JamboJema
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 1,143
- 209
Sabodo si wa kulaumiwa bali Sheria zetu. Kuulizana asili ni ubaguzi ambao tumekuwa tukiupinga miaka yote. Kwa sheria zetu, mtu kuwa na asili ya asia haimfanyi awe nusu mtanzania, na mwenye asili ya umatumbi kuwa ndio mtanzania kamili. Nasema ilaumiwe sheria kwa kuruhusu kuunda vitabaka vya watanzania. Leo 'mhindi' akipata uraia ataenda kuoa/kuolewa India na mhindi huyo wa kitanzania atakuwa na haki ya kumuombea uraia mme/mke wake huyo. Hapo tayari wahindi wawili wenye 'karatasi' za utanzania wanapata stahili zote za mtanzania. Mmatumbi ambaye kwa bahati mbaya hana hata kijikaratasi cha kuutetea utanzania wake anabaki kulalamika.
Ningekuwa mie ndo nina madaraka katika hili, utanzania wa mtindo huu ningeukataa. Bora nitoe muitacho permanent residence na sio uraia kwa watu wa jinsi hii. Tunakwisha as a country tukitazama! Tuzirejeree sheria zetu za uraia.