Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

WANANE YANGA KUIKOSA NDANDA SC, KESHO

Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara , Yanga SC kesho wanashuka kwenye dimba la Nangwanda Sijaona Mtwara kuvaana na Ndanda SC huku wakikosa huduma za wachezaji wao wanane kutokana na sababu tofauti. .

Wachezaji hao ni Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Lamine Moro, Juma Balinya, Ali Ali, Maybin Kalengo, Paul Godfrey na Cleofas Sospeter.

Kwa mujibu wa meneja ambaye pia ni mratibu wa timu hiyo Dismas Ten, Feisal Salum amepewa ruhusa maalum ya kwenda kumuuguza mzazi wake, na wengine saba wanakosekana kutokana na kuwa majeruhi.

Azamtv.
 

AMEANZA KAZI: Kocha wa muda wa Yanga SC Charles Boniface Mkwasa #Master(kushoto) akiwa na msaidizi wake Said Maulid #SMG wameanza rasmi kukinoa kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda SC kesho kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara.

Azamtv
 
Baada ya kuanza majukumu yake kwenye kikosi cha Yanga, kocha Charles Mkwasa amewataka wachezaji kutambua ukubwa na thamani ya kucheza Yanga

Mkwasa amewahakikishia wachezaji kuwa kama watajituma na kujitolea kwa moyo mmoja, hakuna sababu ya timu kutopata matokeo mazuri "Niwahakikishie wote mlisajiliwa na Yanga kwa sababu mlionyesha ubora na kuwa na sifa ya kuichezea timu hii. Jukumu langu mimi ni kuwasaidia ili muweze kutimiza malengo ya timu," amesema "Fahamuni mpo hapa kuipigania klabu hii na kubeba vikombe, hilo ndio lengo kuu kwa kila mchezaji anayeitumikia klabu hii" "Tunapaswa kuishi katika utamaduni huu na ili kutimiza dhamira hii ni lazima tuanze kushinda michezo yetu" "Tutakaposhinda kila kitu kitarejea katika hali yake, uwanja utajaa na furaha kwa mashabiki itarejea"

Mkwasa ataiongoza Yanga kwenye mchezo wake wa kwanza kesho dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara

Kikosi cha Yanga kilitua Mtwara jana, leo wanatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo
 
Hamna kocha hapo, Mkwasa hajawahi kua kocha mzuri hata kidogo
 
MWAKALEBELA AFUNGA MJADALA WA MWINYI ZAHERA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuungana ili kuhakikisha timu inafanya vyema na wasikubali kuyumbishwa na yanaoendelea kwenye vyombo vya habari kuhusu kocha Mwinyi Zahera

Zahera ambaye hivi karibuni mkataba wake ulisitishwa na uongozi wa Yanga, umekuwa akifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari akitoa tuhuma nzito kwa uongozi wa Yanga

Mwakalebela amesema Wanayanga hawapaswi kukubali kuyumbishwa, maamuzi yameshafanyika na kinachotakiwa waangalie mbele

Aidha amesisitiza kuwa Yanga haina muda wa kujibu tuhuma zake "Hatuna sababu ya kujiingiza kwenye mijadala ambayo ina lengo la kutugawa. Kwa sasa akili yetu ipo kwenye mechi dhidi ya Ndanda na hatuna muda wa kumjadili mtu ambaye hayupo kikosini. "Zahera hawezi kututoa kwenye reli, tunapambana kusaka ushindi kwenye mechi yetu Mtwara. Alikuwapo kikosini, kama kulikuwa na matatizo kwanini hakuzungumza hadi asubiri alipotimuliwa? Hatupo tayari kumjibu ili asitupotezee dira na mipango yetu," amesema.
 
KILA LA KHERI TIMU YA WANANCHI HAPO 16:00HRS DHIDI YA NDANDA FC.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…