Yondo Sister yupo hai? Naombeni historia yake

mkuu sio ubinafsi wa Jb mpiana, bali ilikuwa ni makubaliano kuwa kila mwanamuziki wa wenge bcbg atoe solo albam. ndipo jb akaanza kutoa project yake ya albam ya fex de lamour wimbo uliompa tuzo nyingi. albam hii maarufu kama ndombolo ya solo ikauza sana kuliko hata albam za wenge bcbg walizozitoa kama kundi, kwa kuwa alishirikisha baadhi ya wana wenge, wakataka waifanye albam ya kundi na wagawane mapato, jb akakataa, ndipo zilipoanza futina na zikiongozwa na werason ngiama makanda wa meison mere, akazushiwa jb ni mshirikia alienda hadi kwa mganga akanyweshwa damu ya mtu ili apendwe zaidi. na hii iliwauma baadhi ya wana bcbg hasa wale waliokuwa ndio waasisi wa bendi waliomkaribisha jb kisha kuja kuwa kinara zaidi yao. mwisho watu wakagawana mbao,meli ikazama, wengi ikamegika vipande, marie paul akaanzisha bendi ya wenge el paris, werason akaanzisha wenge meison mere,baadaye adolf domingize akaanzisha wenge tonyatonya,blaize bula nae akatoka kivyake.
ila kiukweli bendi zilizitakana na wenge bcbg ziliziweza kusimama mpaka sasa ni ya wenge ya werason na jb mpiana.
sasa kati ya wera na jb, wera son akabaki kuwa sio mtunzi mzuri wala muimbaji mzuri bali ni muandaaji wa show nzuri,kwa masebene tu na uchezaji wako vizuri kuliko wenge ya jp mpiana. kwa upande wa wenge ya jb, jb mpiana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mtunzi na mwimbaji bora na imethihirika wazi kuwa yeye ndiye aliyekuwa anaibeba wenge bcbg 4x4 by far kabla haijavunjika kiumbaji na kimpangilio wa muziki.jamaa ni mpangiliaji mzuri saana wa muziki na mwinbaji mzuri. tafuta show ya jb live at kinkole ndio utajua jb ni nani

Ni kweli nakumbuka alimshirikisha hadi Papa Wemba nadhani kwenye wimbo uitwao Cavelier Soliter( spelling sikumbuki vizuri) kwenye hiyo hiyo album( moto wa mapebzi- feu'x de lam our) iliyompa umaarufu mkubwa JB Mpiana hadi kundi kuvunjika.
 
yamekuwa hayo tena?????? usinisemelee maana nasikia kapitia jkt asije kuniharibu shepu bureeeeeee!.

na kama shepu yako ndo kama iyo apo kwenye avatar ufikiria mara mbili.....lol...we unanchokoza unategemea nini?
 
Ni kweli nakumbuka alimshirikisha hadi Papa Wemba nadhani kwenye wimbo uitwao Cavelier Soliter( spelling sikumbuki vizuri) kwenye hiyo hiyo album( moto wa mapebzi- feu'x de lam our) iliyompa umaarufu mkubwa JB Mpiana hadi kundi kuvunjika.

caliver soliter wacha kabisa,solo iliyopigwa kwenye huo wimbo ni balaaa, i like the song,imenikumbusha kanda niliyonunua mwaka 1997 ilikuwa ni mixtape ya bolingo iliitwa ndombolo ya solo vol 4 ,ilikuwa na hicho kibao cha calivar soliter,masuwa,na nyimbi za extra.musika,papa wemba,general defao etc. looooong time, muziki wa congo wa sasa hamna kiti, ni drums tu na atalaku baasi. tofauti ya muziki wa sokous wa zamani na sasa mi kuwa solo gitar ndiyo ilikuwa inaongoza muziki akimfuatia mpiga drums kisha atalaku/rapa au mwimbaji kwa sasa ni tofauti, mapigo na mabadiliko katika muziki yanaongozwa na rapa/ atalaku anataka kuimba nini au anaimba nini kisha vyombo vinamfuatia,matokeo yake muziki unakosa ladha na mipigo isiyopangilika, mfano mzuri ni muziki anaoimba kofi olomide umepelekea kukosa mwelekeo kabisa, ukimsikiliza kofi olomide,wa zamani ana ladha kuliko kofi wa sasa.
kelele zimezidi mno kwenye miziki ya sasa, wenyewe wanaita sebene,ila manjonjo yalizidi sanaaa huaribu ladha. ila jb mpiana aliliona hili kitambo na anajitahidi kimantaine real bolingo
 
Yaa, jamaa kachapa gitaa hatari. Diblo Diballa ni mkali tena sana. Ila kwa gitaa lenye ladha, Dally Kimoko ni hatari. Ladha yote tamu ya wimbo uitwao Madi-Yondo, Album nzima ya Soukouss Stars ile ladha ni yake. Si kwamba anakuwa peke yake, kwa mfano utakuta yupo na Lokassa Yambongo, tena na huyo Diblo wakati fulani walicharaza mpini.

Mzee hawa watu unawajua au una bahatisha !?........kuna Album inaitwa 'Soukous Stars in the Hollywood' mpini wa Solo Gitaa ulipigwa na Saladinn !
walikuwemo 'Majani. ya Fedha na Nguma Lokito. Yondo Sister na Mzee Shimita.
Dally Kimoko anakaa kitako kwa Diblo Dibala.
 
kweli mkuu umenikumbusha kwenye albam ya sokous star morenita solo imepigwa na saladin na sio dally kimoko
 
Dally Kimoko alikuwapo pia. Angalia vizuri wimbo SOPHIA utamwona pamoja na Saladin, Lokasa YaMbongo na Ngouma Lokito.
 
.......naona ndugu una 'mahaba' na Dally Kimoko, kwani nijuavyo mimi Album nzima ametembea Saladin na Solo ya umeme !
 
mkuu sio ubinafsi wa Jb mpiana, bali ilikuwa ni makubaliano kuwa kila mwanamuziki wa wenge bcbg atoe solo albam. ndipo jb akaanza kutoa project yake ya albam ya fex de lamour wimbo uliompa tuzo nyingi. albam hii maarufu kama ndombolo ya solo ikauza sana kuliko hata albam za wenge bcbg walizozitoa kama kundi, kwa kuwa alishirikisha baadhi ya wana wenge, wakataka waifanye albam ya kundi na wagawane mapato, jb akakataa, ndipo zilipoanza futina na zikiongozwa na werason ngiama makanda wa meison mere, akazushiwa jb ni mshirikia alienda hadi kwa mganga akanyweshwa damu ya mtu ili apendwe zaidi. na hii iliwauma baadhi ya wana bcbg hasa wale waliokuwa ndio waasisi wa bendi waliomkaribisha jb kisha kuja kuwa kinara zaidi yao. mwisho watu wakagawana mbao,meli ikazama, wengi ikamegika vipande, marie paul akaanzisha bendi ya wenge el paris, werason akaanzisha wenge meison mere,baadaye adolf domingize akaanzisha wenge tonyatonya,blaize bula nae akatoka kivyake.
ila kiukweli bendi zilizitakana na wenge bcbg ziliziweza kusimama mpaka sasa ni ya wenge ya werason na jb mpiana.
sasa kati ya wera na jb, wera son akabaki kuwa sio mtunzi mzuri wala muimbaji mzuri bali ni muandaaji wa show nzuri,kwa masebene tu na uchezaji wako vizuri kuliko wenge ya jp mpiana. kwa upande wa wenge ya jb, jb mpiana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mtunzi na mwimbaji bora na imethihirika wazi kuwa yeye ndiye aliyekuwa anaibeba wenge bcbg 4x4 by far kabla haijavunjika kiumbaji na kimpangilio wa muziki.jamaa ni mpangiliaji mzuri saana wa muziki na mwinbaji mzuri. tafuta show ya jb live at kinkole ndio utajua jb ni nani

Hivi kundi lile la G7 ambalo lilikuja kwa kasi ya ajabu likawatisha hadi Extra Musica( siyo ile iliyojitenga Extra Musica International) liliishia wapi? Kama una habari zozote kaka niarifu/ pm. Nasikia Emelia na Alain Mpella wameshakimbia Wenge. Emelia alimfuata Adolph Dominguez.
 
.......naona ndugu una 'mahaba' na Dally Kimoko, kwani nijuavyo mimi Album nzima ametembea Saladin na Solo ya umeme !
Na huo ndio ukweli. Hakuna mahali Dally Kimoko kapiga gitaa kwenye album hiyo ya Morenita. Hapo wapo Lokassa, Saladdin Fellela na Ngouma Lokito. Waimbaji ni Ballou Kanta (Aba Guimo na Morenita), Yondo (Cayina), Lucien Bokilo (Robin Pretty), Shimita (Rhoda)
na nyingine ambazo wameimba na pamoja. Hili kundi likuwa balaa. Nina album zao 4 kwenye library yangu.
 
Kiukweli Dally Kimoko ni mkali dhidi ya Diblo Dibala
Sio kweli ndg! Ukitaka kujua utundu wa Diblo, sikiliza wimbo wa 'Pon mon bouge' wa Pepe Kalle kapiga yeye. Kama huamini sikiliza album nzima ya Extra Ball ya Kundi zima la Loketo, au ya kwake mwenyewe Diblo inayoitwa 'Laissez Passer'. Ninayo album nzima hiyo, nita upload nikiwa na muda. Dally Kimoko hawezi hata kumzidi Nene Tchakou (kapiga solo kwenye Inde Monie ya Bongoman). Kimoko ni maarufu, ila sio mtundu wa kuchezea nyuzi (free style guitarist)
 
respect. Nene Tchakou nae ni hatari. nalisikia alishakufa ila sina uhakika. huyu jamaaa ukitaka kuupata utamu wa solo yake tafuta albam zote za Alain Kounkou mzee wa sakayonsa nyimbo kama masapa lyida utamtamtambua nene tchakou ni nani,albam kama 360 volts ilikuwa tishio kwenye ulimwengu wa sokous!
 
Swadakta. Umetisha ndg. Nina baadhi ya nyimbo za Kounkou, nazipenda sana, sikujua kama gitaa kapiga Tchakou. Nakushauri u download album ya Tchakou mtandaoni inayoitwa 'Soto', kamshirikisha Mabele, kachezea gitaa ile mbaya. Zicheki ktk youtube. Hawa akina Olomide, Ipupa na Wazekwa wanaongea sana, hatupati hata nafasi ya kusikia vyombo vya muziki, zaidi ya kelele zao.
 
sasa ni kelele tu. na kofi ndio aliyeanza kuharibu muziki wa congo
 
Mzee hawa watu unawajua au una bahatisha !?........kuna Album inaitwa 'Soukous Stars in the Hollywood' mpini wa Solo Gitaa ulipigwa na Saladinn !
walikuwemo 'Majani. ya Fedha na Nguma Lokito. Yondo Sister na Mzee Shimita.
Dally Kimoko anakaa kitako kwa Diblo Dibala.
Assantii, tunaendelea, ni zamu ya mheshimiwa CHAZA sasa, Mheshimwa Idimi ajiandae
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom