Tonya Mbalela Michael > MICHEZO NA BURUDANI🇹🇿
DONDOO ALICHOONGEA ZAHERA LEO.
1. Nasubiri barua ya kusitisha mkataba wangu, na kama ilivyo taratibu ya mkataba itabidi wanilipe hela yangu.
2. Uongozi na mashabiki wa Yanga SC, lazima wajue matokeo huendana na maandalizi! huwezi kupata matokeo mazuri wakati kuna mambo mengi yanavurundwa na uongozi.
3. Tulipokuwa Gaborone kucheza na Township Rollers, viongozi walitaka tupande gari la timu ya Township, kitendo ambacho sio sawa hata Kelvin Yondani alikasirika sana . . Kiongozi wa msafara hana pesa za kukodi gari nyingine ikabidi nitoe mimi pesa yangu dollar 2000 (kama milioni 4 na laki 5) tukakodi basi lingine.
4. Baada ya mchezo tunarudi johhanesberg kutoka Gaborone, Chakula kikachelewa nikauliza makamu mwenyekiti akasema watakula chakula cha mchana saa 11 halafu usiku hawatokula kwa kuwa hawana pesa! nikawapeleka wachezaji na benchi la ufundi katika mgahawa mmoja kule wakala ilipofika usiku wakala chakula kilichoandaliwa na viongozi.
5. Mchezo dhidi ya Pyramids tulifikia hotel mbovu sana ipo sokoni, chakula kikiletwa wachezaji 6 wanakosa inabidi wasubiri wapikiwe! kesho yake nikamuomba namba Hafidh ya boss wa GSM, nikampigia simu kumueleza maisha tunayoishi. . kesho yake tukabadilishiwa hotel.
6. Baada ya mechi, timu ikiwa inawahi Airport. . wafanyakazi wa Hotel walituzuia kwa kigezo kuwa tunadaiwa pesa ya vinywaji (maji na juice) shilingi laki 5, alikuwepo Makamu mwenyekiti ambaye alinifuata na kuniomba nilipe hiyo pesa watanirudishia nikatoa shilingi laki 5 tukaondoka.
7. Nimetoa pesa nyingi sana zingine waliahidi kunirudishia na wafanye hivo.
8. Yanga SC ni timu kubwa lakini mambo yanayofanyika hayapaswi kufanywa na timu kubwa.
9. Wachezaji niliopendekez wasajiliwe ni Kalengo, Sydney, Balinya, Sibomana, Issa na Molinga basi hao wengine wao ndo walikuwa wananipigia simu na kuniuliza kama ni sawa.
10. Nilipendekeza tuwe na Kindoki, Shikalo na Kabwili, cha ajabu wakaenda kumsajili kipa wa Mbao (Metacha) halafu yule wa Kenya wakawa hawajamalizana na uongozi wa Bandari. . ikabidi nitoe dollar 11,000 kukamilisha usajili wa Shikalo , nashukuru hii nilirudishiwa.
11. Viongozi wa msimu uliopita hawakuwa na nguvu kipesa ila tulifanya sana kazi, tulishirikiana ila uongozi huu wakiongozwa na mwenyekiti ambaye alikuwa anaingilia sana mambo ya ufundi kwa kigezo tu ana taaluma ya ukocha.
12. Mfano mwenyekiti anamkosoa Feisal kwa kumwambia cheza hivi na wewe Makame usipande sana mbele wakati ni tofauti na maelekezo niliyowapa mimi. Mchezo dhidi ya Lipuli mwenyekiti aliingia dressing room na kuongea kama kocha japo sijawahi pangiwa kikosi.
13. Ni lazima Yanga SC kubadili mfumo wao wa uendeshaji klabu ili kuzuia mitafaruku kama hii.
14. Wachezaji wa zamani akiwemo Dante wao ndo walitoa wazo la uchangishaji pesa, cha kusikitisha baada ya makusanyo pesa zile zikaenda kulipa wachezaji wapya wakati kuna wachezaji wa zamani walikuwa wanadai signing fee ya misimu iliyopita. Namuunga mkomo Dante kwa mgomo wake.
15. Najivunia kuiinua Yanga SC, Niliikuta ipo chini leo naiacha ikiwa juu! hii timu ilipaswa kumaliza nafasi ya 7 . .
16. wamenifukuza wakati hakuna sehemu yoyote inapoonesha perfomance ni mbovu, hakuna waliponipa target kuwa timu ifike makundi. . wangeniacha hata michezo 15 ndipo wanihukumu.
17. Timu yoyote duniani inayonihitaji itanipigia simu nami ntafanya nao kazi.