mkuu sio ubinafsi wa Jb mpiana, bali ilikuwa ni makubaliano kuwa kila mwanamuziki wa wenge bcbg atoe solo albam. ndipo jb akaanza kutoa project yake ya albam ya fex de lamour wimbo uliompa tuzo nyingi. albam hii maarufu kama ndombolo ya solo ikauza sana kuliko hata albam za wenge bcbg walizozitoa kama kundi, kwa kuwa alishirikisha baadhi ya wana wenge, wakataka waifanye albam ya kundi na wagawane mapato, jb akakataa, ndipo zilipoanza futina na zikiongozwa na werason ngiama makanda wa meison mere, akazushiwa jb ni mshirikia alienda hadi kwa mganga akanyweshwa damu ya mtu ili apendwe zaidi. na hii iliwauma baadhi ya wana bcbg hasa wale waliokuwa ndio waasisi wa bendi waliomkaribisha jb kisha kuja kuwa kinara zaidi yao. mwisho watu wakagawana mbao,meli ikazama, wengi ikamegika vipande, marie paul akaanzisha bendi ya wenge el paris, werason akaanzisha wenge meison mere,baadaye adolf domingize akaanzisha wenge tonyatonya,blaize bula nae akatoka kivyake.
ila kiukweli bendi zilizitakana na wenge bcbg ziliziweza kusimama mpaka sasa ni ya wenge ya werason na jb mpiana.
sasa kati ya wera na jb, wera son akabaki kuwa sio mtunzi mzuri wala muimbaji mzuri bali ni muandaaji wa show nzuri,kwa masebene tu na uchezaji wako vizuri kuliko wenge ya jp mpiana. kwa upande wa wenge ya jb, jb mpiana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mtunzi na mwimbaji bora na imethihirika wazi kuwa yeye ndiye aliyekuwa anaibeba wenge bcbg 4x4 by far kabla haijavunjika kiumbaji na kimpangilio wa muziki.jamaa ni mpangiliaji mzuri saana wa muziki na mwinbaji mzuri. tafuta show ya jb live at kinkole ndio utajua jb ni nani
Ni kweli nakumbuka alimshirikisha hadi Papa Wemba nadhani kwenye wimbo uitwao Cavelier Soliter( spelling sikumbuki vizuri) kwenye hiyo hiyo album( moto wa mapebzi- feu'x de lam our) iliyompa umaarufu mkubwa JB Mpiana hadi kundi kuvunjika.