Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Sijawaona wazanzibar wote au washaenda Zenj!?
 
Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa miaka miwili (2) na wadhamini wao kampuni ya GSM, mkataba unaoifanya GSM kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali zenye nembo ya klabu hiyo.

Awali GSM ilisaini mkataba na Yanga kwa ajili ya kuzalisha na kuuza jezi tu, mkataba ambao bado upo hadi sasa. Mkataba huu mpya utawafanya mashabiki na wanachama wa Yanga kupata bidhaa nyingine kama track suits, bukta/pensi, scarfs, t-shirts, vikombe, key holders na vingine vingi.

Eng. Hersi Saidi amesema wanafurahi kupata fursa ya kutengeneza bidhaa nyingine zaidi kwa ajili ya klabu ya Yanga. Amesema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa nyingine tofautitofauti ukiachana na jezi.

β€œTukiwa kama wadhamini tunapenda kuona Yanga ikipata mapato zaidi kupitia nembo yao. Kwa muda mrefu sasa klabu imekuwa ikipoteza mapato ambayo yamekuwa yakiishia kwenye mikono ya watu wachache.”

β€œKwanza fikiria ni jezi ngapi zimeuzwa bila klabu kufaidika na matumizi ya nembo yao? Kumbuka wakati huo klabu ilikuwa inapata wakati mgumu kupata fedha kutoka vyanzo tofauti ili kuendesha shughuli zake za kila siku.”

Ameongeza kuwa, GSM wanataka kuiona Yanga ikiwa imara kiuchumi.

β€œTunahitaji kunufaika pia na udhamini wetu. Unawezaje kuuza bidhaa za klabu wakati mashabiki na wanachama hawafurahishwi na matokeo? Kwa hiyo matokeo mazuri ya timu yataleta chachu kwenye mauzo ya bidhaa za klabu hivyo watafurahia uwekezaji wetu.”

Hata hivyo Hersi amesema mashabiki na wanachama wameanza kuwa na imani na timu yao na kuona sasa inaweza kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara au Kombe la Azam Federation Cup (FA) kwa msimu huu.

Changamoto

Hersi anasema wazalishaji wa jezi feki wamekuwa changamoto kwenye udhamini huo licha ya GSM kuwa na haki ya kuzalisha jezi za Yanga.

Amesema bado kuna mashabiki wananunua jezi ambazo hazina ubora kutoka kwa mawakala wasio na vibali jambo ambalo limekuwa tatizo licha ya wao kuchukua hatua za kisheria kwa wauzaji wa jezi feki.

Kwa mujibu wa Hersi, bado wanatafuta njia ya kuzuia watu wanaozalisha jezi feki na kuziuza lakini pia akatoa wito kwa mashabiki kuacha kununua jezi feki ambazo hazina ubora kwa sababu kuendelea kufanya hivyo ni kuikosesha klabu mapato.

Source: The Citizen
 
YANGA KUZINDUA WEBSITE NA APPLICATION

Uongozi wa Yanga umepanga kufanya uzinduzi mkubwa wa Website na Application ya Yanga Sc.

Afisa habari wa Yanga Sc Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kipo tayari kwa sasa hivyo mashabiki wajiandae ku support timu yao kwa kuweza (kupakua) download app rasimi ya Yanga Sc.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika siku ya Alhamisi Makao Makuu ya Klabu na matukio yote yatakuwa Live kupitia platform mbali mbali za mitandao ya kijamii ya Yanga Sc.

@Yangafulldozz
 
Kwani ikipita na hiyo Timu yako mtani mna maajabu gani!??

Usiache kujilinda mtani Corona inaua

Sent using Jamii Forums mobile app
Lengo kutaka Corona ipite si maajabu tuliyonayo Mtani lengo ipite tupate kukiboresha Kikosi chetu na kufanya mengine mazuri ndani ya Yanga ambayo kwa sasa yamesimama kwa ajili ya hili janga.

Ahsante kwa ushauri Mtani. Najitahidi kadri ya uwezo wangu Mtani.
 
Hivyo we Mtani hutaki Corona ipite eee?
Hahah mtani mie Mwenyewe nataka ipite nishachoka kujifukiza!!

Ukweli kabisa mungu atunusuru ila kila mmoja achukue tahadhari kujikinga maana haitapendeza kusikia mpendwa yetu awaye yeyote amepatwa na maradhi haya,

Nasisitiza tujilinde mtani hasa sisi ambao tunaendelea kutoka kutokana na majukumu ya hapa na pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah nimeamini bado una Imani na timu yako duh!!

Tuombe na nyie muwapo Katika funga msiache kuombea gonjwa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaa. Jifukize tu Mtani usichoke. Teh teh

Yaani acha kabisa wengine tunawafungia ndani ila sisi tunaotoka kutafuta ugali ndio changamoto mno

Ipite hebu mana imefanya mumeanza kumsahau Morisson. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Duh hvi Morrison mtakuwa nae kweli msimu ujao!??Mana kwa janga hli gsm hawatawapa pesa ya usajili.

Hvi kwanini hatupewi tu kombe letu!??

Tukitoka ni mwendo wa Kujipaka Sanitizer,Barakoa za kutosha na tahadhari kama zote...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtani kumbe uko nyuma sana eee Tusiwe naye kwa sababu gani tena wakati tulishamsajili kwa miaka miwili tayari. πŸ˜€

Acha kabisa Mtani hii corona ni balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…