake ni kama hazipo.
 
Back
Top Bottom