You must be kidding me! - 21.9Millions USD?

Heri masikini fukara kuliko tajiri mtumwa. Hatuwezi ishi kwa kutgemea misaada milele. we must change!!!
 

Maneno matupu hayatabadilisha jinsi tulivyo....
 
Wajameni tusiushupalie sana huu msaada wa tujisenti twa Hu Jin Tao. Hutu ni tujisenti twa 'mgeni njoo mwenyeji apone'. JK na sisi Watanzania hatuna budi kushukuru kwa hicho kidogo maana tuko hoi bin taaban.

Hiyo ni ile hela ya pipi aliyepewa dogo alikuwa anamsindikiza dada yake ili aende dukani kununua pipi na akisharudi shughuli imekwisha isha. Serikali ndio dogo, Tanzania ndio dada na China ndio mtoa hela ya pipi.

China ni kitu ingine, wakati huu wa kuyumba kwa uchumi wa dunia ndio mchina anautumia kujiimarisha.
Pamoja na misaada lukuki toka China, Mchina anahakikisha anaimarisha soko lake huku akihakikisha no technology transfer ili wewe ubaki soko milele. Ni nchi iliogoma kusaini tamko la haki za binaadamu na mikataba yoyote ya anti piracy na nawahakikishia very soon Tanzania itakuwa koloni la wachina kiuchumi,
 
Niliona picha ya Mkapa kwenye ufunguzi wa uwanja. Hivi hakuona aibu kwenda kuomba kujengewa uwanja kwa $ 50m wakati kipindi hicho hicho ndio yeye na genge lake walichota $133m za EPA. AIBU!

Mwanakijiji kumbuka pia tumeweza kujenga minara pacha ya BoT kwa $450m. Ni viwanja vingapi hivyo?

Masanja nimekukubali; kwamba kinachotakiwa ni wananchi kuamka na kuwajibisha watawala regardless chama kitakachokuwa madarakani.
 
CCM wapi ndugu?????

Kenya na Malawi opposition now wameshika serikali karibu 10 years -ruswa tu mtindo mmoja!


Unasemea hao wapinzani ambao wote wamemeguka kutoka chama kilichokua tawala kwa karne milioni? Hiyo ni opposition au ni kama kuchukua hela na mkono wa kulia halafu unazihamishia kushoto?
 


Ndugu yangu katika post zooote...hii ya leo ndio imenifurahisha sana..well done bro!! hatuwezi tukaendekeza huu uomba omba bila bila sababu zozote za msingi..utakuja kutuletea shida mbele..tutalemaa!! this is enough..na sasa inabidi tuanzishe kampeni ya kuikataa hii misaada..maana naona inatuzidishia uvivu, shida, matatizo, na chuki badala ya maendeleo....
 
Labda M.M anisaidie kama nimempata, mimi nimemuelewa tofauti kidogo.....Nimeona kama anawakilisha ujumbe wake kwa njia tofauti kama aliyotumia bwana Mpoto kwenye mashairi yake ya ....'safari kwa mjomba'.
 
M Mwanakijiji, kumbuka chururu si ndo ndo ndo!
 

Tena kama nilisikia vyema walisema alikuja na ujumbe wa watu 140? ambacho sielewi akija na watu wote hao garama ya kuwa tunza ni kwa mwenyeji? ama wanajilipia?
 
Tulisahau tu kumwomba ile sheria yao inayoshughulikia wala rushwa wakubwa kama wanasiasa, watendaji wakuu wa serikali na taasisi za UMMA.
 
huo msaada,is totaly an insult,we dont need it,washitakiwa wa epa,wana mapesa mengi waliyotuibia,tukiyachukua hayo tunaweza kufanya mambo mengi sana,
hawa wachina wamejaa kila sehemu,wakifanya shughuli za umachinga ambazo hata sisi tunaweza kuzifanya,wanatuibia kinoma,nenda urafiki textile,kila spea mipaka mifagio inatoka china
 

Penye uzia penyeza rupia kakak... huyu anapenyeza in advance tuu hapa
 
Chinese are no fools, its like luring us with something small so they can get something big in return!! Chinese are everywhere in Tanzania right now with their fake products, others are selling sandals at Kariakoo!! Charity begins at home, he could have used that 22M-USD to clear the pollution they are making with their fake products
 
Mimi binafsi initially nilifikiri ni 21.9bil USD? .....OK huu ni msaada kama misaada mingine? Ambacho hakiniingii akilia, msaada wa magnitude hii kuandamana or kusindikizwa na HU Jintao? rais wa taifa linalodhaniwa kuwa na uchumi mkubwa dunia?.....No sikubaliani naye kabisa.....hizo agreements angeweza kuzisaini balozi wake tu! Labda kama the main agenda ya visit yake ilikuwa tofauti kabisa na na hili la kutoa misaada!

Ok wengine wametaja eti, kiasi hiki ni kikubwa kusainiwa hasa ukizingatia dunia imekumbwa na CREDIT CRUNCH! Mbona babu Bush alimanage kusaini a record msaada was USD698 wakati alikuwa in the midst of Credit Crunch tena iliyoikumba nchi yake in particular?

Naungana namchangiaji mmoja aliyesema, ni bora tungefanya jitihada za recover hela zetu za EPA, Radar, Richmond etc zingetusaidia zaidi kuliko hizo zinazokuja na masheriti kibao....e.g mara utasikia, watalaam wa kilimo, mawasiliano etc watatoka china, na hapa tuwalipe kama experts kutoka kny that 21.9, bado utaambiwa agricultural inputs tununue China tena at inlfated prices....so at the end utaona masaada wote unarudi China. Sasa si bora tuhangaike kurecover hela zilizochotwa na mafisadi hapahapa, ambazo matumizai yake hayana masharti wandugu?
 
Sisi tunapenda kuomba lakini sisi hatupendi kuombwa, Ombaomba ktk jiji la Dar wote tunawatimua kila siku kwa sababu tukipita ktk mataa na mashangingi yetu wanatuomba.

lakini sisi kila siku njia na mguu kuomba, nawao wanajisikia hivyo hivyo kama wewe unavyojisikia ukikutana na ombaomba mtaani. Wangeweza na wao kukutimua lakini wao wamebuni njia mbadala ya kuzirudisha pesa zao kiaina na faida juu.

Watanzania jamani kuomba ni hasara kubwa tuache nawasihi tabia hiyo haifai
 
...Mbona babu Bush alimanage kusaini a record msaada was USD698 wakati alikuwa in the midst of Credit Crunch tena iliyoikumba nchi yake in particular?

...Mungu wangu, kumbe unaamini "msaada" ule wa Joji Kichalka ulikuwa bure bure tu? ...hujasikia kuhusu kusimamishwa ujenzi kwa wakazi wa Kigamboni? hujawahi sikia jinamizi linaloitwa OFCOM?

...Heri ya Nyerere aliyekuwa anaona mbali na kukumbatia misaada ya Wachina kujenga URAFIKI textiles mills etc etc kuliko hii misaada ("kwenye mabano") ambayo tunapokea toka kwa watu wenye ajenda za kivita zaidi mfano IRAN, na MAREKANI...

Kabla hatujageuzwa kama wakazi wa kisiwa cha Diego Garcia, ...tujiulize kwanini IRAN, MAREKANI na CHINA wanakimbilia kuisaidia Tanzania wakati huu, ...sio kuangalia kiwango cha misaada tu!!!
 
Tulisahau tu kumwomba ile sheria yao inayoshughulikia wala rushwa wakubwa kama wanasiasa, watendaji wakuu wa serikali na taasisi za UMMA.

WildCard,

Hili ndo kubwa zaidi. Ile sheria yao hata tukaitumia tu kwa mda wa miaka 10 basi! Je wangependa kutupa? Na tuko tayari kuitumia?

Ahsante mkuu!
 
Kama unadhani kuna taifa linalotuheshimu sisi wababaishaji(watz), fikiria mara mbili.

Hahahahaha! Yaani nimecheka peke yangu mpaka watu wamenishangaa!!! I love JF......Ni kweli, ukiwa mbabaishaji hakuna mtu atakuheshimu. Sana sana watakuwa wanakukebehi tu!

Mwalimu aliwahi kusema kwamba, umasikini ni mbaya sana, lakini umasikini wa akili ni mbaya zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…